Kikwete ampiga kijembe Rage

Kikwete ampiga kijembe Rage

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,944
Reaction score
4,511
RAIS Jakaya Kikwete amemshangaa Mwenyekiti wa Simba SC ya jijini Dar es Salaam, Ismail Aden Rage kwa kuitisha mkutano wenye ajenda moja kwa ajili ya wanachama wa klabu hiyo.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Simba Rage, alitangaza kuwepo kwa mkutano wa klabu hiyo Machi 23 na kueleza wazi kuwa kutakuwa na ajenda moja ya kujadili mapungufu ya Katiba. (HM)

Akizungumza mbele ya umati wa watu waliohudhuria mazishi ya Mbunge wa Chalinze, Saidi Bwanamdogo mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Kikwete ambaye alifika katika eneo la makaburi, alimuuliza Mwenyekiti huyo wa Simba kuhusiana na maandalizi ya mkutano huo.

"Ndugu yangu Rage mimi Mwenyekiti mwenzio, lakini sijawahi kuona mkutano wenye ajenda moja ndio kwanza huo wa kwako, yaani wewe kiboko, pamoja na makelele yote lakini umeweza kutuliza hali ya mambo mpaka leo umedumu kuwa mwenyekiti," alisikika Rais Kikwete akisema huku mamia ya waombolezaji wakicheka.

Akizungumzia kauli hiyo ya Rais Kikwete, Rage alisema ili kuwa kiongozi imara ndani ya klabu za Simba na Yanga, inakupasa kuwa na roho ngumu, kwani bila ya kufanya hivyo wanachama watakuwa wakikuchezea kila kukicha.

"Mheshimiwa Rais kuwa kiongozi ndani ya klabu hizi mbili kunahitaji umakini sana, kwani bila ya kufanya hivyo wewe utakuwa ni kiongozi wa kupelekwa kila siku na hatimaye unamaliza muda hakuna ulichokifanya ndani ya uongozi wako," alisema Rage.

Chanzo: Mtanzania
 
Hahahahahahaha!..

Hizo Yanga ni kiboko kuna yule kiongozi alileta kama hizi za Rage wakamfuata kwake usiku akapigwa mkwara,kesho yake

ilibidi ajiudhuru mwenyewe.
 
Hata akimpiga kijembe hatushangai tunajua yeye ni yanga damu, hata usajiri w twite yeye ndie alie haribu sasa kwa okwi imekula kwake ndio maana analeta maneno, chezea Rage wewe
 
Mbinu anazotumia kuzima moto hapo klabuni kwake zitamsaidia hata kutetea ubunge wake 2015 Tabora.
 
hivi kuna kamati gani nzuri ya ufundi nimuendee Rage?
 
Watu wanakunywa maji na fisi huko singida tunajadi michezo!! Unaweza cheza kwenye njaa! Kweli wa tz
 
Wanasimba walisha hamia Azam na mbeya cty yy anaongoza jengo na wachezeji. Hata huo mkutano utauona.
 
Mbinu anazotumia kuzima moto hapo klabuni kwake zitamsaidia hata kutetea ubunge wake 2015 Tabora.

Bila kuathiri uhuru wa kuchagua mbunge mnayemtaka; nashauri wana-Yanga mlioko Tabora msimchague tena Rage, maisha yamdunde hadi ashangae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom