Kikwete ataka mikutano ya hadhara

Kikwete ataka mikutano ya hadhara

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
JAKAYA Kikwete, Rais mstaafu wa awamu ya nne na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyemaliza muda wake, amewataka viongozi wa chama hicho kufanya mikutano ya hadhara kote nchini ili kukiimarisha chama hicho, anaandika Regina Mkonde.

Kikwete ameyasema hayo leo wakati akitoa hotuba yake katika mkutano maalumu wa chama hicho wa kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti wa chama hicho Taifa.

“Viongozi wetu kutofanya mikutano kwa wananchi ndiyo sababu mambo yalianza kutuharibikia huko nyuma na hatutaki iwe hivyo tena, naomba mwenyekiti ujaye wa chama, usiache hii hali iendelee.” Amesema Kikwete huku akiongeza;

“Viongozi wakienda kwenye mikutano ya hadhara hushangaa namna wananchi wanavyojitokeza kwa wingi kuwasikiliza, kwa nini mnaogopa kwenda kwa wananchi, kama tunawatafuta wanachama wapya hivi tutawapataje bila kwenda walipo?” amehoji Kikwete.

Rais mstaafu Kikwete pia amempongeza katibu mkuu wa chama hicho Kanali mstaafu Abdurahman Kinana kwa kuendesha mikutano mingi ya hadhara ili kufufua uhai wa CCM katika kipindi chote cha miaka mitatu kama katibu mkuu wa chama hicho.

“Nampongeza Kinana kwani katika kipindi chake, amekuwa nguzo imara ameenda katika mikoa, wilaya na majimbo yote hapa nchini kuzungumza na wananchi na alifika mpaka maeneo ambayo viongozi wa chama huko hawakuwahi kufika. Amesema Kikwete.

Amesisitiza kuwa viongozi wa chama hicho kutokwenda kwa wananchi na kufanya mikutano ni miongoni mwa sababu za CCM kuyumba na kuwa na wakati mgumu wa kupata kura za wananchi katika uchaguzi mkuu uliopita.

Kauli hii ya Kikwete imekuja leo, ikiwa ni miezi michache tangu kutangazwa kwa marufuku ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ambayo ilitangazwa na Rais Magufuli na kutiliwa mkazo na Jeshi la polisi hapa nchini.

Ni marufuku hiyo ya mikutano ya hadhara ndiyo iliyosababisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia Naibu Katibu Mkuu wake (Bara) John Mnyika kufungua kesi mwanzoni mwa juma hili katika mahakama ya haki ya Afrika Mashariki kupinga zuio hilo la serikali.

Wito wa Rais mstaafu Kikwete kumtaka Rais Magufuli kuendeleza utamaduni wa viongozi wa CCM kufanya mikutano ya hadhara imetafsiriwa kama ukosoaji wa wazi dhidi ya marufuku ya serikali na Jeshi la Polisi juu ya mikutano hiyo hapa nchini.
 
Siasa bila matusi hapo sawa, siasa makanisani hapana, siasa za kikabila na kikanda hazifai, siasa za virova vya red brigade, na miwani zao za kuchomea welding, maji taka😱
 
Taasisi kubwa kama kiongozi wa nchi inahitaji busara sana. Asante JK kwa kuligusia hili. Mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba ukiachilia mbali kwamba ni mikakati ya kuboresha chama.
Binafsi nilijua ipo siku hilo jambo litapingwa na wengi. Wacha demokrasia iwepo halafu ujigambe kuwa umewaletea watu maendeleo
 
Elewa. Mikutano ya kisiasa ruksa na si mikutano ya vurugu.
Waambie jamaa zako vurugu ni marufuku.
Intelijinsia ikigundua ni fujo, marufuku kufanyika
 
Siasa bila matusi hapo sawa, siasa makanisani hapana, siasa za kikabila na kikanda hazifai, siasa za virova vya red brigade, na miwani zao za kuchomea welding, maji taka😱
Umesahau wale green guards au wao wapo kikatiba ??!!
 
Magu pokea huu ushauri wa Mzee smart kuliko wote wa Afrika JK.
Nalog off
Tatizo kubwa la Magu anashindwa kujitune kufit kwenye upolitician......

Yeye amejiegemeza zaidi kwenye serikali na kwenye uenyekiti wake inaonekana atakuwa anatumia 'mbeleko' ya Policcm katika kufanya shughuli za siasa ndani ya CCM.

Nilimsikia akijicontradict waziwazi kwenye hotuba yake, alipoanza kwa kusema atakapokuwa Mwenyekiti atatumia Katiba ya Chama inavyosema ya kutumia vikao vya chama katika maamuzi mbalimbali ya Chama........

Lakini wakati huo huo akasema kama angekuwa yeye ndiye Mwenyekiti wakati ule wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, wakati wajumbe wa NEC walipokuwa wanaimba wana imani na nanihiii.......

Akadai kama yeye ndiye angekuwa kwenye nafasi ya uenyekiti wa JK, robo ya wale na akasema hata nusu ya wale wajumbe wangepotea.........

Ingawa hakufafanua 'angewapotazaje' hao robo hadi nusu ya wajumbe hao wa NEC, ni dhahiri tafsiri unayoipata ni kuwa angewatumbua!
 
Hahaha hata mimi niliiona hiyo, hilo ni dongo laivu
Kama umeisikiliza hotuba ya JK kwa umakini utagundua kuwa anapingana waziwazi na mbinu zinazotumiwa na JPM za kuliagiza Jeshi la Polisi lizuie mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, lakini wakati huo huo Jeshi hilo la Polisi liruhusu mikutano ya CCM kufanyika........

Ndiyo maana akasisitiza kuwa njia pekee inayofaa kwa CCM kupambana na wapinzani, ni wanapoona wapinzani wameenda kufanya mikutano na wananchi na wao CCM waongeze bidii mara 2 kwenda kufanya mikutano hiyo na wananchi.....

Kwa namna ninavyofahamu hulka za JPM, sidhani kama atakubaliana na ushauri huo wa JK na badala yake atataka kutumia kofia zake za Upresidaa huku akiwa Amri Jeshi Mkuu kuagiza vyombo vyake vya usalama kuvunja Katiba ya nchi Ibara ya 3, ambayo inaruhusu mfumo wa vyama vingi nchini,na badala yake atalitaka Jeshi hilo la Polisi liendelee kuzuia shughuli za siasa za vyama vya upinzani kama vile nchi hii ipo kwenye mfumo wa Chama kimoja!
 
Jk hua namwelewa ktk matamko na ushauri wake japo nae taarab nyingi saa aingine ila kampa ushauri mzuri sana
 
jk Ana busara sake bwana na siyo wale wanakulupuka na maamuzi kutoka chumbani na wake zao
 
Elewa. Mikutano ya kisiasa ruksa na si mikutano ya vurugu.
Waambie jamaa zako vurugu ni marufuku.
Intelijinsia ikigundua ni fujo, marufuku kufanyika
Mbona unaruka ruka kama pia. Marufuku ilikuwa wazi kabisa mpaka 2020, leo imewagusa mnaanza kimbia kivuli.
 
Back
Top Bottom