Kilimanjaro, Uhuru Peak 5895 in 1 day | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimanjaro, Uhuru Peak 5895 in 1 day

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Eeka Mangi, Jan 27, 2009.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mtalii toka Norway ambaye ni mpanda milima wa siku nyingi amejaribu kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku moja. Mtalii huyu alianza safari yake leo asubuhi tarehe 27/1/09 saa 11.30 pale Umbwe gate na ametumia masaa 7.19 hadi uhuru. Nitoapo taarifa hii ni kuwa ameshafika Millenium camp njiani kuja Mweka gate. Anatazamiwa kuwa Mweka gate saa yoyote kuanzia 10.30 jioni hii. Ninaelekea Mweka gate na nitawaletea yatakayojiri huko. Kwa wanaojua Kinorwegian tembelea www.jarletraa.no
   
 2. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Can it be done using the Machame route? What's the guy's name?
   
 3. Piemu Esquire

  Piemu Esquire Member

  #3
  Jan 27, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mangi hizo ni fix wewe uliwahi kuupanda mlima huo?Sidhani kama kuna mtu anaweza kuupanda kwa marathon.HAKUNA BWANA
   
 4. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mh, hard to believe it
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli itakuwa vema wakimpima ili kujiridhisha kwamba hajatumia madawa ya kuongeza nguvu (eg steroids). Siku hivi kuna udanganyifu mwing sana duniani kisa umaarufu/kuweka record! Tumesikia yaliyompata mwanariadha (The three-time Olympic gold medalist, and the world's fastest mom) Marion Jones wa USA.
   
 6. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Thats true,,,, ametumia masaa 10 na dakika 46. Hata hivyo huyu hajavunja rekodi. Kuna Muitaliano aliyjulikana kwa jina la Bruno aliwahi kupanda Kilimanjaro Marangu route kwa masaa 8 na dakika kadhaa. Pia kuna Mtanzania aitwaye Simon Mtui aliwahi kupanda Kilimanjaro via Umbwe route kwa masaa 8. Huyu anaitwa Jarle Traa na kama nilivyosema hapo kabla kama Kinorway kinapanda tembelea tovuti yake www.jarletraa.no huko utaona route na muda aliotumia.
   
  Last edited: Jan 28, 2009
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Good info' for future references
   
 8. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Baada ya watu mbalimbali kubisha kuhusu hili, nilifanya jitihada mbalimbali za kukusanya data kuhusu ni nani amefanya nini na wapi katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
  Niliyoyapata ni kama ifuatavyo:-
  Mtu aliyepanda Kilimanjaro kwa kasi (fast ascent)kuliko wote ni Bruno Brunod wa Italy. Mwaka 2001 alipanda mpaka Kileleni mita 5895kwa masaa 5 dakika 38 na sekunde 40 kupitia njia ya Marangu. Hii ilithibitishwa na Uongozi wa Kinapa, Ingawa kuna madai kuwa kuna Sean Burch wa Virginia anayedai kuwa alifika kileleni kwa masaa 5:28 Juni 7, 2005 na Christian Stangl wa Austria anayedai pia alifika kileleni kwa kutumia 5:36 October 2004 ingawa hii haikudhibitishwa na Kinapa. Bruno Brunod alimalizia kuweka record kwa kushuka toka Kileleni hadi Marangu gate kwa masaa 2:56:12 na hivyo kufanya jumla ya masaa 8:32:52

  Anayeshikilia rekodi ya kupanda na kushuka kwa kasi (Fast ascent and descent)ni Mtanzania aitwaye Simon Mtui (Nomad) aliyepanda na kushuka kwa masaa 8:27 kupitia njia ya Umbwe na kuteremkia Mweka December 26, 2004. Pia alijaribu kuvunja rekodi yake lakini akafikia kupanda na kushuka kwa 9:19 tarehe 22 February 2006 inagawa pia alikuwa na matatizo ya kuharisha, dakika 3 za kujipiga video yeye peke yake na dakika 2 za kutapika. Anabakia kuwa mtu mwenye kasi zaidi kwa kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro.
  Mwanamke ambaye anshikilia rekodi ya kupanda kwa kasi Kilimanjaro ni Rebecca Rees-Evans toka UK aliyetumia masaa 13:16:37 kupitia njia ya Marangu.

  Na sasa huyu aliyepanda kupitia njia ya Umbwe na kuteremkia njia ya Mweka tarehe 27 January 2009 Jarle Tra toka Norway kwa kutumia masaa 7:19:34 na kutumia jumla ya masaa 10:46. Kwa Uhakika zaidi tembelea www.jarletraa.no kama kinorg kinapanda au hata kuambulia picha zake.
   
 9. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #9
  Jan 30, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Kama unataka kupanda milima,lazima uwe na afya nzuri. Pia haya mambo bora uwaachie vijana. Ukianza kusema,'' Mtoto wa miaka 15 ameweza kuupanda mlima,kwa nini mimi mwenye miaka 70 nishindwe?'',utaingia hasara. And yet ukienda Marangu kutazama records za watu wanaoupanda ule mlima,utashangaa kuona umri mkubwa wa watu wanaoupanda ule mlima. Niliona mtu mwenye miaka 72. Kumbuka maneno ya Sun Tzu. Alisema words to the effect ,kwamba,''inexperienced Generals wanapigana vita,halafu,baada ya vita,wanatizama kuona kama wameshinda;lakini experienced Generals wanashinda vita kwanza,halafu ndio wanapigana."
   
Loading...