Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 775
- 1,332
Ni rafiki yangu wa kama miaka mitano, tumezoeana sana tangu tuko chuo. Tumekuwa marafiki kwa kipindi kirefu huku tukiwa na mahusiano yetu ya kimapenzi na watu wengine. Katika kipindi chote hiki, mahusiano yetu na watu wengine hayajawahi kuathiri urafiki wetu hata kidogo.
Hivi karibuni rafiki huyu ameanza uhusiano na mtu mpya. Huyu dada mimi ni classmate wangu wa enzi za sekondari ila hatukuwahi kuzoeana kwakweli (namuona anaringa, uzungu mwingi so damu zetu haziendani). Uhusiano huu naona unaelekea kuvunja urafiki wetu aisee na sifurahishwi.
Siku hizi wote tunafanya kazi hivyo kuonana ni nadra sana lakini tunajitahidi kupanga kukutana mahala na kupeana updates za maisha. Kila akija kuonana na mimi anakuja na girlfriend wake. Yani anaweza akaja alone ila baadae lazima huyo dada aje kutujoin.
Simchukii huyu dada wala sio kwamba nina hisia za kimapenzi kwa rafikiangu wala nini ila tukiwa watatu kunakuwa na awkward situation fulani yani. Wenyewe tunaongeaga saana na vicheko havikauki ila akiwepo yeye inakuwa ni ukimya tu na vimaneno vichache kutoka kwa rafikiangu akijaribu kuneutralize situation lakini bado kunakuwa ovyoovyo yani.
Sasa nawaza sijui nimwambie tu mshkaji kuwa awe anakuja mwenyewe au niwe nakataa mialiko?
Naomba ushauri