Kila siku naota napaa, msaada kuhusu hii ndoto tafadhali

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Jul 25, 2016
533
739
Wakuu ni takribani miezi mitatu sasa tangu nianze kuota hii ndoto ya kupaa na mara nyingi hii ndoto huwa naiota mida ya alfajiri na nikishapaa huwa najikuta katika mazingira tofauti na ulimwengu huu nisiyoyafahamu. Kwa wale wajuzi wa haya mambo ya ndoto naombeni msaada wenu juu ya hili, je hii ni ndoto ya kwawaida au inawezekana nachukuliwa na wachawi?
 
Nilipokuwa mdogo kila nikiumwa na kuanza kupata nafuu naanza kushuka kwenye mabonde marefu sana. Najikaza na kujikunja nisiumie lakini sifiki chini.
 
Elezea madhari nzima ya ndoto bila kusahau chochote.

Unapaa kwenda wapi?
Unakuwa na watu wengine?
Unapaa kutumia nini?
Ukishapaa unakutana na nini huko juu!?

Embu fafanua zaidi ili usaidiwe, ndoto ni lazima ufafanue zaidi ili watu wakusaidie.
 
mi nilikuwa nikianza kulala hata sijaala vizuri naota kama nateleza sehemu kama mlimani halafu chini ni maji ile nateleza nashtuka hadi narusha mguuu ila imeacha
 
Wakuu ni takribani miezi mitatu sasa tangu nianze kuota hii ndoto ya kupaa na mara nyingi hii ndoto huwa naiota mida ya alfajiri na nikishapaa huwa najikuta katika mazingira tofauti na ulimwengu huu nisiyoyafahamu. Kwa wale wajuzi wa haya mambo ya ndoto naombeni msaada wenu juu ya hili, je hii ni ndoto ya kwawaida au inawezekana nachukuliwa na wachawi?
No sio wachawi, inawezekana una uhusiano na UCHUMI wa Tanzania, maana nao unapaa kwa takriban miezi 10 sasa.
 
Elezea madhari nzima ya ndoto bila kusahau chochote.

Unapaa kwenda wapi?
Unakuwa na watu wengine?
Unapaa kutumia nini?
Ukishapaa unakutana na nini huko juu!?

Embu fafanua zaidi ili usaidiwe, ndoto ni lazima ufafanue zaidi ili watu wakusaidie.
Mkuu kwa kweli maana mazingira yake ni tofauti kabisa na huku duniani, huwa nakuwa mwenyewe wakati wa kupaa maana sioni mtu mwingine na kuhusu ninachokutana nacho huko ni mambo ya kustaabisha mfano juzi kuamkia jana niliota nikiwa nimeshika bunduki huku nikipambana na kundi la watu ambao mpaka sasa sikumbuki tulichokuwa tunapigania

Back
Top Bottom