Kikwete na Mkapa tubuni ili tusonge mbele!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,941
Reaction score
51,063
Baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela alianzisha tume ya Ukweli na maridhiano kwa ajili ya kutibu majeraha yaliyotokana na utawala wa Kikaburu katika nchi hiyo. Mfumo huo ulifuatwa pia na nchi ya Rwanda baada ya mauji ya Kimbari ya mwaka 1994.

Hapa Tanzania kati ya watu wanaotuhumiwa sana kwa kuifikisha nchi hapa ilipo sasa ni Jakaya Mrisho Kikwete na Benjamin Mkapa. Mkapa anatuhumiwa kutumia Ofisi za Umma kufanyia mambo yake binafsi na kutumia nafasi ya urais aliyokuwa nayo kwa faida yake binafsi.

Kikwete anatuhumiwa kutumia ofisi ya Umma (Ikulu) kufaidisha watu wake wa karibu pia kuzembea kuchukua hatua kwa watu waliokuwa wanafanya ufisadi dhidi ya rasirimali za umma na taifa.

Kwa sasa kauli na matendo ya wanasiasa wanaoongoza serikali ya awamu ya Tano, yanaashiria kwamba waliachiwa nchi na watangulizi wao ikiwa imevurugwa sana kiasi kwamba inabidi "inyooshwe" kwanza ili mambo yakae sawa.

Lakini Kikwete ambaye ndiye alikuwa Rais kabla ya Magufuli yupo hai, ni kwa nini asituombe watanzania radhi ili kumpa rais wa sasa nafasi ya kushughulika na mambo mengine ya maana zaidi badala ya kuhangaika na kuinyoosha nchi iliyopindishwa na kina Kikwete na Mkapa?

Kama Rais Magufuli kila siku analalamika kwamba watu "walizoea dili" na kulikuwa kumejaa "majizi" kwenye utumishi wa Umma, bila shaka hali hiyo haikusababishwa na yeye bali watangulizi wake ambao pia ni wana CCM wenzake Kikwete na Mkapa!

Kwa kuwa kwa katiba yetu haiwezekani kuwachukulia hatua Kikwete na Mkapa, ni kwa nini wao wenyewe wasiwe waungwana tu na kutoka hadharani na kutubu kwa kupanga mipango ya maendeleo hovyo hovyo na kulea uozo unaomsumbua mwana CCM mwenzao waliyemuachia uongozi wa nchi?

Sijamtaja Al Haj Ali Hassan Mwinyi kwa kuwa yeye alimalizana na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi hizo akiwa hai!
 
Yaani watubu kumpa JPM nafasi ya nini? Kwanini huyo JPM asitumie mamlaka yake dhidi yao?! Yaani umuombe mhalifu kuwajibika badala ya kushinikiza mamlaka husika ku-deal na mhalifu?
 
Anaenyoosha si na yeye alikuwa miongoni mwa waliopindisha? Vipi samaki wa wachina,yanayosemwa kuhusu uuzaji wa nyumba za gvt.
Sina maana kuwa watangulizi hawajakosea! Hapana namaanisha kila binaadamu anamapungufu makubwa sana na yeye mwenyewe hawezi kuyaona hadi binaadamu mwinzie amwambie.
Kukubali au kukataaa unachoambiwa na binaadamu wenzako hilo ni suala jingine ila nukta ya msingi ni lazima uwe na mapungufu na uambiwa na wenzako.
Mh Mkapa na Jakaya wamefanya mengi mazuri na hatukujua walikuwa wanakosea wapi kutokana na vipindi vya uongozi wao,hii ni sawa na Mwl Nyerere alivyoongoza wako watu leo ukiwatajia Nyerere wanatamani wakupige (siwajui) ila naamini kibinaadamu wapo!
Mkamilifu ni MUNGU TU.
 
JPM ameshiriki pakubwa kuipindisha Nchi. Kama anajiamini sasa aanze kupeleka watu kwenye mahakama ya mafisadi
 
Akimaliza muda wake ... Uwanja wa chattle utaota nyasi..

Ccm ni ileee ilee oohhh ni ilee ileee....
 
Lakini si utakuwa umejengwa. Kuna kitu wazungu wanaita "White Elephant Project"
 
Hivi huyu @allenkilewela si mnasema ni mwanasheria msomi,mbona anaandika ugoro?,
au ndo hasara ya kupeleka mtoto mbumbumbu sekondari nini?,

eti wameifikisha nchi hapa tulipo,
kwani tuko wapi na tulitoka wapi?.

Kama usomi wenyewe ndo huu,bora hata sikuhangaika kupoteza hela yangu kuutafuta,

mtu unajiita msomi,unaongea pumba hadi hata sisi ma LY tunakushangaa bana..what a shame
 
Hivi huyu @Allen kilewella si mnasema ni mwanasheria msomi,mbona anaandika ugoro?
Duh! usinipe uanasheria ili kufanikisha lengo lako la kuua haiba yangu (Character assassination). mimi ni machinga na ni LY wa hapa Iringa. Ukija Iringa ukisema mimi ni mwanasheria watu watakushangaa. Ila mwakani nitafanya mtihani wa QT ili nianze safari ya wasomi.

Ugoro gani nilioandika hadi upatwe na taharuki?
 
Ukiwahi kuwashauri Sumaye, Lowassa, Nyalandu nk juu ya hili?
 
NAKUPONGEZA KWA KUTEKELEZA SERA YETU YA UPINZANI YA KUFITINISHA SERIKALI NA WANANCHI KWA NJIA MBALIMBALI.MUNGU AKUBALIKI

Baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela alianzisha tume ya Ukweli na maridhiano kwa ajili ya kutibu majeraha yaliyotokana na utawala wa Kikaburu katika nchi hiyo. Mfumo huo ulifuatwa pia na nchi ya Rwanda baada ya mauji ya Kimbari ya mwaka 1994.

Hapa Tanzania kati ya watu wanaotuhumiwa sana kwa kuifikisha nchi hapa ilipo sasa ni Jakaya Mrisho Kikwete na Benjamin Mkapa. Mkapa anatuhumiwa kutumia Ofisi za Umma kufanyia mambo yake binafsi na kutumia nafasi ya urais aliyokuwa nayo kwa faida yake binafsi.

Kikwete anatuhumiwa kutumia ofisi ya Umma (Ikulu) kufaidisha watu wake wa karibu pia kuzembea kuchukua hatua kwa watu waliokuwa wanafanya ufisadi dhidi ya rasirimali za umma na taifa.

Kwa sasa kauli na matendo ya wanasiasa wanaoongoza serikali ya awamu ya Tano, yanaashiria kwamba waliachiwa nchi na watangulizi wao ikiwa imevurugwa sana kiasi kwamba inabidi "inyooshwe" kwanza ili mambo yakae sawa.

Lakini Kikwete ambaye ndiye alikuwa Rais kabla ya Magufuli yupo hai, ni kwa nini asituombe watanzania radhi ili kumpa rais wa sasa nafasi ya kushughulika na mambo mengine ya maana zaidi badala ya kuhangaika na kuinyoosha nchi iliyopindishwa na kina Kikwete na Mkapa?

Kama Rais Magufuli kila siku analalamika kwamba watu "walizoea dili" na kulikuwa kumejaa "majizi" kwenye utumishi wa Umma, bila shaka hali hiyo haikusababishwa na yeye bali watangulizi wake ambao pia ni wana CCM wenzake Kikwete na Mkapa!

Kwa kuwa kwa katiba yetu haiwezekani kuwachukulia hatua Kikwete na Mkapa, ni kwa nini wao wenyewe wasiwe waungwana tu na kutoka hadharani na kutubu kwa kupanga mipango ya maendeleo hovyo hovyo na kulea uozo unaomsumbua mwana CCM mwenzao waliyemuachia uongozi wa nchi?

Sijamtaja Al Haj Ali Hassan Mwinyi kwa kuwa yeye alimalizana na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi hizo akiwa hai!
 
NAKUPONGEZA KWA KUTEKELEZA SERA YETU YA UPINZANI YA KUFITINISHA SERIKALI NA WANANCHI KWA NJIA MBALIMBALI.MUNGU AKUBALIKI
Kivipi ndugu yangu. Unadhani kama Kikwete asingemuachia Magufuli nchi ikiwa hovyo hovyo magufuli angepata taabu? Wale maelfu ya wafanyakazi hewa, madeni feki, shirika la ndege lililokuwa limekufa na kadhali na kadhalika!
 
Unapenda sana misimu!!
Tungeanza na Magufuli kwanza atuombe radhi na kama kiwezekana arudishe nyumba zetu alizoonga na kugawa kama njugu!!
tapatalk_1497437380818.jpeg
 
Back
Top Bottom