Kila mwanaCCM kapungukiwa na hili.

Kila mwanaCCM kapungukiwa na hili.

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,953
Habari wanajukwaa!

Bila kumwonea mtu aibu napenda kuonyesha mambo ambayo wanaCCM wamepungukiwa. Kati ya haya machache nitakayoorodhesha chini ndiyo wenzetu wamepungukiwa aidha moja au zaidi. Mambo hayo ni;
1.Uzalendo. Haiingii akilini mtu au mbunge kufurahia miswada ya dharura ya maliasili ambayo ipo tu haiishi au kuharibika kesho. Yapo mambo yanayohitaji miswada ya dharura ila si madini wala gesi.Wabunge wanaangalia posho na kumfurahisha Rais na si kwa manufaa ya watanzania wa leo na wa kizazi kijacho.
2.Elimu. Wengi wanaoshabikia mambo ya CCM na serikali yake ni waliokosa elimu ambayo ingewapa mwanga wa kujua na kuweza kuibua hoja zenye nguvu.
Mfano:Muulize mtanzania ni nini faida ya zoezi zima la utumbuaji majipu la rais Magufuli? au nini faida za zoezi la uhakiki wa watumishi kwa Tanzania utajibiwa majibu ya ajabu yasiyoeleweka.
Mwingine atajibu sasa tunaheshimiana,mwingine atasema walikuwa wapiga dili n.k
3.Uchafu wa kocha mkuu. Watanzania wengi hawajui kuwa huyu mtumbua majipu huko nyuma (mgongoni mwake) yake yeye mwenyewe ana majipu makubwa yanayoonyesha kuwa yeye si mzalendo na wala hana uchungu na taifa hili bali anachokifanya sasa ni kuonyesha tabia yake ya asili ya ubabe.
Mtu kama mimi nitamshangilia vipi mtu aliyelitia hasara taifa maradufu kwa maamuzi yake ya kukurupuka kabla hajaingia Magogoni.
 
04a9bea864388a62ec5e9d55964984ab.jpg
 
Ukitaka reference ya CCM
Chukua ZANU-PF, ANC, FRELIMO

Ccm hawajawahi kuwa wazalendo wa nchi hii labda mtu mmoja mmoja tena kwa kuogopa asiende kinyume na matwakwa ya chama
 
Habari wanajukwaa!

Bila kumwonea mtu aibu napenda kuonyesha mambo ambayo wanaCCM wamepungukiwa. Kati ya haya machache nitakayoorodhesha chini ndiyo wenzetu wamepungukiwa aidha moja au zaidi. Mambo hayo ni;
1.Uzalendo. Haiingii akilini mtu au mbunge kufurahia miswada ya dharura ya maliasili ambayo ipo tu haiishi au kuharibika kesho. Yapo mambo yanayohitaji miswada ya dharura ila si madini wala gesi.Wabunge wanaangalia posho na kumfurahisha Rais na si kwa manufaa ya watanzania wa leo na wa kizazi kijacho.
2.Elimu. Wengi wanaoshabikia mambo ya CCM na serikali yake ni waliokosa elimu ambayo ingewapa mwanga wa kujua na kuweza kuibua hoja zenye nguvu.
Mfano:Muulize mtanzania ni nini faida ya zoezi zima la utumbuaji majipu la rais Magufuli? au nini faida za zoezi la uhakiki wa watumishi kwa Tanzania utajibiwa majibu ya ajabu yasiyoeleweka.
Mwingine atajibu sasa tunaheshimiana,mwingine atasema walikuwa wapiga dili n.k
3.Uchafu wa kocha mkuu. Watanzania wengi hawajui kuwa huyu mtumbua majipu huko nyuma (mgongoni mwake) yake yeye mwenyewe ana majipu makubwa yanayoonyesha kuwa yeye si mzalendo na wala hana uchungu na taifa hili bali anachokifanya sasa ni kuonyesha tabia yake ya asili ya ubabe.
Mtu kama mimi nitamshangilia vipi mtu aliyelitia hasara taifa maradufu kwa maamuzi yake ya kukurupuka kabla hajaingia Magogoni.
HATIMAYE ILE SIFA CHAFU YA UFISADI KWA WANACCM IMEONDOKA....NINA IMANI NA HIZI ULIZOZIWEKA ZITAKWISHA TU NA KUHAMIA KWENYE KILE CHAMA KINACHOKUSANYA MAKAPI.
 
lowassa na sumaye ni wazalendo wa ccm na sasa ni wazalendo wa chama cha wema
 
Nianze kwa ku declare kuwa sina mahaba na upande wowote wa kisiasa (kati ya watawala CCM na wapinzani wa aina yoyote)

Mleta Mada naona huwatendei haki hao watu, Ingawa umeandika kuwa hayo ni mapungufu yao, lakini nikisoma between the lines naona mawazo yako hayana Uzalendo, wala huoneshi kuwa na elimu zaidi ya hao unao washutumu. Ninge kushauri tu uangalie zaidi maslahi mapana ya nchi yetu. Kumbuka kuwa binadamu wote tuna mapungufu yetu tusiwe judgmental saaaaana.

Mfumo wetu tulio uchagua/ulio tukuza umetufanya tuwe vilaza kwenye mambo mengi. Hivyo tusichekane wala kulaumiana bali tujikite kwenye kutafuta weledi wa kuyajua mambo na kuyasimamia yaliyo sahihi na yenye manufaa kwa nchi.
 
Mleta mada yupo sahihi hapo kwenye uzalendo.

Kwa kweli wabunge wa CCM na wanachama wa CCM hawana uzalendo zaidi ya kuhangaikia ushindi wa chama chao kwanza.

Mfano leo nilikua nawasikiliza baadhi ya wanaCCM wakati wakitoa maoni yao juu ya mambo ya madini na mikataba yake.
Wengi bado tu wanaendelea kushabikia kuwa mtu mmoja ndiye apewe mamlaka juu ya kila kitu.
Walielewesha kwa mifano mingi lakini wanabakia kama vile watu wasio elewa kabisa.
Oooh unajua rais ndio baba wa nchi ,ooh madara ya rais yaheshimiwe ,sijui rais ndiye mkuu wa serikali.n.k. Yani wamesahau jinsi tulivyopigwa na wawekezaji kwa utaratibu huo huo wa kumwacha mtu mmoja ajifungie ndani na kusaini mikataba.
Yani hata wabunge wa CCM ambao kwa wingi wao ni wa wakilishi wa watu wa makabila na dini zote kutoka maeneo yote ya Tanzania lakini bado wanaona mtu anayesema wao ndio wasimamie na kuipitia mikataba kabla ya kusainiwa ni mpinga nia njema ya serikali.

Lengo la wabunge na wana CCM ni nini hasa kwani naona wanataka mikataba ibaki kwa taratibu zile zile ili baadae tena watuletee rais atakayewaachia wapiga dili waendeleze dili zao.

Najiuliza kwani kuna ubaya gani mikataba hiyo kujadiliwa bungeni na kuondolewa mapungufu yake,?
 
Back
Top Bottom