illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Leo alfajiri wakati nikielekea kutafuta mkate nimekuta vurugu kubwa maeneo ya Namanga Dar es Salaam ambapo mgambo wa jiji wakishirikiana na kikosi maalumu walikuwa wanavunja lile banda la chips na ile nyumba ya uwani huku ikiharibu mali kwa kutumia mashoka na zile nyundo zenye kilo nyingi.
Pale huwa wanauza chips lakini ukipita jioni utakuta magari ya kifahari yamekuja kununua chips kiasi cha kusababisha eneo hilo kuwa na msongamano mkubwa sana. Baada ya kuangalia vizuri nikagundua kuna vijana wa Makumbusho wamejaa na wenyewe wanafanya uharibifu huo nikaangalia huku nikaona mabaka mabaka kama ya jei wii duh nikajua tu hapa kuna ile oparesheni ya ngada inaendelea kimya kimya.
Kwahiyo wale wa chips kwa Edo poleni hayo ndo yaliyojiri mtu anatoka Mbezi anakuja kununua chips Namanga halafu hashuki kwenye gari analetewa ndani ya gari.
Duh Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!!