Kila nikifanya attempt naangukia kwa divorcee, single mother au mke wa mtu, why?

jean phillipe beyun

Senior Member
May 18, 2015
142
167
Wadau pokeeni Salam zangu

Mm nipo kwenye early 40's sijaoa bado lakini nipo kwenye shinikizo kubwa sana kutoka katika ukoo wangu juu ya hili, Kuna wakati mama alitishia hata kuniletea mwanamke. Kubwa zaidi lililonifanya nichelewe kuoa ni kujipanga kimaisha, ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba, kusomesha wadogo zangu na kuweka boma langu kule kijijini, yote haya nimeyakamilisha

Jambo linalonitatiza ni kuwa kila nikipata mwanamke anakua ni mke wa mtu, au divorcee au single mother, nakuja kugundua baadae mahusiano yakiwa na Muda fulani tena ni baada ya mumewe kuanza kunisumbua niachane na mkewe, mwezi flani nilivamiwa bar na kundi la watu na kanifanyia fujo mbaya mmoja wao akidai mwanamke nilie kuwa nae ni mkewe, binti huyo husingeamini kama ni mke wa mtu, alinificha

Nimefanya attempt kama nne hivi tangu January matokeo ndio kama hivyo nilivyowaeleza, hivi karibuni nikafanikiwa kumpata dada mmoja hivi, ni lawyer, yupo kwenye legal team ya shirika flan hivi, ni mzuri sana, tukawa tumetoka out mara kadhaa, and eventually tukawa tumelala mara mbili Tatu hivi, Bahati nzuri mama yupo hapa tangu may, nikampeleka kwa mama wakafahamiana na akawa approved, mama akasema fanya juu Chini mfunge ndoa haraka

Hata hivyo siku tuliyokwenda kwao nikawa surprised, katika maongezi mzee wake ambae ni mstaafu akawa kama ananiasa kuwa niwe mtu mzuri kwa mwanae, nisiwe kama mume wa binti yake wa mwanzo ambae walishindwana wakaenda kuvunja ndoa mahakamani, nikaloa kabisa kwa taarifa hizo. Anyway baadae binti akanieleza mwanzo mwisho kuhusu hiyo ndoa ya kwanza, as usual kama ilivyo kwa watalaka wengi akampelekea lawama mtalaka wake, hata hivyo niliondoka bila raha

Hata sasa nimekua mnyonge kama vile najitoa flani yeye ndie ananitafuta sana, kiukweli kwa malezi niliyolelewa huwa nashindwa kumuelewa mwanamke alieshindwa ndoa kwa matatizo yanayoweza kuvumilika katika umri mdogo wa miaka 30. Pia sikutaka kufunga ndoa bomani, nilitaka nifungie ndoa yangu kanisani maana mm ni mkristo ninaeshiriki mambo yote kanisani, Huyu binti alifunga ndoa ya kwanza kanisani, hawezi kurudia tena

Mama yangu anasema huyu huyu anafaa, ameshanunuliwa vitu vingi na huyu binti kama zawadi, na kupewa pesa, sasa anasema hakuna sababu ya kujiuliza mara mbili mbili nimuoe hivyo hivyo

Wadau sijui mlikua mnasemaje?
 
Duuuuuuuu asee pole sana rafiki......kuna vtu nilikua nasomaga tu ushuhuda wa watu kuhusu familia kupresha hili kuoa...mi pia nnayo kama yako ila wewe yako makubwa zaidi...........MCHUKUE HUYO MWANAMKE SABABU BADAE MTAACHANA NA UTARUDI KWENYE MAISHA YAKO NA MAMA ATAKUWA TAYARI NA FURAHAA.
 
tatizo:

unaoa kwa shinikizo(sio mapenzi yako)
.unatongoza watu wa umri wako(tafuta angalau 30-35)
.una perception kwamba ambao hawajazaa au kuwahi kuolewa hawajatulia/hawafai kuwa wake wema)
. ama unakurupuka.

Yeye anatafuta ambao hawajawahi kuolewa wala kuzaa, sijui atawapata wapi though wapo.... labda amchukue binti wa sekondari amsomeshe baade aje amuoe, manake hata hao wa vyuoni wanaolewa kila siku
 
Kuoa/kuolewa ni kipaji. so wote tumeumbwa kuwa Mme/mke. Na kuwa umerekebisha kila kitu kwenye maisha si leseni ya kuoa/kuolewa. Muda umekwishakutupa kuoa mwanamke wa ndoto yako. ila maisha bila ndoa inawezekana.
 
Wadau pokeeni Salam zangu

Mm nipo kwenye early 40's sijaoa bado lakini nipo kwenye shinikizo kubwa sana kutoka katika ukoo wangu juu ya hili, Kuna
Dah mpendwa pole sana!!!Nafurahi wewe ni mtu wa Mungu as u said!!Sasa ni hivi uko kwenye mtihani mkubwa sana sana mwombe Mungu aingilie kati then ufanye maamuzi ya busara.Pili swala la watu kuachana ni swala gumu sana kujua nani alikua trouble maker in real sence maana kiroho hivi vitu ni very sensitive sana isije kuwa huyo dada au ex;hubby kuna roho zinawafuatilia mpk kuharibu ndoa yao.So kama ni huyo dada hutapona na hiyo ndoa.Pia usioe kwa shinikizo au mama kumpenda mtu unayemwoa hapana bali oa kama wewe mana ndo utaishi nae for the rest of your life.

Hivyo basi usisahau kurejea ktk vitabu vya bwana ktk mathayo (19:03-09) utafakari na ufanye maamuzi ya kumpendeza Mungu ili ukae kwa amani ktk ndoa yako. Usisahau you still have chance kupata wako wa kufanana naye mana ni ahadi ya Mungu si wa aliyekua wa mwenzio mana si mapenzi ya Mungu tusipende kujifurahisha au kufurahisha wengine Mfurahishe Mungu naye atakufurahisha.Ndoa iliyopangwa na Mungu huwa Mungu anaisaidia sana no matter what.

Will keep you in my prayer.Goodluk!!
 
1466159005118.jpg
 
40's?? Still swayed by pressure? Still can't make life decisions? Damn brah! That's 4 damn decades around the block.

If you're past your 20's and still buy into stupid myths like the cliché single mothers', then I feel sorry for you.

Frankly, you've lived almost all your life already bro, so you should drop that "picky" luxury card you're still holding on to.
 
Back
Top Bottom