Kikwete: Haikuwa rahisi kumshawishi Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,374
Mwenyekiti wa CCM anayemaliza muda wake anasema kuwa alitumia kila aina ya ushawishi ili Magufuli akubali kumpokea kijiti kabla ya Novemba 2017. Anasema kuwa alimuendea Ikulu kumshawishi ampokee kijiti. Hata hivyo, Rais Magufuli alimjibu kuwa ana mambo mengi ya kushughulikia ndani ya CCM hivyo haoni kuwa ni muda muafaka wa yeye kubeba dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa CCM. Kikwete anasema kuwa pamoja na maelezo yake ya kina, hakika Magufuli hakukubali kubeba dhamana hiyo. Mwisho na kwa lengo la kukata mazungumzo hayo, Rais Magufuli alimkaribisha ugali na hivyo jitihada zake zikagonga mwamba.

Anasema kuwa kutokana na hali hiyo, alimtuma Makamu Mwenyekiti Philip Mangula akamshawishi Rais kwani uzee ni dawa. Baada ya mwezi na nusu, Mangula akarudisha jibu kuwa Rais amekubali kuwa Mwenyekiti wa CCM na ndipo tarehe ikapangwa.

Kikwete anasema kuwa hata yeye alimkatalia mzee Mkapa mwaka 2006 kwa sababu kama hizo hizo ambazo. Hata hivyo anasema kuwa tofauti na 2006 ambapo hakukuwa na magazeti chonganishi na mitandao ya kijamii, mwaka huu wamemtungia uongo kuwa eti yeye anang'ang'ania madaraka na kwamba hataki kumkabidhi madaraka Magufuli. Shabaha yao ni kuchochea mfarakano na baada ya kuona CCM ni moja. Anawaomba wana CCM kuwa wamoja kwa vile wapinzani wao kila wanachokamata hakikamatiki.

Anasema kuwa kama angekuwa hataki kuachia nafasi, baada ya awali Rais kusema kuwa hana haraka ya kuwa mwenyekiti wa CCM, asingemtuma mzee Mangula. Aliamua kumtuma mzee Mangula kutokana na umuhimu wa kofia mbili kwa chama na serikali. Anasema kuwa mfumo huu wa kofia mbili una faida kubwa kwa chama na walioasisi mfumo huu waliona mbali. Anasema kuwa yeye hakutaka guu lake liote tende kwa kufanya maamuzi ya kutenganisha kofia.

Asante na hongera rais mstaafu kwasababu uku nje kulikuwa na maneno mengi
 
Mkuu, ni wapi nimesema hayo? Naona unanilisha maneno ambayo sikusema. Kwenye maandiko yangu niliweka bayana hili kuwa Kikwete hataki kuongeza hata sekunde moja ila wale wapambe wake ndio walikuwa wanahangaika
Ahsante!upo ddma?
 
Jk anavyopromosha CV yake ndani ya CCM anamaanisha nini.....au ni kupeleka msg kuwa anaijua vyema CCM kuliko anayemuachia......maana anasema amekitumikia chama miaka 41 mfululizo, ngoja nisubirie anayempokea Naye CV yake ndani ya Chama.
 
Na aliogopa kuongelea tena asinyimwe ugali na Raisi...eti raha kukaribishwa kula nae chakula..yaani Raisi.
 
Mwenyekiti wa CCM anayemaliza muda wake anasema kuwa alitumia kila aina ya ushawishi ili Magufuli akubali kumpokea kijiti kabla ya Novemba 2017. Anasema kuwa alimuendea Ikulu kumshawishi ampokee kijiti. Hata hivyo, Rais Magufuli alimjibu kuwa ana mambo mengi ya kushughulikia ndani ya CCM hivyo haoni kuwa ni muda muafaka wa yeye kubeba dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa CCM. Kikwete anasema kuwa pamoja na maelezo yake ya kina, hakika Magufuli hakukubali kubeba dhamana hiyo. Mwisho na kwa lengo la kukata mazungumzo hayo, Rais Magufuli alimkaribisha ugali na hivyo jitihada zake zikagonga mwamba.

Anasema kuwa kutokana na hali hiyo, alimtuma Makamu Mwenyekiti Philip Mangula akamshawishi Rais kwani uzee ni dawa. Baada ya mwezi na nusu, Mangula akarudisha jibu kuwa Rais amekubali kuwa Mwenyekiti wa CCM na ndipo tarehe ikapangwa.

Kikwete anasema kuwa hata yeye alimkatalia mzee Mkapa mwaka 2006 kwa sababu kama hizo hizo ambazo. Hata hivyo anasema kuwa tofauti na 2006 ambapo hakukuwa na magazeti chonganishi na mitandao ya kijamii, mwaka huu wamemtungia uongo kuwa eti yeye anang'ang'ania madaraka na kwamba hataki kumkabidhi madaraka Magufuli. Shabaha yao ni kuchochea mfarakano na baada ya kuona CCM ni moja. Anawaomba wana CCM kuwa wamoja kwa vile wapinzani wao kila wanachokamata hakikamatiki.

Anasema kuwa kama angekuwa hataki kuachia nafasi, baada ya awali Rais kusema kuwa hana haraka ya kuwa mwenyekiti wa CCM, asingemtuma mzee Mangula. Aliamua kumtuma mzee Mangula kutokana na umuhimu wa kofia mbili kwa chama na serikali. Anasema kuwa mfumo huu wa kofia mbili una faida kubwa kwa chama na walioasisi mfumo huu waliona mbali. Anasema kuwa yeye hakutaka guu lake liote tende kwa kufanya maamuzi ya kutenganisha kofia.
Hapo kwenye swala la kumkatalia mkapa si kweli,kwanza kipind kile yeye na lowassa walipounganisha nguvu ya kumzidi mkapa alichukia na uwenyekit alibwaga kwavle mtu wake sumaye hakupita...na dr salim wakamzushia alihusika ktk kifo cha karume znz
 
Huo ni mtazamo wako
 
Back
Top Bottom