Katika gazeti la Habari Leo ambalo ni gazeti la serikali la leo kuna habari inasema Kikwete anajiandaa kumkabidhi uenyekiti wa Ccm rais Magufuli mwezi june mwaka huu. Hakuna anayeweza kutilia shaka chanzo hiki cha habari. Na ukizingatia uteuzi wa Sendeka jana, huu unaweza kupanga safu mpya kabla ya kumkabidhi chama mweyekiti mpya.
Kiujumla mi naona kama wanachelewa. Tunataka kuona Magufuli mwenye mamlaka kamili ili kusiwepo kisingizio cha kutowakamata wauza unga sugu na hasa watoto wa vigogo waliojificha Ccm. Magufuli akiwa Arusha alisema majipu mengine yako Ccm, ni kweli na tumkumbushe kwamba majipu yote yako Ccm na huku nje alikuwa anatumbua vipele.
Escrow, EPA, IPTL, Makontena, Bomba la gesi, Mabehewa hewa zote ni kashfa za viongozi wakubwa wa chama na siyo walimu na manesi wanaotumbuliwa kila siku! Tunahitaji kuona nyoka wa makengeza wakishushwa kutoka kwenye miti ya midimu na magamba yaliyokwama kiunoni yakivuliwa. Tunataka kusikia waliosema ni upepo tu utapita wakizolewa na dhoruba.
Vinginevyo tuliosema tatizo la nchi hii ni mfumo hoja yetu itaendelea kusimama