Kikwete: Nginja nginja hadi 2015.

Kikwete: Nginja nginja hadi 2015.

enzihuru

Member
Joined
Aug 6, 2012
Posts
82
Reaction score
10
Kwa mara nyingine tena, mheshimiwa Rais wetu ambaye anaweza kuingia kwenye vitabu vya jines kwa rekodi yake ya kushindwa kuwachukulia hatua wahalifu ambao anadai kuwajua wakati anayo mamlaka ya juu ya nchi, ameongeza msamiati mwingine kwenye kiswahili; 'nginjanginja'. Baada ya kulikosa kwenye kamusi ya kiswahili, nikarejea kwenye ile ya kikwele na kuona kuwa maana yake ni mshindo au nguvu kubwa itokanayo na kimbunga kama kile kilichosababisha maafa kule marekani.

Hivi ndivyo mwenyekiti wa CCM anavyowaambia wanachama wake, 'tangu sasa ni nginja nginja mpaka 2015.Kushindwa si suala la kujadiliwa, lazima tushinde na tumuingize ikulu mwanaccm pale Dar es salaam na pale Zanzibar'.Hii ni ujumbe mzito kwa vyama vya upinzani.CCM imepania kubaki madarakani na kwa gharama yoyote ile. CCM imepanga kutozuilika na chochote kile kama vile kile kimbunga hakikuzuilika pale marekani.

Sasa si tu ushindi wa kimbunga balihata majibu ya kimbunga na kampeni za kimbunga.Kimbunga kijapo, hakuna wa kukizuia na maafa si ajabu hivyo kila raia anapaswa kuchukua tahadhali.Kanali mstaafu Kikwete anaongoza na kanali mstaafu Kinana anaratibu mkakati huu.Hakuna M4C wala V4C mbele ya nginjanginja hadi 2015.
Kikwete + Kinana = KiKi

Maandalizi ya uchaguzi huo wa 2015 ni zaidi ya kujiandaa na kiama ya wafu.Take care.
Asalaam aleykum.
 
Only if we(citizens, leaders despite of our political differences)..would put just little more effort on National matters letting them being priority than focusing who will/wont win 2015..we'd be better off!
 
Taifa letu haliwezi kukombolewa na vyama siasa hata siku moja, ni masikini wachache watakaoamua siku moja kuwa enough is enough na kuleta mabadiliko muhimu.
kwa system nzima tuliyonayo ya mamlaka muhimu kutwaliwa na chama tawala, sio rahisi kwa chama pinzani kupishwa ikulu. Mamlaka muhimu za nchi zimegeuka kuwa dhuluma kwa vyama cha upinzani, wananchi so nchi yetu inahitaji mapinduzi nje ya vyamavya siasa.
 
Ccm nzima wakisikia cdm wanapata muharo. Wanaigopa km kipindupindu.Mkutano wote ilikuwa cdm. Km unabisha muulize mzee wa kusinzia bungen, wasira. Ana hasira sana.
 
CCM ndembe ndembe hadi 2015, umeme mgao, madini yanaibiwa, walimu mishahara ya dharau, gsi na benki za uswisi, wanamatusi wapnda vyeo. Hovyo kabisa
 
Mie silaha yangu ni kura wala si maneno ya kejeli wala matusi!
Mungu aniweke 2015.., bunduki yangu ni kura yangu then tutaona nani aliyeshika makali kati ya mpiga kura na mpigiwa kura!
 
Back
Top Bottom