Kila mtu ana shida zake

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,647
Reaction score
4,495
Unaamka umekosana sana na mkeo,nyumbani unapaona nyumbani pamekuwa kama jela yaani mpaka unaamua kwenda kwa mwenyekiti wa mtaa ili kupeleka kesi kuwa mkeo amebadilika amekuwa na kiburi na tabia mbaya.Ila unapofika kwa mwenyekiti wa mtaa unamkuta mwenyekiti wako wa mtaa anaosha vyombo huku kasimamiwa na mkewe,kumbe yule unayemtegemea akutatulie matatizo yako,yeye ndio anayo makubwa zaidi yako[emoji16][emoji16][emoji16].
Unashida na pesa na huna pa kuzipata unaamua kwenda kumkopa rafiki yako kipenzi,ambae unajua kuwa hawezi kukuangusha,Lakini cha ajabu unapokwenda kuelekea kwake,unakutana nae njiani akiwa na mabegi[emoji45][emoji45]anakwambia kuwa alikuwa anakuja kwako kuomba hifadhi ya muda,maana kafukuzwa kwenye nyumba aliyopanga kisa hana pesa ya kulipa kodi.
Haya mambo hutokea sana maishani,
Kwani hata yule Hakimu anaye-endesha kesi za watu,unaweza kuta anashindwa kuendesha matatizo ya familia yake.
Si ajabu kuona fundi seremala aliyekuchongea kitanda na kochi,yeye analala chini na hata viti
Kwani hamjaona fundi nyumba nae kapanga?
Unaumwa unakimbilia hospitali ili kupata matibabu,unapofika unamkuta yule Daktari unayemtegemea akutibu nae kalazwa anaumwa hoi.
Hii inatuonyesha kuwa hakuna binadamu aliyekamilika,sote tuna matatizo ila tofauti ni kuwa;matatizo yetu yanapishana.
Huu ndio wakati wa kutafuta msaada utokao juu,maana yeye aliye juu ndio hujua matatizo yetu na ndiye awezaye kuyatatua kwa muda muafaka.Naye kamwe hapatwi na magonjwa,shida,matatizo wala mauti;Yeye yu hai milele hata milele jumapili njema
 
Picha ipo wapi. Unalivunjia heshima jukwa hili mkuu. Hili jukwa la picha mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…