KILIMANJARO: Milioni 100 zaporwa duka la kubadilisha fedha

Kagondo

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
296
79
Watu wasiojulikana wamevamia duka la Chase Bureau De Change linalotoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni, mali ya Ashraff Khan na kuiba milioni 100 huko wilayani Moshi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana, baada ya wezi hao kuvunja dirisha la chuma na kuingia sehemu ya kutunzia fedha na kufanikiwa kuiba shilingi za Tanzania, Kenya, na Euro (jumla milioni 100), huku mlinzi wa zamu wa duka hilo akitoweka na kuelekea kusikojulikana.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, huku akitoa taarifa za kuwepo kwa wizi kama huo dukani hapo mwaka 2005, ambapo amesema watu wenye silaha walivamia duka hilo na kupora milioni 44 mchana wa saa sita.

Aidha, kamanda Mutafungwa, amebainisha kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwepo kwa dalili za njama za ndani zinazojumuisha kutoonekana kwa mlinzi sehemu ya tukio, huku akiongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea dhidi ya tukio hilo.
 
Katika watu ambao sio wa kuwaamini ni.pamoja na mlinzi wako. Hilo lilikuwa ni dili.
Siku hizi hakuna wizi ambao hauwausishi wahusika wa ndani, angalia hata kwenye mabenk utakuta Polisi na Teller lazima wahusike kwenye huo wizi
 
Watu wasiojuikana wamevamia duka la Chase Bureau De Change linalotoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni, mali ya Ashraff Khan na kuiba milioni 100 huko wilayani Moshi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana, baada ya wezi hao kuvunja dirisha la chuma na kuingia sehemu ya kutunzia fedha na kufanikiwa kuiba shilingi za Tanzania, Kenya, na Euro (jumla milioni 100), huku mlinzi wa zamu wa duka hilo akitoweka na kuelekea kusikojulikana.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, huku akitoa taharifa za kuwepo kwa wizi kama huo dukani hapo mwaka 2005, ambapo amesema watu wenye silaha walivamia duka hilo na kupora milioni 44 mchana wa saa sita.

Aidha, kamanda Mutafungwa, amebainisha kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwepo kwa dalili za njama za ndani zinazojumuisha kutoonekana kwa mlizi sehemu ya tukio, huku akiongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea dhidi ya tukio hilo.
Mlinzi anapata 200,000 analinda 100,000,000 well done Mlinzi akale Pension huko Watakua walikua 3 kila mmoja 33.3Million Mlinzi atafanya biashara nzuri sana aje Dar huku nitampokea na Kumshauri bishara ya kufanya ndo inatakiwa muwe hivi siyo muhindi tuu hata kampuni za kijinga Jinga Wapige 200Million au zaidi Sepa nchi hii yaani unalinda huku una process visa
 
Mara nyingi walinzi uwa wanalipwa na kampuni za ulinzi, kwa hiyo ulipwa na kmpuni za ulinzi
 
Inahitaji akili nje ya hizi za kawaida kusifu jambo lolote la wizi.Hivi kuwa na 100M inamaana mlizi alipwe kama 5M ndio ataridhika am? Na nani kasema kuwa 100 M ni faida? Unajuaje kama kwenye 100M mtaji hauwezi kuwa 90M na faida ikawa 10M?
Tuache ushabiki usio na tija. Hao wanoiba huko kesho wakikosa hizo mia wanshuka hadi kwenye bodaboda yako, simu tv nk.
 
Watu wasiojulikana wamevamia duka la Chase Bureau De Change linalotoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni, mali ya Ashraff Khan na kuiba milioni 100 huko wilayani Moshi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana, baada ya wezi hao kuvunja dirisha la chuma na kuingia sehemu ya kutunzia fedha na kufanikiwa kuiba shilingi za Tanzania, Kenya, na Euro (jumla milioni 100), huku mlinzi wa zamu wa duka hilo akitoweka na kuelekea kusikojulikana.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, huku akitoa taarifa za kuwepo kwa wizi kama huo dukani hapo mwaka 2005, ambapo amesema watu wenye silaha walivamia duka hilo na kupora milioni 44 mchana wa saa sita.

Aidha, kamanda Mutafungwa, amebainisha kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwepo kwa dalili za njama za ndani zinazojumuisha kutoonekana kwa mlinzi sehemu ya tukio, huku akiongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea dhidi ya tukio hilo.

Insurance Company italipa
 
Ingawa si vyema kuyafurahia mateso ya mwanadamu mwenzako lakini matendo ya hawa ndugu zetu wenye asili ya asia dhidi yetu sisi weusi...yanatufanya tufurahie machungu yao.......

PENYE NJAA HAKUNA AMANI......
 
Back
Top Bottom