Kikwete atuma ujumbe mzito Uchaguzi Mkuu 2015

Kikwete atuma ujumbe mzito Uchaguzi Mkuu 2015

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,782
Reaction score
5,172
KWA UFUPI

  • Rais Kikwete, ambaye atakuwa akimaliza kipindi chake cha miaka kumi tangu akabidhiwe nchi mwaka 2005, ametoa kauli hiyo ikiwa ni wiki chache baada ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kutawaliwa na vurugu na ukiukwaji wa sharia.

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ametuma ‘ujumbe mzito’ dhidi ya watakaofanya vurugu ama kuvuruga Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu, akisema watachukuliwa hatua kali.

Rais Kikwete, ambaye atakuwa akimaliza kipindi chake cha miaka kumi tangu akabidhiwe nchi mwaka 2005, ametoa kauli hiyo ikiwa ni wiki chache baada ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kutawaliwa na vurugu na ukiukwaji wa sheria na taratibu na kusababisha wakurugenzi sita kutenguliwa ajira zao wakati wengine watano wakisimamishwa ili kupisha uchunguzi.

“Hatua za kinidhamu zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya watu waliovuruga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwishoni mwa mwaka jana ni ujumbe mzito kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,” alisema Rais Kikwete juzi wakati akizungumza na mabalozi wa nchi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Tunatuma ujumbe mzito kwamba matukio hayo hayatavumiliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015,” alisema Rais Kikwete.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Desemba 24, baadhi ya wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wamekamatwa na wengine kufikishwa mahakamani kutokana na kufanya vurugu wakati, kabla na baada ya uchaguzi huo.

Mbali na kukamatwa watu hao, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia Desemba 17, 2014, aliwasimamisha kazi wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali kutokana na kuchelewa kuandaa na kupeleka vifaa vya kupigia kura.

Pia, walitimuliwa kazi kutokana na uzembe kutekeleza majukumu yao katika Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14 na 20 mwaka jana.

Vyama vya siasa, CUFna Chadema vimeendelea kulalamikia matokea ya uchaguzi huo, ambao CCM ilipata ushindi mkubwa, lakini ikapoteza baadhi baadhi ya mitaa iliyokuwa ngome ya chama WRais Kikwete alisema licha ya vurugu katika baadhi ya maeneo nchini, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umeonyesha kukua na kukomaa kwa demokrasia nchini.

Hata hivyo, tamko lake halikupokewa vizuri na viongozi wa vyama vya upinzani.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, John Mnyika, alisema badala ya kuzungumzia vurugu, Rais alipaswa kuwaeleza mabalozi amemchukulia hatua gani Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kutengeneza kanuni mbovu zilizosababisha uchaguzi uvurugike.

“Aidha, alipaswa aeleze amemchukulia hatua gani Pinda kwa kujibu bungeni kuwa maandalizi yote ya uchaguzi yalikuwa tayari, ikiwamo bajeti kumbe hali ni tofauti na hivyo kuathiri upatikanaji wa vifaa na ubora wa uchaguzi,” alisema Mnyika.

Pia, alisema inawezekana wakurugenzi waliosimamishwa walikataa kutii maelekezo ya kuhujuhumu upinzani.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya alisema japokuwa Serikali iliwatimua kazi wakurugenzi ambao hawakuwajibika ipasavyo kwenye uchaguzi huo, bado matatizo yanaendelea.

“Wakurugenzi wamepewa adhabu na wengine wamefukuzwa, lakini tatizo limeendelea kubaki pale pale. Leo wakurugenzi wanawaapisha watu ambao hawakushinda, hizi nazo ni kasoro,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally amesema alichofanya Rais ni kuwakumbusha wasimamizi wa uchaguzi kuwa makini wakati wa kusimamia mpango huo kwa kuwa zipo sheria zinazoliongoza na kutoa adhabu kwa anayekiuka.

“Sheria ya Uchaguzi Mkuu inataja adhabu, labda kisiasa anaweza kusema tu. Hata hao wakurugenzi waliofukuzwa kazi hawakuondolewa kwa sheria ya uchaguzi, waliondolewa kwa njia nyingine,” alisema.

Bashiru alieleza kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa haukusimamiwa na NEC, ndiyo maana Serikali imetangaza kuwa kuanzia mwakani utasimamiwa na tume hiyo.

Kimataifa

Rais Kikwete alisema mpaka sasa, Tanzania imetoa zaidi ya askari 3,000 kwenye Operesheni za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kulinda amani katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Darfur nchini Sudan na Lebanon.

Alisema kutokana na idadi hiyo, Tanzania inakuwa nchi ya sita kwa kuchangia walinda amani wengi barani Afrika na ya 12 duniani.

“Siku zote tumekuwa msaada na tutaendelea hivyo ili kuhakikisha kuwa mashariki mwa DRC kunakuwa huru bila makundi ya watu wenye silaha yanayotishia amani ya Congo na majirani zake,” alisema Rais Kikwete.

“Uwakilishi wowote mbaya unafanywa na watu wanaojifanya kuijua Tanzania na kukifanya kile wanachokiamini kuwa kweli. Hili halikubaliki na ni jambo la aibu. Linafanywa na watu wenye nia mbaya na nchi yetu.”

Kuhusu elimu, Rais alisema Serikali ina mpango wa kutoa bure elimu ya sekondari kuanzia mwakani kwa lengo la kuwafanya Watanzania kupata elimu ya msingi na sekondari bure.
chanzo mwananchi


 
CCM ndio mabingwa wa kuvuruga uchaguzi kwa kujitangazia ushindi sehemu walizoshindwa. Hakuna mwanaCCM hata mmoja magereza aliyewahi kufungwa kwa wizi wa kura, hivyo kauli ya Kikwete ni sawa na kujishebedua tu
 
Waliovuruga ni ccm. Yaani wanamwapisha mtu ambayechajachaguliw leo hii wanabana matta** wanadai wamefanyiwa vurugu.
Ulevi wa madaraka ni mbaya
 
Nimeshapkea hayo maelekezo mimi kama mkuu wa jeshi la polisi nchini nitawaelekeza vijanawangu wafanya fujo wote watanyoka tu.
 
Nimeshatoa heshima yangu ya mwisho kwenye kaburi la ccm Please join me and pay your last respect in ccm grave.

Naona tangu kimekupanda hakijashuka tumia dawa vizuri utapona penghine fahamu kuwa ccm ni chama cha mungu bangi zenu haziwezi kuiondoa ccmmadarakani ila watanzania ndiyuo wanaweza kufanya hivyo ila siyowavuta bangi kama wewe.
 
Kikwete ni mnafiki mkubwa. Kwa nini asiwachukulie hatua walioharibu uchaguzi wa serikali a mitaa? Kwani hawajui? Mara zote yeye mwenyewe amekuwa akitoa maelekezo ya uhuni huo kwa wafuasi na watumishi wake. Na ndiyo maana hawezi kuwachukuliwa hatua badala yake anabaki anapuliza puliza kuwadanganya Watanzania.

Kikwete anapaswa kufahamu kwamba WATANZANIA WENYE UJINGA KAMA WAKE NA FAMILIA YAKE WAMESALIA WACHACHE SANA.

Hatutaki unafiki wake. Hana sababu ya kujisemesha semesha wakati ukweli anaujua.

Angewachukulia hatua moja kwa moja walioweka mapingamizi yenye mashaka kwa 42% ya wagombea, waliokimbia na masanduku ya kura; waliotangaza matokeo ya washindi fake wakawaacha washindi halisi, walioita na waliokwenda kuapishwa tu wakati hawakushinda; waliobandika majina ya washindi bila kura;, waliobandika majina hewa ya wapiga kura; wala asingekuwa na sababu ya kubwabwaja.

Tayari ujumbe ungeshafika na angerejesha japo sehemu ndogo ya heshima ya uraisi wa Jamhuri ambayo ameipaka mafuta na mavi ya nguruwe!.
 
Amekaa kimya sasa anaenda kuwaeleza mabalozi lengo ni chama chake kipate ushindi mengine atajua jinsi ya kuyafanyia usanii ,amalizie kipande chake kwa amani.Hali itakuwa mbaya.
 
hatua zilizo chukuliwa ni kiduchu sana wakurugenzi walio chukuliwa hatua ni kondoo wa kafara. wakurugenzi kibao wamechangia kuharibu ichaguzi. na wakurugenzi wanahusika kutoa maagizo kwa baadhi ya wakurugenzi kutangaza walio shindwa ndo wameshinda. amani ktkbuchaguzi ujao utategemeana sana na umakinibwa serikali ya kikwete mwenyewe kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru na wa haki. inauma sana kuona watu wanapoteza maisha kwaajili yabwatu wachache wanao fanya vitendo dhalimu dhidi ya upande mwingine. serikali ifanye pia kila linalo wezekena kuwe na tume huru ya uchaguzi ili kuepusha shali
 
My Presida, Si sahihi hata kidogo kusema mwakani elimu ya primary na Secondary itakuwa bure...Swali kwa Sera za UKAWA??,Kwa maana in 2016 nchi na dola litaongozwa na Wapinzani.
 
My Presida, Si sahihi hata kidogo kusema mwakani elimu ya primary na Secondary itakuwa bure...Swali kwa Sera za UKAWA??,Kwa maana in 2016 nchi na dola litaongozwa na Wapinzani.
Unajipotosha mwenyewe jihurumie mwenyewe!
 
Mwaka huu hatuogopi vitisho vya ccm liwalo na liwe hii nchi ni yetu sote.
 
Maamuzi ya nguvu ya uma si kama maamzi ya bunge. Then uchaguzi mkuu asiufananishe na sakata la ESCROW, unapozungumzia uchaguzi mkuu ni mabadiliko ambayo hayazuiliki, ni lazima kukubaliana na matokeo yatokanayo na maamizi ya nguvu ya umma NUKTA
 
Back
Top Bottom