Nimefuatilia sana hili zao hapa Tanganyika, wote wameotesha kama mapambo, ila wenzetu hapo jirani wamelima kwa kumaanisha. Ukianza kulima zao hili inabidi ulime kwa scale kubwa, ni kama ilivyo kwa karanga miti, hapa bongo hazitiliwi maanani kabisa ila zinalipa vizuri. Ukienda Saharani Tanga mission kuna kilimo hiki tangu 1946, Karanga miti a.k.a macadamia humea pia Mby na kwingineko.
Kule nchi za middle east, hasa Israel, kuna kuna mizeituni balaa. Mafuta ya mzeituni ni biashara kubwa sana. pale SUA ktk kitalu cha jamaa miche ipo na inanunuliwa,ila hakuna mashamba ya mfano ya mazao haya mawili.