Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,334
- 72,798
Kizungumkuti kimeanza kuonekana. Hii ni kutokana na kauli za Rais Magufuli kuwa yeye sio mwanasiasa bali mtendaji, na hata matendo yake yameanza kuonyesha kuwa kauli yake ni ya ukweli.
Ndani ya chama pengine hilo swali wanajiuliza sana na ndio maana wameahirisha zoezi la mwezi huu June kumkabidhi chama cha siasa kilicho asisiwa kwa umakini miaka mingi iliyopita kwa mtu ambaye sio mwanasiasa.
Wote tunajua kuwa Jakaya Kikwete ni mwanasiasa, tena aliyekulia ndani ya shughuli za siasa maisha yake yote na hata kama utendaji wa kiserekali ulipata kasoro nyingi bado ndani ya chama ameweza kukivusha pale watu walipo amini kuwa sasa kimevurugika. Yote hayo ni kwa vile ni mwanasiasa naye anajua hivyo.
Jee chama alichokabidhiwa kukiongoza toka kwa waasisi wake kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa na wazee wengine mashuhuri anaweza leo kukubali kukikabidhi kwa mtu ambaye kauli na matendo yake yanadhihirisha kuwa sio mwanasiasa?
Atakubali kweli akiwa bado anaishi kushuhudia chama walichotoka nacho mbali kikidhoofu au kujifia kwa vile tuu eti kulikuwa na utaratibu (usio rasmi) kumkabidhi mrithi wa Urais? Kwa mweledi wa siasa za mizengwe kama Kikwete uwezekani huo ni mdogo na jee kutakuwa na athari gani hayo yakitokea?
Tukumbuke CCM ni chama tawala.