Kikwete anaongea na watanzania gani?

Mie amenigalagaza pale aliposema hata marais waliomtangulia walishindwa kutatua matatizo ya nchi sembuse yeye! Yaani huyu mjamaa aliomba urais ili akae tu ikulu, kutembea juu ya red carpet na kutanua majuu? Alitaka urais akijua kuwa ni rais wa kushindwa tu?

Hata hivyo sishangai sana na kauli hiyo kwa sababu katika ule mdahalo wake TBC1 na na waandishi wa habari siku mbili kabla ya uchaguzi alisita sana kujibu swali alilolulizwa: "Unataka Watz wakukumbuke kwa kitu gani ukimaliza urais?" Baada ya muda akajibu: "Nataka Watz wanikumbuke kwamba niliwatoa hapa na kuwafikisha pale."

Yaani alitutoa kwenye bei ya sukari ya Sh 500 kwa kilo hadi sasa karibu 2,000/- na kaimaliza kabisa muda wake 2015 itakuwa 4,000/- kwa rate hii!

Alitutoa kwenye bei ya bati 5,000/- had sasa 15,000/-, cementi 6,000/- hadi 13,000/-!
 
mi najiulizaga swali hilo kila mara nikiwasikiliza hawa viongozi wetu wakiongea sijui labda tunaishi tanzania mbili tofauti wenzetu haya yanayotukuta sie hayawakuti wao
 
JK anapashwa kuwashukuru CHADEMA Kwa kumwamsha kutoka usingizini
anakuja na mbinu za kitoto kweli badala ya kuja na mbinu za kuweza kutukwamua kiuchumi na kuondoka na jinamizi la umeme na mfumko wa bei, acha kulia hovyo na CDM waache wazunguke na wewe kama una jeuri wajibu kwa vitendo kama vile mwisho wa mgao leo jioni, kuanzi kesho sukari, mafuta ya kula, pamoja na vingine bei chini wananchi watambue kweli sasa umedhamiria sio hotuba yote imejaa malalamishi ooooohhhh CHADEMA CHADEMA vuruguru ghasia tupe jipya
 
Back
Top Bottom