Kikwete anapoteua mawaziri wake ...

wakuu haiwezekani haya yote mabaya yanayotokea serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha miaka mitatu,bali kinachofanyika na awamu ya nne ni kurekebisha makosa yaliyofanywa awamu zote tatu zilizopita kama mzee ruksa alivyosema jana.

JK alisimama mbele ya wananchi na kwa maneno yake mwenyewe alisifia mambo yote aliyofanya Mkapa na bila aibu yoyote aliapa kuyaendeleza kwa ari, kasi na nguvu mpya. Na kwa hili amefanikiwa kama tunavyoshuhudia tunavyozidi kudidimia kwenye ufisadi. Mzee ruksa ? - kipindi chake chote cha miaka kumi alikuwa yupo yupo tu ama tunasahau upesi hivyo.

Kilichokuwa kinatakiwa ni good intentions ya kila rais anayekuja kuchukulia yaliyote mabaya yaliyofanywa na seriali iliyomtangulia kama changamoto na kuyarekebisha kwa kufuata taratibu na sheria za nchi ilizojiwekea.

Hebu fikiria kama hili lingekuwa kweli - hivi sasa tungekuwa tunapaa haswaa. Kama unasikia ndoto za Alnacha ndizo hizi - good intentions bila uwezo wala ujasiri ni kama kama kelele za mbwa mkali asiye na meno (toothless bulldog). Nchi imekuwa kama shamba la bibi - si ujanja kupata ?

kama ingefanyika hivyo kwa kila awamu basi serikali ya awamu ya nne ingekuwa na vitu vichache kama changamoto kubwa lingekuwa kuleta maendeleo halisi kwa watanzania . thx

Come on wake up man, it's close to fifty years now na chama kile kile, siasa zile zile, sera zile zile, viongozi waliotokana na mfumo ule ule na nia zile zile ndizo hizo - sasa tutegemee kipi kipya ? Serikali ya awamu ya nne hasa ndio imefunga kazi kwa usanii - imeshindwa hata kupambana na virusi ndani yake. Whither to Tz ?
 
Back
Top Bottom