Wewe ni begginer, usiwaze mambo makubwa ya green house kwa sasa... kwa sasa njoo kwenye kilimo tu cha msimu ambacho kitakuongezea huo mtaji wako.. Kama unaweza angalia ukanda wa Songwe, au Ruvuma..huko mvua ni za uhakika na unaweza kulima mazao kama mahindi, maharage na soya kwa bei nzuri,,..Mashamba yanapatikana kuanzia 40,000 kwa kukodi..kuna gharama nyingine kama za kuandaa shamba na kununua mbegu,mbolea na vibarua..ila mwisho wa siku inalipa kwani ukanda huu mvua ni za uhakika.. Muhimu ni usimamizi..usije ukatuma hela ukiwa mjini uwe mkulima wa simu..utaliwa na ukichukie kilimo..jikane nafsi,piga kambi hiyo miezi yako mitatu utaona mafanikio..au kama huwezi kupiga kambi hakikisha unakuwepo wakati wa hatua muhimu mfano kupanda, juweka mbolea na palizi..baada ya hapo unaweza kuweka kijana anakuangalizia tu kama kutakuwepo na magonjwa na wadudu anakupa taarifa wakati unaendelea na mambo yako mjini... Pia uwatumie wataalamu wa kilimo wa eneo husika...Nenda idara ya kilimo halmashauri sema unaomba ushauri kwa mtaalamu wa mazao na utaongea nae kupata picha ya nini ufanye kwa eneo husika..Vijana wa kisasa lazma tufanye vitu kitaalamu na siyo kwa mazoea... Karibu shambani