Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila
Kinshasa:
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, amewafukuza kazi watumishi zaidi wa umma nchini humokatika juhudi zake za kupambana na rushwa, usimamizi mbaya wa matumizi ya fedha katika idara mbalimba nchini humo ikiweno forodha na idara ya utozaji kodi.
Rais Kabila amewafukuza kazi wafanyakazi 119 huku wengine zaidi ya 2,500 kulazimishwa kustaafu.
Mwaka uliopita Rais Kabila aliwafukuza kazi ama kuwastaafisha watumishi wa umma wapatao 1,300 na majaji wapatao 100.
Rais huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo amekuwa akipambana kuinua uchumi wa nchi hiyo na kupunguza madeni ya nje.
Rais Kabila anahitaji mapato zaidi kutoka katika miradi ya madini ambayo ndiyo uti wa mgongo wa taifa
Ni somo zuri sana kwa JK. Kijana aliyekulia na kusoma Tanzania anadiriki kufanya maamuzi magumu. JK akiambiwa kuwa anashindwa kufanya maamuzi magumu watu wanapiga kelele. Njii hii bila kuwatimua kazi na kuwafunga baadhi ya watumishi na watendaji serikalini huu ujinga ujinga utaendela. Big Up Kabila..
.. Na yeye ni mkora tu that's why anashindwa kuwabana na hao wakora wengine anajua watatoa siri....Big up Kabila! tunataka na rais wetu aige mfano wako, anadai yeye hana mamlaka ya kuwabana mafisadi...usanii mtupu
.. Na yeye ni mkora tu that's why anashindwa kuwabana na hao wakora wengine anajua watatoa siri....
Kuna Rafiki yangu Mkuria antumia sana neno hilo akimanisha mtu wa kurubuni rubuni bila shaka huyu jama naye ni Mkuriamkuu nini maana ya mkora? na huyo mkora ni nani?
Rais wetu hawezi full stop
Anaweza kwa wafanya kazi wa chini kama hao wa TRA na walimu !!! Ila sidhani kwa wala Rushwa na mafisadi kama anaweza !!
Hali ya uchumi Tanzania imekuwa mbaya mbaya sana.. Jana nilikuwa najaribu kuzungumza na jamaa zangu kuhusu mambo ya kawaida yanayo tuzunguka..
Kwa sasa imeonekana hata biashara ya ukahaba kwa vibinti vidogo vya miaka 16 na 17 imeongezeka sana kutokana na hali ya kipato kuwa ndogo kwa wananchi.!!
Hii ni dalili tosha kabisa kwamba tunaelekea mahala kubaya sana There is no point of return hata iwe je kwa sasa !!!
Rais wetu hawezi full stop
Dakika za majeruhi na awamu ya mwisho atakuwa mbogo sana.....stay tuned....lazima awaadabishe,awabadilikie na mahakamani pia!!!!
Haa Haaa umenifurahisha sana mkuu.Naifahamu. Juzi nikiwa Ubungo ilipoa ishara ya gari kuanza kuondoka nusura niingonge ya mbele yangu maana kumbe trafik alikuwa yuko pale aaongoza jinsi ilivyokuwa inampendeza.Hivi kwa miaka minnne hii hamjamchoka tu kumsema JK! hata kuuliza kuwa anaweza? jamani ebu tuangalie upande mwingine.
unafahamu robot wewe??