Kikwete: CCM tukiishi kwa kutegemea Polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli

Kikwete: CCM tukiishi kwa kutegemea Polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Imeandikwa na Julius Magodi na Habel Chidawali, Dodoma | Jumatano, Novemba 14, 2012

RAIS Jakaya Kikwete juzi aliwaonya wanachama wa CCM akiwataka waache kubweteka kwa kuwategemea askari polisi katika masuala ya kisiasa, kwani kufanya hivyo watakuwa wanajidanganya.

Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM uliofanyika kwa siku tatu mfululizo katika Ukumbi wa Kizota mjini Dodoma.

Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema kitendo cha wanaCCM kuishi katika siasa kwa kutegemea Jeshi la Polisi hakipaswi kukubaliwa kwani kimepitwa na wakati.

"Mnaishia kulalamika tu kila siku, eti wanatukana halafu mnaishia kusema ndiyo kawaida yao au utasikia mtu anasema eti Serikali haipo! Kazi ya Serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu," alisema Kikwete na kuongeza:

"Sasa mnataka wakisema Serikali ya CCM haijafanya kitu Polisi wawafuate, au wakisema Kikwete nchi imemshinda, Polisi wakawakamate? Kama wakisema hatujafanya kitu ni kazi yenu kusema kwamba tumefanya kitu, waonyesheni barabara, shule na mambo mengine."

Licha ya kwamba hakuwataja moja kwa moja, kauli za Rais Kikwete zilikuwa zikielekezwa kwa uogozi wa Chadema ambao kimsingi kinaonekana kuwaumiza vichwa CCM.

Huku akirudia mara kadhaa maneno hayo alisema, "Nataka mfahamu ndugu zangu kuwa tukiishi kwa kutegemea Jeshi la Polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli."

Kikwete aliwatuhumu viongozi wa upinzani kwamba ni waongo na kwamba wakati mwingine wamekuwa wakizusha mambo ambayo hayapo, huku wakijifanya kuwa na ushahidi wa kimaandishi.

Alimtaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwamba kuna wakati aliwahi kuzusha kwamba yeye (Kikwete), na makada kadhaa wa chama hicho wakiwamo Rostam Aziz walikuwa jijini Mwanza usiku, wakati si kweli kwani siku waliyodai alikuwa Nachingwea mkoani Lindi kwenye mikutano ya kampeni za urais.

Katika mazingira hayo, aliwataka wanaCCM kila mahali kujibu hoja za wapinzani kwa kauli na vitendo na wasikubali kuburutwa kwani uongo ukiachwa kwa muda mrefu unageuka kuwa ni ukweli.

Aliwaeleza kuwa ukimya wao katika kujibu hoja za wapinzani ni sumu kwao na kwamba wenzao wameanza kuaminika zaidi yao licha ya kuwa CCM ndio wenye majibu yote.

"Mkijibu kwa hoja wanatulia, sio Polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala. Walipoitoa kijana wetu akasimama na kupiga msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani," alisisitiza Kikwete.

Mbali na hilo aliwaonya kuacha malumbano ya mara kwa mara akieleza kuwa hali hiyo inakibomoa chama.

Alisema baadhi ya wanaCCM wamekuwa wakitumia muda mwingi kukosoana wao kwa wao, huku wakitoa nafasi kwa adui zao.

Mwenyekiti huyo alisema hakuna mtu kutoka nje ya chama anayeweza kukidhoofisha CCM kwa hoja isipokuwa chama hicho kinaumizwa na wanachama wake ambao wamekuwa wakilumbana bila sababu.

Akizungumzia suala la wagombea urais aliwataka wanachama wenye nia kufuata taratibu zote za chama pamoja na kuvumiliana ili ifikapo Mei 2015, mkutano utafanya uamuzi wa nani anasimama kupeperusha bendera ya chama hicho.

"Kwa wale mnaotaka kugombea, andikeni hiyo tarehe tutakuja hapa kuteua, lakini msituvuruge lazima mfuate utaratibu. Utaratibu huo utatangazwa, maana mkianza kupita huko na huko ndiko tunakopata matatizo," alisema Kikwete.

Kikwete juzi alichaguliwa kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata asilimia 99.92 ya kura zilizopigwa, huku kura mbili zikimkataa. Kadhalika mkutano huo uliwachagua Dk Ali Mohamed Shein kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania & Zanzibar) na Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania Bara).



Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Jamani huyu Rais wangu,

Mfano wa uongo wa upinzani ni mwaka 2010 alipoambiwa yuko Mwanza ilhali yuko Nachingwea

Mfano wa upambanaji wa hoja, ni kuchanachana bajeti iliyowakilishwa na Zitto Kabwe....


Mungu ibariki Tanzania,
 
mungu anaumbua sana watu..hilo neno limemtoka tu haikuwa nia yake,yeye ndo huteua IGPna tunaamini kuwa yeye ndiye anawatuma
 
Jamani huyu Rais wangu,

Mfano wa uongo wa upinzani ni mwaka 2010 alipoambiwa yuko Mwanza ilhali yuko Nachingwea

Mfano wa upambanaji wa hoja, ni kuchanachana bajeti iliyowakilishwa na Zitto Kabwe....


Mungu ibariki Tanzania,

wewe ,siku ile mwigulu aliwafanya kitu mbaya siku hiyo na imeingia kwenye history.
 

"Mkijibu kwa hoja wanatulia, sio Polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala. Walipoitoa kijana wetu akasimama na kupiga msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani," alisisitiza Kikwete.


Hapo kwenye RED. Kama Kikwete anafurahishwa na kituko alichokifanya Mwigulu Mchemba kwenye bunge la bajeti mwaka huu dhidi ya bajeti mbadala ya upinzani na kwamba hivyo ndivyo anataka makada wa chama chake wajibu hoja hakika CCM itaendelea kuporomoka na kupoteza mvuto.

Yaani Rais na Mwenyekiti wa chama anasifia Mwanasiasa ambaye badala ya kujibu hoja anatoa lugha za matusi, kujaa povu, kuchana hotuba na kuishia kuvalisha mbwa sare za chama kinachowakaba koo. Huu ni udhaifu mwingine.
 
Hakika JK kwa hili umenena, umekaribia kufa sasa umeamua kuwatupa wenzako, Kwa hio hata Mauwaji tuliyoyashuhudia ni kutokana na Polisi kuwalinda eee?? Sasa tutaona
 
Raisi JK kaweka wazi chama chake kinategemea polisi kufanya siasa na kushinda. Kwa hiyo amekubaliana na madai ya Chadema kwamba mauaji yanayofanywa na polisi kwenye mikutano mingi ya siasa hasa ile ya CDM ni maelekezo ya serikali yake ili kupaka matope mikusanyiko ya CDM na kuwatisha wananchi.

Damu ya marehemu wote lazima italia na wote walioimwaga bila hatia. Hakika dhambi hii itaitafuna CCM na viongozi wake mpaka kaburini.
 
Ayaaa weee ! Jk kamaliza kila kitu , duh ! Kwa hiyo Kamuhanda alisakiziwa kuwadhuru Cdm ? Sasa atajibeba na imekula kwake.
 
Jamani huyu Rais wangu,

Mfano wa uongo wa upinzani ni mwaka 2010 alipoambiwa yuko Mwanza ilhali yuko Nachingwea

Mfano wa upambanaji wa hoja, ni kuchanachana bajeti iliyowakilishwa na Zitto Kabwe....


Mungu ibariki Tanzania,
CCM wana ugonjwa wa akili........wote kabisa.
Mwenyekiti anasema wapambane kwa HOJA.......hoja zenyewe ni zile za Nchemba bungeni. Strange enough amekuwa rewarded for that bullshit!

Kweli CCM wanafikiri sawasawa??!
 
Masikini Jk anajaribu kuokoa jahazi linalozama kwa nguvu zake zote! lakini anasahau kwamba "Sikio la kufa halina dawa!!" CCM hawawezi kujibu hoja kwa hoja maana kutuonyesha barabara na shule sio jibu kwani hatuwezi kuisifia serikali ya CCM kwa kufanya kazi yake! they could have done lots and lots better kama sio kushamirisha umimi, kuhujumu uchumi, rushwa na ufisadi.

JK atwambie kama CCM na serikali yake ina hoja yenye akili ya kujibu kuhusu ufisadi wa Richmond, EPA, dowans, Mabilioni ya pesa za watanzania yaliyoko kwenye akaunti nje ya nchi na chaguzi za uongozi wa CCM na kwa hiyo uongozi katika serikali uliojaa rushwa ambayo hata yeye mwenyewe amekiri na kulalamika badala ya kuchukua hatua madhubuti!

Katika mambo kama haya CCM hawana hoja ya kurudisha bali kuegemea nguvu ya dola kuwasaidia kwa vitisho na mauaji ya watanzania wenye maoni tofauti na wanaotaka kubadilisha mustakabali wa taifa.

Frederick Sumaye aliwaasa siku nyingi kwamba wasitegemee dola kuwatetea, mbinu hiyo ina madhara ya kuwafanya wananchi kuichukia CCM na serikali yake na kusababisha wananchi kuamua kuiadhibu kwenye sanduku la kura kwa kura ya hasira.

baada ya kusema hilo nampa ushauri wa bure JK kwamba CCM haiwezi kukarabatiwa au kurekebishwa, CCM has to die first kabla haijafufuliwa; kama kuna kufufuliwa maana UPC UGANDA na KANU KENYA, UNIP ZAMBIA, MCP MALAWI vinaelekea kusahaulika kwenye ramani ya siasa za Afrika!! historia iko wazi kwa hili.

Naelewa JK anatimiza wajibu wake kwa chama chake afterall A BOER CAN NEVER COMMIT SUICIDE!!, lakini ukweli ni kwamba CCM is iredeemable, its fate is decided; done and sealed awaiting to be consigned to HELL
 
Kwa kuthubutu kutamka hili namuunga mkono na Kumpongeza kwa hili tu maana kunavingozi wengi wa CCM ni zaidi ya polisi wanaona CCM ni Polisi, CCM ni Mahakama na CCM Bunge pia. Bahati mbaya watendaji wa polisi, Mahakama na Hata bunge nao Hujikomba kwa CCM!
 
mungu anaumbua sana watu..hilo neno limemtoka tu haikuwa nia yake,yeye ndo huteua IGPna tunaamini kuwa yeye ndiye anawatuma
Labda siku hiyo alikuwa amepata cha Arusha.............:majani7: hii kitu huwa inawafanya watu waongee ukweli mtupu!!
 
Back
Top Bottom