"Kila anguko lina inuko lake"

"Kila anguko lina inuko lake"

mtoto mdogo sana

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2020
Posts
476
Reaction score
1,446
Habari za Muda huu Wataalam
I hope weekend yenu pia iko sawa. Kwa upande wangu namshukuru Mungu.

Kupitia visa na mikasa na matukio ambayo huwa nakutana nayo hapa JamiiForums nimejifunza mengi. Kwangu mimi JF is more of a Home to me.

Kupitia matukio na majaribu na masaibu na mateso niliyopitia tangu nikiwa mdogo, niliwahi kufikiri kuwa huenda sitawahi kuja kuish maisha ya kawaida yaani ku "matter" kwenye maisha ya watu, achilia mbali kutengeneza maisha yangu mwenyewe.

Niliishi kama mdudu kwa kipindi kirefu sana mpaka nikapoteza stadi za kuishi kijamii kabisa. Nadhani hapa JamiiForums nimeshawahi kusimulia historia ya maisha yangu mwishomi mwa mwaka 2020.

Baada ya mfululizo wa matukio, mwishowe ukaja wakati wa "turnaround"
Ilifika wakati wa kuishi uhalisia. Kwa mara ya kwanza nikafanikiwa kujiskia mtu huru, sio auxiliary tena kama nilivozoea.

JamiiForums ilinikutanisha na watu mbalimbali ambao kupitia kwao niliweza kujifumza stadi zote za kijamii nilizozikosa, mpaka ikafika muda sasa wa kuingia katika ulimwemgu.

Nilikuwa Mtoto wa mtaani, nilikuwa chokoraa, niliishi maisha magumu tangu nikiwa na miaka 8, ila Mungu akanipigania, nikafanikiwa kwenda shule.

Mungu anajua namna ya kuziba nafasi zilizoachwa wazi. Pamoja na kuwa yatima, ila Mwenyezi Mungu aliniwekea watu kwenye maisha yangu ambao walinipambania hata bila ya kuwa na malengo ya ku benefit chochote.

Mwaka 2020 nikamaliza Chuo kikuu nikiwa sina pa kuanzia, lakini muda huo Mungu akazidi kunifungulia njia. Pamoja na majaribu, I proved I was worthy of redemption. Vipaji, karama na mapito yangu viliniandaa niwe ngangari kumudu Mungu alichoniandalia.

Kuna muda nikikaa natafakari miaka mita o iliyopita, nachekelea tu... Yaani maisha yangu mwenyewe ni stori ambayo kama ningesimuliwa na mtu, nisingeiamini. Yet here I am.

Najua tulio wengi hatuna past za kujivunia, ila amini kwba ni suala la muda tu, Mungu atampitisha kila mtu njia anayostahili.
 
Nikikumbuka nyuma na hasa nilipo tokea kwenye familia duni na fukara ilio jaa umasikini na ugumu wa maisha, nabaki kusema ASANTE MUNGU.
 
Hongera kwa kutoboa. Ni wakati sahihi sasa wakurudisha unachopata kule ulikotoka ili uliowaacha huko nao wainuke.
 
Umesema Mungu amekupigania na hivyo amekuletea watu wasimame na wewe mpaka ume graduate.
Hongera sana.
Ushauri wangu kwako kama utafanikiwa kuyafikia malengo yako usiwasahau wengine waliotapakaa mitaani.
Mitaa yetu imejaa chokoraa.
Kupitia nafasi zako ( Kazi na pesa ) rudi nyuma uwatazame wenzako wasio na matumaini.
Fanya kitu nao wapate matumaini.
 

Mkuu
Stori ilianzia


Kisha ikaendelea kwenye uzi wangu


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom