Kikwete amezindua mpango wa "bare minimum" katika kufaulu Sekondari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amezindua mpango wa "bare minimum" katika kufaulu Sekondari

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Amanikwenu, Feb 4, 2011.

 1. A

  Amanikwenu Senior Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wote naamini tunakumba kuwa mwezi uliopita Rais Kikwete alizindua mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari Awamu ya Pili. Mpango huu unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz/documents). Kwa ujumla ni mpango mzuri japo kuna maeneo ambayo yanapaswa kuboresha zaidi na kutengewa fedha zaidi. Pamoja na malengo yaliyomo katika mpango huu nimeshangazwa sana na lengo kuwa, ufaulu wa Wasichana katika Hisabati umepangwa kuongezeka toka asilimia 16 (mwaka 2009) mpaka asilimia 25 (ifikapo mwaka 2015). Hapa maana yake ni kuwa bado tumepanga kuwa mpaka kufikia mwisho wa mwaka wa utekelezaji (2015) wa mpango huu Wasichana waendelee kufeli Hisabati kwa asilimia 75. Hii haingii akilini hata kidogo. Binafsi ningefikiri lengo lingekuwa ni kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi yeyote atafeli somo la Hisabati na mengine ifikapo mwaka huo wa 2015. Hii inawezekana kabisa ni suala la kuamua na kutenda. Naamini Hisabati ndiyo somo rahisi kuliko yote na ndiyo somo ambalo ukiamua na kujituma una uhakika wa kupata alama ya A bila tatizo.
   
 2. A

  Amanikwenu Senior Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa upande wa Overall Performance mpango ni kuwa ifikapo mwaka 2015 asilimia ya wanafunzi watakaokuwa wanapata division 1 mpaka 3 wawe asilimia 50%. Hapa pia nina wasiwasi kwani kwenye Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari lengo lilikuwa ifikapo mwaka 2010 asilimia 70 ya wanafunzi wanaofanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne wawe wanapata division 1, 2, na 3 Lakini cha ajabu ni kuwa katika mtihani uliofanyika 2010 ni asilimia 11.5 tu ndiyo wameweza kufaulu kwa ngazi ya daraja la kwanza mpaka la tatu. Naona taifa liko shimoni. Kazi ni kulitoa huko.
   
 3. A

  Amanikwenu Senior Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu, mtaniwia radhi kwa wale ambao mlipata F au D katika Hisabati katika mitihani yenu ya kumaliza kidato cha nne.
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Inavyoelekea, hivi sasa elimu ya sekondari imetolewa kafara kwa malengo ya kisiasa; uliwahi kuona wapi mpango wa maendaleo unaandaliwa bila ya kujua kwanza idadi ya watu wanaotarajiwa kufaidika kutokana na mpango huo! Lakini hilo ndilo linalofanyika hapa kwetu kwa upande wa elimu ya sekondari. Kila mwaka idara ya elimu inapanga mapema ni kiwango gani cha ufaulu kinamfanya mtahiniwa awe na haki ya kuingia sekondari. Baada ya matokeo kutangazwa, kunakuwepo na msukumo mkubwa wa kisiasa wa kuhakikisha wote waliofikia kiwango hicho wanapatiwa nafasi. Hata hivyo kwakuwa mda wa maandalizi unakuwa haupo, mambo yote yanafanyika kwa msingi wa kulipua. Matokeo yake ndiyo haya tuliyo yashuhudia mwaka uliopita ambapo karibu asilimia 90 ya watahiniwa wote kwenye mtihani wa kidato cha nne wameshindwa.
   
 5. A

  Amanikwenu Senior Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inabidi wanasiasa wetu sasa wafikie hatua ya kuona aibu na wamuogope MUNGU. Ni muhimu sana hata kama kijana ataishia kidato cha nne awe amepata elimu iliyo bora.
   
 6. A

  Amanikwenu Senior Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ila tunakoelekea Serikali haina njia lazima ihakikishe vijana wetu wanasoma katika mazingira yanayokubalika, wanakuwa na walimu bora na wakutosha na pia wanafanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho kuanzia shule za msingi.
   
 7. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
   
Loading...