Kilichonisikitisha apple store. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichonisikitisha apple store.

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Sniper, Jul 11, 2011.

 1. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mimi ni mtumiaji wa apple products (iphone, ipod ...), leo nlikuwa nabrowse appstore, nkasearch "swahili", then nkapata results apps za kiswahili, hicho kilinifurahisha, lakini kilichonisikitisha ni kwamba karibia apps zote zililzokuja zilikuwa ni za wenyetu wakenya.

  Wakenya wanatengeza kamusi za kiswahili wanaziuza online, wakati tunaokijua vizuri kiswahili tupo tu tumelala.
  Watanzania tuamke tuchangamkie hizi fursa za technolojia, kuna mambo mengi sana ya kuyaweka kwenye platform za simu (android/iphone/symbian...), nawasilisha.
   
 2. Millah

  Millah JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pia inawezekana hawatengenezi Wakenya, lakini wanaotengeneza wanahusisha Kiswahili na Wakenya. Kwa mfano App ya iPad, iPhone na iPod inayojulikana kama Learn Kenyan Swahili Vocabulary imetengezwa na Innovative Language Learning ambapo Developers hawa sio Wakenya ingawa upo uwezekano kuwa kuna Mkenya wanafanya kazi nae. App nyingine ni Basic Swahili ambapo ina bendera ya Kenya lakini Developer ni Nana Sarpong na haki miliki ya app hii ni ya lkambpuni ijulikanayo kama Nkyea Learning System ambayo ni kampuni iliyopo Ghana. Pia uTalk HD Swahili imetengenezwa na Euro Talk pia ina rangi za bendera ya Kenya.

  Kwa hiyo si kwamba Wakenya wanatengeneza apps za Kiswahili bali Ulimwengu unakihusisha Kiswahili na Kenya kuliko Tanzania. Hili nadhani ndio tatizo Mkuu. Kwa mawazo yangu ni kwamba Kenya walitutangulia sana kwenye utalii wakati ule sisi tulupokuwa tumen'gan'gania "Ujamaa na Kujitegemea" ndio maana kujulikana kwao kunaleta matokeo haya. Kuna baadhi ya watu wanadhani Kilimanjaro iko Kenya kwa vile wanautumia katika matangazo yao ya Utalii.
   
 3. zolong1

  zolong1 Senior Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 143
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hata ovistore ni hivyo hivyo.Mfano wa app ni tuvitu by shimba technologies Ltd kutoka kenya.
   
 4. bwax

  bwax Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  tatizo lililopo kwa watanzania ni kwamba wengi wao hawataki kujishughulisha kwenye hizi kazi za kutafsiri kama hakuna malipo.

  Kwa sehemu kubwa kutafsiri lugha huwa hakuna malipo zaidi ya kuwa acknowledged.

  Kenya wanafanikiwa kwenye hili eneo kwa sababu wanaangalia baadae atafaidika nini kama kwa sasa anatoa huduma bure.

  Seroius we need to change on this.
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nchi za nje wanajua Kiswahili kinaongelewa Kenya. Hata Prince Williams alikuja kusoma Kiswahili Kenya. Mlima Kilimanjaro unajulikana upo Kenya. Google yenyewe version yake ya Kiswahili inmekaa Kikenya kenya. Ukianagalia hata makampuni ya kimataifa ya habari kwa lugha ya Kiswahili yame base Kenya. Al Jazeera nao watafungua TV ya Kiswahili Kenya. Nimesikia Joomla nao watakuwa na version ya Kiswahili lakini cha Kenya.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  hiyo ya joomla nakumbuka wakati najifunza katika community database ya watalam kwa east africa wataalam walijiondikisha kwamba wana uzoefu na joomla kwa east arfica ni wakenya. Ingawa najua na watanzania wapo lakini hawajajitangaza au hawajui kujitangaza au hawaoni umuhimu waujitangzaza tena free.

  So unaweza kuona kuwa wenzetu wakenya wanajua kutumuia every opportunity kujiweka katika nafasi bora ya ushidndani. Sisi ni kwenye siasa tu kenya ndio wanakuwa 2nd best.
   
 7. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mkuu.. 100% wakenya ukiwapa upenyo wanafanya kweli..Jamaa wametuacha na wanaendelea kutuacha.. Hii South Sudan ..itawainua sana..Yaani sijui watanzania tuna matatizo gani.. yaani muda wote tunaishia kulaumu tu..Kuna watu wengi Bongo wameenda shule ya nguvu..lakini kama tumelogwa..
   
 8. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Waache Wakenya watuzidi akili ,wa TZ hata umeme umetushinda sasa nani atakuja kuwekeza hapa bongo ukweli unabaki palepale Nairobi ni hub ya EA,kwa huku chini ya ikweta nafikiri ni SA peke yake ambayo inaizidi Kenya,wacha tubaki kuulamu ukame kwa kukosa umeme badala ya kufikiria njia mbadala za kuondoa tatizo la umeme,tokea enzi za Mzee ruksa hili tatizo lipo kila anayekuja anategemea mvua,Kenya oyee (kwa hasira)hata kama siipendi Kenya lakini naikubali huo ndio ukweli na uwazi ,kwaherini
   
Loading...