Kilichopo Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichopo Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 5, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kilichopo Zanzibar hivi sasa ni UZANZIBARI kwanza au niseme Zanzibar kwanza halafu Tanzania au Muungano.
  Ikiwa kuna tishio huko Mombasa kuwa hawatapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wa Kenya kwa sababu Mombasa si sehemu ya Kenya kutokana na nyaraka za zamani ,tunaweza kusema Mombasa ni sehemu ya Zanzibar na hivyo kuwa ni sehemu ya Tanzania kwa sababu za Muungano.

  Kwa WaZanzibari ,wao wapo na nchi yao na katika jambo lolote lile wanahakikisha Zanziabar inakuwepo na kubakia kama Zanzibar na serikali yake,Raisi wake ,na kila kitu kimamlaka inabakia nchi kamili na kuhakikisha inarudi katika UN.

  Je ni nchi gani ina ofisi mbili za UN ,kisheria hakuna ,inakuwaje Tanzania bara (Tanganyika) kuna ofisi ya UN na Zanzibar kuna ofisi ya UN ? Hivyo tunakokwenda ni kuwa kila mmoja kuwa na nchi yake ,Tanganyika kwao na Zanzibar kwao na hili halitaki kuwepo na ugonvi wala chuki bali kama tulivyoungana kwa furaha na bashasha ndivyo hivyo hivyo tutakapohitimisha kwa hayohayo ya furaha na amani kabisa. Yote ni hiyo KATIBA IJAYO.

  Sasa tatizo ni huko Tanganyika ,kwani kama tatizo litatokea katika KATIBA mpya na kukosa utatuzi itamaanisha ndio mwisho wa Muungano.

  Je Tanganyika kutakuwa salama ? Jawabu kwa watanganyika wengi wanahoji na huko Zanzibar kutakuwa na amani ?

  Hali ilivyo kwa Zanziabar bila ya shaka yeyote ile amani itakuwepo na ndio hii ambayo inaendelea kuundwa kwa kuwekwa na kurekebishwa kwa Katiba ya Zanzibar ,bomu linalochemka ni huku Tanganyika ambako KATIBA iliyopo imekaa kimuungano na nchi nyingine.

  WaTanganyika wamejitayarisha vipi ikiwa Muungano utavunjika ? Kwani serikali iliyopo ni ya Muungano ,haiwezekani ikaendelea kuwepo ikiwa Muungano haupo. Nionavyo kuna umuhimu wa kuunda serikali ya Tanganyika .
   
 2. F

  Falconer JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Shabash, umesema mkuu. Hivi ndivo inavotakikana kabisa. Mwakilishi wa Zanzibar klatika baraza aliuliza hizi, "Juzi kulikuwa na sherehe za miaka hamsini wa UHURU wa TANZANIA BARA, jeee, kuna nchia inaitwa TANZANIA BARA?. Si mimi nawaambia siku zote hizi, mambo yenu ni vioja duniani eti miaka hamsini ya TANZANIA BARA, hhahahahahahah. Bado hii ni nchi ya tatu sasa.
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwevu wapi mpiganaji?? Tumekukosa siku nyingi, tunahitaji nguvu yako katika harakati ya kuondokana na mfumo tawaliwa na tawala wa Muungano!
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tahadhari ahali yangu.

  Mwiba unawachoma huo.

  Swadakta kwa maneno yako murua yasio na shaka ndanimwe.

   
 5. c

  chilubi JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 3,037
  Likes Received: 1,018
  Trophy Points: 280
  Goma hiloooo,,,, hehehee!! Wa "tanzania bara" wanakazi kweli kweli, na apo ulipogusa kuwa mombasa wanataka kugoma kupiga kura wakitaka wawe chini ya dola ya zanzibar mbona ni habari yamshtuko?!! :D kaaaazi kweli kweli,,, ila kwa nnavyojua mimi kuwa mfalme alizituoa/kuziuza izo sehemu za mombasa, Lamu na nyenginezo, mana wakisema ivo basi kanda ya pwani yote ya tz bara ni ya zanzibar,,, jeee patatosha apo?!!
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapo Mombasa kuda data zinazoonyesha Mombasa ilitolewa kwa mkataba wa miaka mia na mahesabu yanaonyesha imeshatimia ,aidha Tanzania au Zanzibar ukichanganya na wazalendo wa Mombasa ndio wenye mpini kuliko serikali ya Kenya ,Kimataifa(UN).
   
 7. y

  yaya JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nimejaribu kuisoma thread yako zaidi ya mara mbili, lakini nimetoka kapa. Nimeshindwa kabisa kuelewa ulitaka kusema nini hasa kimantiki?
  Uzanzibari kwanza kuliko u-Tz, kwangu mimi si kosa ni sahihi kabisa.
  Lakini kuhusu Mombasa badala ya kuzungumzia u-Zanzibari kwanza kama ulivyosema awali, wewe huyo huyo unazungumzia u-Tz kwanza!!!??? Hizo nyaraka si zilikuwa kabla ya muungano? Kwanini isiwe Mombasa ni ya Zanzibar lakini si ya Tz?

  Unasema Zenj haitafutika, ulishawahi kusikia kuna jaribio la kuifuta? Au ndiyo kuweweseka huko? Unaogopa kivuli chako mwenyewe?

  Unazungumza kwa kujidai uwepo wa ofisi mbili za UN, Moja Zanzibar na nyingine Dar na kwamba hakuna tena pahala pengine duniani!! Sina uhakika, lakini mbona hujidai kwamba kuna wawakilishi wawili katika UN, mmoja kutoka TZ na mwingine kutoka Zanzibar?? Au huyo wa Zanzibar hayupo kwa sababu hawezi kutambulika kisheria??

  Ushauri wangu kwako, dhibiti moto unaounguza nyumba yako kwanza, usikimbilie kuzima kwa jirani wakati kwako kunateketea!!!
   
Loading...