MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 924
- 1,096
JK:HABARI LEO LIPO KUHIMIZA AMANI NA UTULIVU NCHINI.
WAKATI HabariLeo likiadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, Waandishi wetu Nicodemus Ikonko na Oscar Mbuza walifanya mahojiano maalumu na Rais mstaafu wa serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyelizindua rasmi gazeti hili.
Wakati maadhimisho haya yanamalizika wiki hii, tunarudia tena mahojiano haya kwa faida ya Watanzania, wasomaji na watangazaji wetu.
Swali: Miaka 10 iliyopita ulizindua rasmi gazeti la serikali la lugha ya Kiswahili, HabariLeo, mjini Dodoma ikiwa ni miaka 45 baada ya nchi yetu kupata uhuru. Ni kwa nini serikali iliamua kuanzisha gazeti hili?
Jibu: Unajua serikali ni ya wananchi, ni lazima habari za serikali ziwafikie wananchi. Kwa muda mrefu serikali ilikuwa na gazeti la lugha ya Kiingereza, lakini gazeti la Kiswahili halikuwepo.
Gazeti la Kiingereza la Serikali nalo lina historia yake. Serikali ilikuwa katika mfumo wa ‘Party State’ au Chama Dola kwa maana kwamba chama ndicho kilikuwa kinashika hatamu, magazeti ya chama (wakati huo) yalitosha kabisa. TANU walikuwa na gazeti la Uhuru, lakini pia kulikuwa na gazeti la Nationalist.
Uhuru ilikuwa na kazi ya kuandika kwa lugha ya Kiswahili na Nationalist waliachiwa jukumu la kuandika habari kwa lugha ya Kiingereza. Nationalist lilibadilishwa baadaye na kuwa Daily News na kukabidhiwa mzee Mkapa (Benjamin). Walipewa jukumu la kuandika habari kwa lugha ya Kiingereza.
Baada ya mageuzi ya kisiasa mwaka 1992, yaliyosababisha kufa kwa mfumo wa chama kimoja cha siasa na kuzaliwa kwa mfumo wa vyama vingi na hivyo kutenganishwa kwa shughuli za chama na serikali. Uhuru iliendelea kutoa habari za chama na serikali kwa lugha ya Kiswahili.
Hata hivyo, kutokana na mageuzi hayo ya kisiasa, na kadri miaka ilivyozidi kwenda mbele, magazeti ya binafsi yakaongezeka, ikaonekana umuhimu wa serikali kuwa na gazeti lake la lugha ya Kiswahili badala kuwa na gazeti la Kiingereza peke yake ili kuwapa wananchi habari zake.
Swali: Kitu gani kilikushawishi kwamba huo ulikuwa wakati mwafaka wa kuanzishwa gazeti jingine la serikali?
Jibu: Kama nilivyosema awali, tuliamua kufanya hivyo baada ya kuona magazeti binafsi kwao habari ni zile mbaya tu. Hata kama itakuwa ni habari nzuri, lazima waweke kitu kibaya. Nakumbuka wakati naingia madarakani, ni wakati ambapo serikali ilikuwa inatekeleza mpango wa kuanzisha Benki ya Wanawake.
Uamuzi wa kuanzisha benki hii ulianza wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu. Sisi baada ya kuona ni wazo zuri kwa kuzingatia kuwa hakukuwepo na benki ya kuwawezesha wanawake kiuchumi, nilitoa fedha Sh bilioni 3 na tukaagiza katika bajeti ya kila mwaka benki hii itengewe fedha ili ikue.
Sasa ukiliona jambo lenyewe ni jambo jema. Lakini gazeti moja (jina limehifadhiwa) wao wakaja na headline (kichwa cha habari) ‘Kikwete amkingia kifua Mkapa’. Unaweza kuona namna ambavyo magazeti binafsi yanavyojaribu kuifanya hata habari nzuri iwe mbaya, maana kwao habari mbaya ndio habari.
Kwa hiyo ilikuwa ni lazima tuanzishe gazeti la Kiswahili la Serikali ili lifanye kazi hii ya kufikisha kwa wananchi, habari ambazo ni sahihi kwa lugha yao ya Kiswahili.
Mwaka 2005 wakati tunaingia madarakani, tulikuta ufaulu wa wanafunzi kutoka shule za msingi kwenda sekondari (ukiwa) ni kwa asilimia sita tu, kwa hiyo kiuhalisia, Tanzania ni nchi ya watu waliomaliza elimu ya msingi na si Tanzania tu, takwimu zinaonesha ufaulu kutoka shule za msingi kwenda sekondari kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara wakati huo ni asilimia 20 tu.
Kuna wakati tuliamua kufanya evaluation (tathmini) ili kuona namna magazeti binafsi yanavyoandika habari za serikali, kwa kweli tuligundua kuwa headlines (vichwa vya habari) za magazeti mengi kama sio yote, ni kuhusu mambo mabaya ya serikali. Hiyo pia ilitufanya kufikia uamuzi huu wa kuanzisha HabariLeo.
Suala hili la serikali kuwa na vyombo vyake vya habari si hapa kwetu tu. Ndiyo maana kuna BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza), VOA (Sauti ya America), DW (Sauti ya Ujerumani) na RFI (Radio ya Kimataifa ya Ufaransa). Hivi ni vyombo vya serikali na kazi yake ni kueleza habari za serikali zao kwa usahihi. Sasa hapa watu wanataka serikali isiisaidie TBC, haiwezekani.
Swali: Je, mpango wa uanzishwaji wa gazeti la HabariLeo, haukuwa na upinzani wowote ndani ya chama au serikalini?
Jibu: Hapana. Uanzishwaji wake ulipokewa vizuri sana, tena katika chama uanzishwaji wake ulipokelewa vizuri zaidi maana ni suala ambalo lilikuwa limetajwa ndani ya Ilani ya chama.
Nakumbuka siku linaanza tulikuwa kwenye kikao cha NEC, basi likaletwa pale tukawaonesha wajumbe na baadaye tukawagawia nakala moja moja, wakafurahi sana. Ndani ya serikali vivyo hivyo, lilipoke wa vizuri sana, maana wenzangu wa serikalini waliona wamepata chombo kingine ambacho watakitumia kufikisha ujumbe wanaotaka wananchi waufahamu kwa uhakika zaidi.
Kwa hiyo uanzishwaji wa gazeti la HabariLeo ni uamuzi ambao ulipokewa vizuri sana na watu wa ndani ya chama na serikalini pia.
Swali: Nini tathmini yako ya ujumla juu ya gazeti hili na mwenendo wake kwa kipindi chote hiki?
Jibu: Gazeti linatekeleza majukumu yake kwa kuwasilisha habari zake kwa wananchi na wananchi kuwasiliana na serikali yao kama ilivyokusudiwa kuanzishwa kwake.
Linafanya kazi nzuri dhidi ya magazeti mengi binafsi. Wakati mwingine, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kama World Bank (Benki ya Dunia) au IMF (Shirika la Fedha la Kimataifa) huwa wanatoa taarifa kuhusu shughuli za serikali, sasa ripoti zao hizo zinapokuwa ni nzuri, hawa wa magazeti ya binafsi kwao si habari, wao wanategemea kusikia habari mbaya ili wawe wamepata habari wanazozitaka.
Hali ni mbaya lakini HabariLeo imesaidia sana katika hili, limekuwa linaitendea haki serikali. Lakini pia tumesema gazeti hili la HabariLeo litusaidie katika kujenga umoja na amani ya Taifa letu.
Wapo watu hawajali juu ya amani na utulivu wa taifa letu, hawajali kuandika habari za uchochezi, wapo tayari kuandika habari ili Wakristo na Waislamu wapigane, wachomane mikuki, hawaoni shida kuleta mfarakano, lakini HabariLeo mara zote wamekuwa kwenye line (mstari) inayotakiwa.
Wenzetu wana uhuru mkubwa zaidi kuliko sisi. Nchi kama Marekani wana uhuru mkubwa sana lakini hawawezi kukubali hili. Wao umoja wa kitaifa ni jambo muhimu sana na hawana mzaha kwa chombo chochote cha habari kinacholeta hisia za ubaguzi au mfarakano wao.
Mwandishi wa habari anapotangaza au kutoa kauli yenye dalili ya ubaguzi, wala hata haisubiri serikali kumchukulia hatua, wamiliki wenyewe wanachukua hatua dhidi ya mtangazaji husika. Huwezi kumtukana Rais pale Marekani, unaweza kumkosoa lakini si kumtukana, lakini hapa kwetu mwandishi wa habari anamtukana Rais bila hofu wala sababu ya kufanya hivyo, hili si jambo zuri.
Swali: Je, kuna wakati ulishafaidika katika kufanya maamuzi kutokana na taarifa zilizitolewa na gazeti hili?
Jibu: Ndiyo, yapo mambo kadhaa, unajua siku nyingi sasa siwezi kukumbuka vizuri, lakini yapo mambo ambayo baada ya kusoma katika HabariLeo nilikuwa naagiza wenzangu serikalini wachukue hatua.
Kupitia Ofisi Binafsi ya Rais (OBR), tulilitumia sana gazeti la HabariLeo kufuatilia mambo yaliyokuwa yanaandikwa kuhusu wizara na taasisi mbalimbali za serikali na umma katika utendaji na watumishi wake. Siwezi kutaja mojamoja lakini OBR ilitumia habari zilizoandikwa na kuzifuatilia kwa kuchukua hatua stahiki.
Hatusemi kazi yake iwe ni kusifia tu serikali, pale ambapo mambo hayaendi vizuri, ni kazi ya Habari- Leo kusema haya ili serikali iweze kuchukua hatua. Nakumbuka kuna wakati Habari- Leo waliandika jambo, nikalisoma nikamwambia Waziri nadhani alikuwa Mwapachu, chukua hatua mara moja, usisubiri mimi nielekeze hatua za kuchukua, gazeti hili linatosha kukufanya kuchukua hatua.
Swali: Nini kifanyike ili kuboresha gazeti hili?
Jibu: Gazeti hili lazima liendelee kuishi kwa kuzingatia malengo na matumaini ya kuanzishwa kwake na halinabudi kuendana na wakati. Kama halitakwenda na wakati halitaweza kupambana na magazeti mengine ya binafsi na hivyo litajikuta linapotea.
Lina changamoto kubwa ya aina ya habari za kuandikwa kwenye gazeti hili kwa sasa kutokana na uwepo wa mitandao ya jamii kuripoti habari mapema zaidi badala ya kuripoti siku inayofuata kama ilivyo kwa magazeti mengine. Kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano habari nyingi huwafikia wateja kwa mitandao ya kijamii kwa kompyuta, simu, intaneti na njia nyingine za kisasa za kusambaza habari.
Ni lazima kuongeza weledi na uwezo wa wafanyakazi wa HabariLeo. Ni lazima kuwapa mafunzo ya mara kwa mara wafanyakazi wa gazeti hili. Mafunzo ni muhimu sana katika kuwajengea uwezo waandishi hasa wakati huu ambapo teknolojia inabadilika kila siku.
Msiache mambo yaende kwa mazoea, mkifanya hivyo mtakuwa mnajiondoa wenyewe sokoni. Ni vizuri pia kujikita zaidi katika kuandika habari za uchunguzi lakini pia habari za wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kama Mpanda, Kasulu, Liwale na kwingineko. Habari za wananchi ni muhimu ingawaje wengi wanadhani hazivutii lakini ndizo zenyewe.
Kuandika shughuli za wananchi na maendeleo ya nchi yetu mtakuwa mnafanya mambo ambayo wengine hawana katika vyombo vyao. Vyombo vingine hutumia maoni ya waandishi wao na kuyageuza kuwa habari. Lakini pia vinajenga dhana potofu kwamba nchini mwao hakuna mazuri yanayofanyika. Dhana hiyo ni potofu.
Kuporomoka kwa maadili ya taaluma kumechangia sana hali hiyo. Tayari wamejiweka katika mawazo mgando dhidi ya serikali kwamba kila kinachofanya ni kibaya tu. Ni busara wakaandika pia na mambo mazuri yanayofanywa na serikali hata kama ni kidogo.
Katika hili vyombo vingine vya habari vimechangia sana kuipaka matope serikali kama vile haifanyi mambo yoyote mazuri. Na hii ni moja ya sababu ya serikali kuanzisha gazeti lake la Kiswahili ili watu wapate ukweli toka upande wa serikali pia na siyo mabaya tu kama zinavyoandikwa na vyombo vingine. Magazeti mengi sasa yanaandika habari za watu.
Mwelekeo wa magazeti haya ya Tabloid umekuwa hivyo, ndio maana unasikia mara Magufuli dikteta, mara lile. Mkiweza kuwa source (chanzo) ya habari za maendeleo ya nchi mtapiga hatua kubwa kuliko mlivyo sasa.
Kitu kikubwa ambacho nimekiona ni kwamba media (vyombo vya habari) zetu zimewafanya wananchi wetu kuwa wanung’unikaji, zimefanya wananchi wajenge dhana kuwa katika nchi yao hakuna mambo mazuri yanayofanyika. Ni lazima vyombo vya habari viwajenge wananchi katika kuiamini serikali yao. Hicho ndicho kinachofanyika hata kwa magazeti ya Kenya.
Sisi ni serikali, sisi si malaika, hivyo yapo maeneo tumefanya vizuri na ni vema yakaelezwa na yapo mambo mabaya ni lazima tukosolewe. Orodha ya headlines (vichwa vya habari) ya magazeti yetu yanathibitisha hili ninalolisema maana ni habari mbaya tu za serikali.
Mindset (mawazo mgando) za waandishi wetu wa habari zimeshajazwa habari mbaya tu. Ndiyo, wana haki, just be objective, wakosoe, lakini kama kuna eneo la kupongeza wapongeze. Hata mahali ambapo ubaya haupo wanatafuta, hili si jambo la maana kwa mustakabali wa taifa letu.
Swali: Mambo gani ungependa yapewa nafasi zaidi katika gazeti lako la Habarileo?
Jibu: Mimi nimeanzisha, ni gazeti la uhakika, watu wanaposoma habari katika magazeti mengine halafu wakaingiwa na mashaka hutafuta HabariLeo ili wasome usahihi wa habari hiyo. Kwa maana hiyo ni ukweli kuwa kwa habari za uhakika ni lazima usome HabariLeo. Mimi nadhani endeleeni kusimamia katika weledi na ukweli.
Mkizingatia msingi huu, ipo siku wasomaji wote watabaini kuwa HabariLeo ndiyo gazeti sahihi kusoma. Ipo siku watachoshwa na habari za uzushi na uongo. Tafadhali endeleeni kuwa chanzo kizuri cha habari za kuaminika na msijiingize katika gossip (habari zisizo na ukweli).
Katika magazeti yenu ndiko wananchi wanakopata habari zote za ukweli na uhakika zikiwemo nzuri na mbaya. Mjenge mahusiano mazuri na wasemaji wa wizara zote na pia hakikisheni mnakuwemo katika orodha ya mawasiliano yao katika njia mbalimbali za mawasiliano zikiwemo barua pepe.
Tafadhali muongoze vita dhidi ya distortion (habari potofu). Labda Sheria mpya ya Huduma za Habari y mwaka 2016 itasaidia kudhibiti hali hiyo ya upotoshaji, maana hali ni mbaya. Nawapongeza HabariLeo kwa kutimiza miaka 10.
Chanzo: habarileo