umenena vema, yani siku hizi ndoa zimekuwa kama ni fashion tu watu wanaagalia zaidi harusi na si ndoa, wasichana wanwaza na mie niolewe nisionekane kuwaniko nyuma, akili yote ikiwa kwenye siku ya harusi tu, na si maisha baada ya hapo, matokeo yake ukifika ndani ya ndoa ukakutana na misukosuko kidogo tayari ndoa inakuwa ndoana, tunasahau neno la Mungu linasema mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake, mm naamini pamoja na kuwa mwanaume ni kichwa cha familia, Mungu alitupendelea wanawake akatupa uwezo mkubwa wa kumiliki familia zetu na ndio maana mwanamke asipokuwa stable kwenye nyumba ndoa lazima itayumba, ila kwa wanaume kama uliamua kuoa mana yake huyo ndiye mwanamke uliyemchagua hata kama utakta anamapungufu ni kazi kwako kumrekebisha kwa upole, chukulianeni mizigo yenu, upendo, msamaha viwe kama sala kwenu kulala na kumka na mtu maisha yako yote si kazi ndogo, lakini yahitaji uvumilivu na kuchukuliana, neno linasema enyi waume wapendeni wake zenu kama kristo alivyolipenda kanisa, palipo na upendo wa kweli amani na furaha itatawala, mana kama mmekuwa mwili mmoja sidhani kama mtu anaweza akauchukia mwili wake au akautesa, jamani tusifike mahali ukawa na ndoa za mikataba kama huko kwa wenzetu, ndoa na iheshimiwe na watu wote.