Hata mwanaume hesabia!
Hiyo baraka ya 'side1' M/Mungu alitunyima na kumruhusu shetani achukue mkondo wake kwenye eneo hilo.
Nilichokifanyia utafiti na kujiridhisha ni kwamba, mizani ya penzi huwa haibalance hata siku moja, ndiyo maana wanaozidiwa hufanywa watumwa wa ridhaa.
Ukiona unamshobokea mtu, elewa haujai kwenye kiganja cha mtima wake, hakupendi na unamlazimisha tu.
Likija hili la ukwasi na mavyeo, hizo ni machela za kubebea mapenzi mfu.
Mtu anadangwa na janaume chafuchafu kinuka mdomo na ana 'go' kwa ajili ya hayo mahela, sasa hilo siyo penzi ni kitu kingine!
Hii dunia Mungu angeliyawekea mapenzi frequency, yaani yasachi hadi yapate upendwapo, wallah wanadamu tungeinjoi sana duniani hapa, kupendana kutamu asikudanganye mtu!
Maana hakuna jambo lenye thamani kama mapenzi, hasa kwa wapendanao 50 kwa 50, asiwepo wa kumpunja mwenzake.
Miss bado upogo mama? Sijakuona Jf masiku kibao!
Sent using
Jamii Forums mobile app