Kikwete ahimiza vijana wa Mitandaoni wa CCM wakumbukwe na Rais Magufuli

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,205
1,463
Hongereni wana JF kwa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.

Leo nimemsikia Mwenyekiti Wa CCM akisisitiza kwa Mhe. Rais kuwa vijana Wa mitandao walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha CCM imeshinda kwa kishindo. Ameomba vijana hao WAKUMBUKWE!!

Hilo ni jambo jema lakini naomba tuchangie hoja zifuatazo:-

1. Wako vijana na wakubwa wengi tu ambao walikipigania chama usiku na mchana na hakuna mtu anawajua. Hao nao watakumbukwa na nani???

2. Humu JF tunawajua wengi tu ambao walikuwa wanakipigania chama usiku na mchana mfano Mzee Mwanakijiji nk

3. Je hao nao wapo kwenye list ya Mhe. January Makamba aliyopeleka kwa Rais??? Waje JF wafanye reference!!!

4. Kuna vijana walikuwa CCM wakati Wa uchaguzi humu JF lakini sasa wamegeuka kuwa maadui Wa CCM ??

5. Tunatamani Mhe. January angetupa hayo majina yawe VERIFIED humu JF maana humu hakuna longolongo. Pia tuone STATUS QUO ya hao watu hadi Leo hii!!!!

Wana JF wekeni majina ya wana mtandao Wa JF waliokipigania CCM usiku na mchana na mpaka Leo sio vigeugeu. Watu hawa wanajitolea na hakuna mtu anawalipa. Haki ibaki kuwa haki ili nao wakumbukwe. Naamini jukwaa la JF ni UKWELI NA UWAZI

Queen Esther

New
Kwa jinsi michango inavyoendelea tunaona yapo makundi makubwa manne:-

1. Wapo waliojitolea kwa ajili ya uchaguzi baada ya hapo wamepotea humu JF

2. Wapo wafia CCM tangu uchaguzi mpaka Leo ndani ya uongozi Wa Dr. JPM wanapambana

3. Wapo waliobadili upepo na sasa wanakipiga chama hasa uongozi Wa Dr. JPM

4. Wapo wana UKAWA lakini waliamua kusimama na kweli eg R.B na rodrick alexander

Hilo kundi la pili (wafia CCM)
1 - Mzee Mwanakijiji
2 - Lizaboni
3 - Faiza Fox
4 - Dr. chin
5 - Barbarosa
6 - Yehodaya
7 - Jingalao
8 - Ritz
9 - mmaranguoriginal
10 - kanone
11 - elungata
12 - stroke
13 - borat
14 - msemakweli
15 - queen Esther
16 - chogobilo
17 - simiyu yetu
18 - meningitis
19 - mr. Emmy
20 - LE mutuz
21 - HAMY-D
22 - M2015
23 - teamubwabwa
24 - sky eclat
25 - navy boi
26 - uso wa nyoka
27 - transcend
28 - mcubic
29 - njiwa
30 - msem
31 - maramia
32 - kennedy hincha
33 - kilimbamula
34 - king makolokolo
35 - waberoya
36 - rutashobolwa
37 - pohamba
38 - stroke
39 - Dennis Kajo
40 - abedi kipanya
41 - usher-smith
42 - shikulaushinye
43 - bano
- endelea kuongezea....

Ni vizuri Mhe. January akayaona haya majina. Hawa watu hawakuishia kwenye uchaguzi mpaka Leo wanapiga mzigo kutetea Serikali ya Mhe. Magufuli na hakuna mtu anawajua wala HAWAJAWAHI kuwekewa vocha.

Kama ni kukumbuka hawa wakumbukwe mara mbil. Najua vijana Wa Mhe. Magufli na TISS wanapitia humu naomba salamu ZIMFIKIE Mhe. Rais na Mwenyekiti Wa Chama Dr. JMK

Endelea kuweka majina tafadhali....

Queen Esther
 
Mimi ni mmojawapo nimekipigania chama na naendelea kufanya hivyo lakini si miongoni mwa waliopo kwenye list ya Makamba. Sina haja ya kuwemo kwenye hiyo list list kwa vile nimeamua kufanya kazi hii kwa kujitolea ili niwe huru zaidi
 
waliokipigania chama sio hao vijana wa mtandao wako waliojitolea kwa hali na mali ikiwamo vijana wa chadema na cuf waliochukizwa na ujio wa lowasa kugombea.Hata mwanakijiji aliiunga ccm si kwa sababu anaipenda ccm bali aliona ni bora ccm ya Magufuli kuliko upinzani wa lowasa
 
Wana JF wekeni majina ya wana mtandao Wa JF waliokipigania CCM usiku na mchana na mpaka Leo sio vigeugeu. Watu hawa wanajitolea na hakuna mtu anawalipa. Haki ibaki kuwa haki ili nao wakumbukwe. Naamini jukwaa la JF ni UKWELI NA UWAZI

Queen Esther

Nipo YEHODAYA ukipenda kuniita niite mtoto wa Nyerere ninapigana mbele kwa mbele KUHAKIKISHA NCHI aliyotuachia Nyerere inabaki kwa watoto ,wajukuu na kizazi kilichomeza nembo ya nyerere na kuwa nchi haiendi Kwa fisadi yeyote awe ndani ya CCM au Upinzani
 
waliokipigania chama sio hao vijana wa mtandao wako waliojitolea kwa hali na mali ikiwamo vijana wa chadema na cuf waliochukizwa na ujio wa lowasa kugombea.Hata mwanakijiji aliiunga ccm si kwa sababu anaipenda ccm bali aliona ni bora ccm ya Magufuli kuliko upinzani wa lowasa
Nakubaliana na wewe Mkuu. Kitendo cha CHADEMA kunajisi mapambano dhidi ya Ufisadi wakaamua kumteua fisadi Mkuu kuwa mgombea Urais hakika kilirahisisha mapambano dhidi ya UKAWA. Tuliungwa mkono na wasio wana CCM. Tukiorodhesha makundi yote yaliyosaidia ushindi kwa CCM hakika hatutayamaliza. CCM ni chama pendwa
 
Lowasaa alinunua Magazeti yote my block habari nzuri za Ccm kusikika na zile stori zake za kuji... zisisikike kumbe Mkwere akili nyingi akamwambia January hakikisha kila simu ya Raia ni gazeti la kupashwa habari!
Tunashukuru sana Chifu Mrisho Kikwete na Mama Mzaa Chema Mungu awarehemu huko Mliko!!
Bila ya Jakaya Muda huu Ikulu ingekuwa imejaa Shanga na Samli!
 
Kwikwikwikwikwiiiiiiii! Fisadi Lowasa alipigwa bao la kisigino
 
wakati akiwa anamaliza hotuba yake huko mkoani singida katika uwanja wa namfua sijaona mwenyekiti wa taifa wa CCM na ambaye anamaliza muda wake Rais mstaafu wa awamu ya nne Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtaka Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ahakikishe anawapa zawadi, maslahi na heshima kubwa vijana ambao walijitoa kuipigania CCM katika mitandao ya kijamii ( na hapa alikuwa anamaanisha Jamii Forums kwani huu ndiyo mtandao bora na namba moja Tanzania, Afrika ya Mashariki, Afrika na dunia nzima ) ambao walitumia nguvu yao na kuacha kazi zao usiku na mchana kuipigania CCM humu mtandaoni na hadi kupelekea kuwamaliza kabisa wapinzani hasa hasa ( wana CHADEMA ) ambao walikosa cha kuandika kwani members hawa waliwaweza na kuwashika vilivyo huku wakitoa SIRI za ndani na NYETI za upinzani.

members wenyewe ni hawa wafuatao:

HAMY-D
Lizaboni
GENTAMYCINE

nikiwa kama member humu JF napenda na mimi kuchukua nafasi hii kuwapongeza hao watajwa hapo juu lakini pia napenda kuipongeza Jamii Forums kwa kuweza kuwa na members wa mfano wa kuigwa kama hao na tunaamini kuwa watakuwa ni mfano wa kuigwa kwa sisi wengine tuliopo humu. ukiona hadi Rais mstaafu na Rais aliyepo madarakani anawatambueni basi ni bahati ya aina yake. ngoja na mimi kuanzia sasa nianze kujitahidi kuizungumzia na kuipigania CCM humu JF ili na mimi mwaka 2020 nami niweze kukumbukwa na chama. na ningeshauri vijana wenzangu tusio na ajira hebu tutumie hizi fursa kama za hao members wenzetu tajwa hapo juu ambao walilala masikini na sasa wameamka matajiri baada ya kula shavu na tusipende sana kujihusisha na vyama ambavyo havieleweki, vichanga, vimejaa tu utapeli, ujanja ujanja, ukabila, ukanda na ubaguzi. najuta sana kuwa mwana CHADEMA kwa miaka 11 sasa na nilitegemea nami ningepata japo cheo ndani ya CHADEMA lakini kwa mshangao mimi niliyekuwa naipigania CHADEMA humu nimeachwa na wamechaguliwa watu ambao hata hawakuipigania CHADEMA! narudi rasmi CCM na CHADEMA mtanisamehe.
 
mkoani Dodoma!?mitandao ya kijamii hakumaanisha jf peke yake kuna watu walikipigania chama fb,insta na kadhalika
 
walilala masikini na sasa wameamka matajiri baada ya kula shavu
yaani kikwete anatoa hoja ya kufuja fedha za kodi za wanachi kuwapa wahuni2
hiii kutumbua majipu hakuna maana kabisa,..wafanya biashara wanabanwa kutoa kodi
then pesa zinatumika ndani ccm
kikwete angetoa fedha za chama kulipa fadhila zao tajwa/.,.
hivi kweli tutafika??????
fedha za nchi kutumika kichama
 
u uhuni wa ccm inabidi tuupinge mara dufu
wawakumbuke na fedha za chama ccm
kwani wanamtandao wa ccm wameidia nchi au ccm ebu haya mambo kabla hamjaongea fikilieni kwanza
kikwete awe anawashauri wazuri mambo yakubebana enzi zake za kufuja pesa za umma simazuri
 
Kwa jinsi michango inavyoendelea tunaona yapo makundi makubwa manne:-

1. Wapo waliojitolea kwa ajili ya uchaguzi baada ya hapo wamepotea humu JF

2. Wapo wafia CCM tangu uchaguzi mpaka Leo ndani ya uongozi Wa Dr. JPM wanapambana

3. Wapo waliobadili upepo na sasa wanakipiga chama hasa uongozi Wa Dr. JPM

4. Wapo wana UKAWA lakini waliamua kusimama na kweli eg R.B na rodrick alexander

Hilo kundi la pili (wafia CCM)
- Mzee Mwanakijiji
- Lizaboni
- Faiza Fox
- Dr. chin
- Barbarosa
- Yehodaya
- endelea kuongezea....

Ni vizuri Mhe. January akayaona haya majina. Hawa watu hawakuishia kwenye uchaguzi mpaka Leo wanapiga mzigo kutetea Serikali ya Mhe. Magufuli na hakuna mtu anawajua wala HAWAJAWAHI kuwekewa vocha.

Kama ni kukumbuka hawa wakumbukwe mara mbil. Najua vijana Wa Mhe. Magufli na TISS wanapitia humu naomba salamu ZIMFIKIE Mhe. Rais na Mwenyekiti Wa Chama Dr. JMK

Endelea kuweka majina tafadhali....

Queen Esther

Una utani na akina MUSSA ALLAN wewe
 
duh...sikuwa najua ...kumbe mwanakijiji ni mfia CCM...Alikuwa anajifanya mpinzani huyu
 
Back
Top Bottom