Kilichomwangusha Sumaye chatajwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichomwangusha Sumaye chatajwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Oct 4, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SIASA za makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimetajwa kuwa chanzo cha kuangushwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kupitia Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara.

  Sumaye ambaye anatajwa kuwa ana nia ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, alishindwa na Dk Mary Nagu ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji).

  Katika uchaguzi huo, Sumaye alipata kura 481 dhidi ya Nagu, aliyepata kura 648.

  Mbali na Sumaye, wajumbe wengine waliokuwa wakimuunga mkono akiwamo Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Goma Gwantu, pia walishindwa katika uchaguzi huo.

  Dalili za kushindwa kwa Sumaye, ambaye alikuwa akiungwa mkono na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM wa wilaya hiyo, zilianza kuonekana wiki moja kabla ya uchaguzi huo.

  Kambi ya Dk Nagu ambayo inatajwa kwamba inaungwa mkono na kambi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, ilionekana kuwa na “ushawishi” mkubwa katika vikao vya kamati ya siasa ya mkoa na kwenye Kamati Kuu ya CCM.

  Hali hiyo, ilitokana na ukweli kuwa Dk Nagu kama taratibu ambazo zilihitajika, hakupewa baraka na kamati ya siasa ya wilaya hiyo, kugombea kwa kile ambacho kilielezwa kukwepa mpasuko wa CCM Hanang' na pia kumpa heshima Sumaye.

  Hata hivyo, habari zimeeleza kuwa tofauti na msimamo wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Manyara, ilionekana kumuunga mkono Dk Nagu hasa kutokana na ukweli kuwa karibu nusu ya wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wagombea.

  Kikao cha kamati ya siasa ya mkoa, licha ya kurejesha jina la Dk Nagu pia, kilipendekeza kuondolewa majina ya wagombea kadhaa katika wilaya ya Hanang' likiwamo jina la Mwenyekiti wa wilaya hiyo, Goma Gwaltu ambaye alikuwa kambi ya Sumaye.

  Taarifa za kupendekezwa kuondolewa majina ya wanaomuunga mkono Sumaye, zilitolewa na baadhi ya wajumbe wa Wilaya ya Hanang’, lakini hata hivyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndeng'aso Ndekubali alizikanusha.

  “Kamati ya siasa ya mkoa ni kikao cha siri na nadhani ni mapema mno kulalamikia suala hilo, ni vyema wakasubiri uamuzi wa juu, ” alisema Ndekubali.

  Hata baada ya kurejeshwa majina na Nec, ilibainika kuwa wagombea ambao Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, iliwapa alama za chini, wamerejeshwa katika mchakato wa uchaguzi.

  Dalili za kuanguka Sumaye, pia zilijionyesha siku ya kupiga kura, ukumbini na nje ya ukumbi kutokana na wajumbe waliokuwa wanamuunga mkono Dk Nagu kuwa na uhakika mkubwa wa ushindi.

  Wakati wa kujieleza ili aombe kura, Sumaye ambaye alionekana kama tayari amebaini nguvu ya Dk Nagu, alieleza kushangazwa na uamuzi wa Dk Nagu kugombea nafasi hiyo, hali ya kuwa ni waziri.

  Sumaye, pia alikemea kile alichodai kuwa ni rushwa kwenye chaguzi za CCM na kuahidi kama akichaguliwa, angeshirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha anawachukulia hatua kali watoa rushwa.

  Awali Dk Nagu katika maelezo yake, alitumia fursa ya kuomba kura kukanusha kuwa anatumiwa na kundi la Lowassa ili kumkwamisha Sumaye.

  Dk Nagu alifafanua kuwa yeye kama Mbunge wa Hanang’ na Waziri, kamwe hawezi kutumiwa na kundi fulani kwa masilahi ya makundi kwani hata yeye ana sifa za kuchaguliwa.

  Wakati wa maswali, Dk Nagu hakuulizwa wakati Sumaye aliulizwa maswali matatu ambayo aliyajibu kwa ufasaha, lakini hakuchaguliwa.

  Mwenyekiti wa CCM aliyeshindwa, Goma Gwaltu, alieleza kupinga mambo kadhaa yaliyokiukwa katika uchaguzi, lakini hata hivyo, alisisitiza kujiandaa kutoa tamko rasmi.

  “Nitazungumza siku si nyingi kuelezea uchaguzi huu,” alisema Gwaltu.

  Naye Sumaye kwa upande wake, alisema anakusudia kuzungumzia yaliyojiri katika uchaguzi huo hivi karibuni.

  “Naomba uwe na subira, nitawaita wanahabari na tutazungumza. Leo (jana) nimepigiwa simu na waandishi kama 50, wote nimewaambia kuwa nitazungumza siku chache zijazo,” alisema Sumaye.

  Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Rose Kamili ambaye kwa muda mrefu alikuwa diwani kwa tiketi ya CCM kabla ya kuhamia Chadema, alieleza kuwa Sumaye aliangushwa kwa nguvu ya fedha.

  Alisema kuwa kitendo cha Sumaye kutajwa kuwa anataka kuwania urais katika uchaguzi ujao ndiyo sababu ya kutoswa katika uchaguzi huo ili kupunguza ushindani.


  Kwa upande wake Gwaltu alisema kilichomwangusha Sumaye ni makundi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.

  Alisema kuwa makundi hayo ambayo yameanza kujipanga kwa ajili ya kushinda katika kinyang’anyiro cha kuwania urais, yalifanya kila njia kuhakikisha kuwa Sumaye hapenyi katika hatua hiyo, lengo likiwa ni kufanya upinzani kuwa mdogo 2015.

  Kada mkongwe wa chama hicho ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Basotu, Samwel Kawoga alisema kuwa makundi hayo yalianza kuonekana wazi siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

  Alisema kuwa makundi hayo ni pamoja na yale yanayoongozwa na makada wa chama hicho wanaoutaka urais na mengine ni yale yanayoibuka kila unapofanyika uchaguzi ndani ya chama hicho.
   
 2. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Je, source ya hii ni bomu alilotaka kulipua Mh. Sumaye au imetoka wapi?
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  kama jk ameweza kuwa rais..sumaye kuwa rais pia.... wa ccm lakini sio wananchi
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama wana fanya fair hawa jamaa. Wanashindana kuiua CCM tu!

  Sumaye naye ana tamaa ya madaraka. Amekuwa Serikalini kwa muda mrefu, Waziri Mkuu miaka 10 bado anang'ang'ana na siasa! afadhali amefanywa mbaya.

  Watanzania siyo wajinga kama wakati wake!
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Licha ya kuwamo kwenye kundi la wanaowania urais 2015, pia matamshi yake ya kukemea rushwa ndiyo yamechangia zaidi. Kwani chama chetu hatumuhitaji mtu atakayeondoa mzizi ulioshikilia chama (RUSHWA).
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hata mimi najiuliza kama alikuwa waziri mkuu tena 10 years ...anataka kufanya nini cha tofauti tena sasa kwenye position za chini cause hawezi kurudi tena kwenye ile senior position... au anataka akifa mwili wake uagwe mjengoni? maana hicho tu ndo atakosa...aibu sana ndio maana mimi sipendi wanaume wa nchi hii wanafiki wanafiki sana
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mikikimikiki ya 2015 hayoooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Sasa umemkwapu wa nchi gani Smile?

  Anyway, mimi pia sidhani kama kuwachukia ni issue. Issue ya msingi ni kuwajua na kuwaelewa vizuri. Alistahili alichokipata. kwa sasa anaweza kulalama kuwa aliangushwa na kambi ya Lowassa, but mwisho wa siku waliopiga kura ni wanachama wa ccm wa eneo husika, siyo waliotoka Monduli.

  WACHA WAFU WAZIKANE WENYEWE!
   
 9. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Utawapenda to Smile ila bado hujampata yule anayeendana na wewe. Yaani utafurahi mwenyewe kwa jinsi tulivyowazuri
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  teh nimebanana tu hapa hapa si unajua tena moyo
  back to topic...acha abaki akimlaumu lowasa..wazeee hawa bwana ?
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Sumaye CCM hawakutaki ingawa wewe unawataka, nenda Chadema.
   
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  tupo kisiasa hapa bwana..jadili kuhusu kupigwa chini kwa sumaye na anavolialia kwamba lowasa ndo reason eti!
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Akienda chadema atachelewa sana, manake atakuwa chini ya uangalizi kwa miaka kama 10 hivi!
   
 14. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  CCM ni chama cha fitina na kupika majungu hii ni sifa kuu ya CCM, na hii ni tabia kubwa ya wanachama wa ccm, hivyo sumaye asilalamike bali akae kimya kwani haijui CCM na kazi zake? Pole baba tulia tuli.
   
 15. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Who taold u CDM wanamtaka Mzee Zero?Mpelekeni kwa mkopo CCM B- CUF.:hand:
   
 16. l

  luckman JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  nimeipenda hii
   
 17. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 8,911
  Likes Received: 12,091
  Trophy Points: 280
  Ukweli husemwa:

  Rais Mkapa alishawahi kupiga kelele akisema Nchi haiwadhamini wazee waliolitumikia Taifa kwa ngazi ya juu kwa vile hawaombwi kutoka ushauri. Mkapa alinukuliwa akisema, 'kuna dhana ya kuwa ukizeeka na akili inakuwa imezeeka'.

  Kwa mtaji huu, ninafikiri alikuwa sahihi,inajidhihilisha akili ya Sumaye nayo imezeeka, anahitaji washauri badala ya kuombwa kushauri. CCM na Serikali yake imempa kisogo.

  Kama kawaida ya wanasiasa wa Tanzania, atakuja mbele ya wanahabari na sababu kibao zitakazo ambatana na lawama kwa watu au kikundi fulani ndani na nje ya CCM.

  Kwani hatosheki na pesa zetu nyingi anazochukua kama posho. Huu ni ulafi wa hali ya juu.
   
 18. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kilichomwangusha Sumaye ni sanduku la kura asitafute mchawi.
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mbona Mpendazoe na Shibuda mmewachukuwa.
   
 20. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Namshsngaa Sumaye amesahau nini? Au ile jina ya rais na kupewa PhD za vikaoni?.............
   
Loading...