Kilimanjaro kinara uzalishaji wa mihadarati

Kilimanjaro kinara uzalishaji wa mihadarati

Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,150
Reaction score
14,730
Mkoa wa Kilimanjaro umetajwa kuwa ndio unaoongoza nchini kwa uzalishaji wa mihadarati ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Kamishna wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya (DCEA), Mihayo Msikhela.

Kasema kuwa katika Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Same ndio inayoongoza kwa uzalishaji huo wa mihadarati.

Msikhela aliyasema hayo katika operesheni ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya iliyofanyika leo wilayani Same. Alisema kuna mikoa mitano inayoongoza kwa kilimo cha mihadarati nchini ikiwemo mikoa ya Kagera, Songwe na Tanga, lakini wilayani Same katika maeneo ya Chome na Suji ndio yanayoongoza kwa kilimo hicho cha mihadarati…
 
Back
Top Bottom