Kikwete aendelee muhula mwingine

Naona umebanwa na swaumu kazana kukazia na mate
 
Msimamo wako haueleweki. Kumbuka muda mfupi uliopita kuna mahali umetoka kuandika hivi:

Mara zote unatakiwa upime ,sio unafuata upepo ,kwa kuwa tu watu wanapiga mayowe pale bungeni ukaona ndio hao wa kufuatwa ,kumbe athari za mwezi mchanga zinawapa shida.

Sekunde moja ni kubwa ikiwa wewe ndio mwenye kura ,hivyo mimi kama raia wa kawaida ninacho ringia ni kura yangu ,nitaipeleka pale ambapopana matumaini ,hadi hapa nikwambiapo au niandikapo basi bado matumaini yapo CCM kuliko kwengine kokote kule ,mwendo wa CCM wa mwezi au mwaka jana sio huu tulio nao.

WaTanzania wengi wataturn katika siku sijazo siku ambazo MTanzania ataanza kufungua macho kutokana na juhudi za Makusudi za Mheshimiwa JK. Tusidanganyane huko kwenye makaki amna kitu.
 
Koma kama ulivyokoma kunyonya ziwa la mama yo JK hafai haijapata kutokea Raisi aliyeshindwa kuongoza nchi kama huyu embu usitufanye tuje tupasuke mioyo

Hivi wewe unamimba naona hasira njenje ! Kama KJ ameshindwa angelikwisha kujiuzulu zamani ,huyu JK si nahoza anaebabaika na mawimbi,ni katika wale manahoza waliovuka maji ya shingo. Na ndio hivyo anayavuka ,sasa mtu kama huyu ndie kiranja anaeweza kuiongoza Tanzania bila ya kukwaruzana.
 
Du! Wakati rada zinaonesha kuwa raisi atakayetangulia kusalmiana na Mzee (Mwalimu) Nyerere pale 'Butiama'
kati ya wastaafu wote ni Kikwete?

 

Urais wa Tanzania siyo Tendo la ndoa useme mtu atafika mara nyingi anavyotaka!..
Damn!
 
Mie nadhani tungerudisha ruksa miaka 5 kisha mr. clean aje ajenge misingi tena kwa miaka 5..... Halafu Jk aisimamie kama ilivyo sasa...........au tuunganishe vyama vyote vya kisiasa. ........ha ha ha..
 

Labda akagombee urais Zanzibar 2015 awe rais wa Tanzania Visiwani.... LOL!
 
Vichaa vingine havina dawa. Mwiba unaishi wapi iwapo unaona makengeza kwa mpendwa wako ambaye licha ya kuchokwa na wananchi amejichoka hata yeye mwenyewe. Huenda nawe ni wale wanaofakamia mabaki na kunenepeana kiasi cha kupofuka na kudhani wote wanaishi kwa vinono kama wewe. Siku moja utaujua ukweli hata kama utakuwa umechelewa. Ila usiwe wa kwanza kulalama.
 
hahaaa mweee ...asante Mwiba kwa kunichekesha leo ...mungu akupe maisha marefu uelendelee kutuchekesha hivi hivi

Ndio maana ukikosekana hapa ninakumiss sana Mwiba, post zako zina akili sana

Inawezekana Mwiba ameamua kuleta ujumbe kwa njia hii ya kuudhi/ kuchekesha watu kulingana na vipi unaichambua mada yake.

Nililoliona mimi, sijui kama amekusudia hivyo au la, ni ujumbe uliomo katika hayo maandishi mekundu.
Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa Katiba Mpya isiwe tayari itakapofika 2015.

Baada ya kazi ya usanii wa ukusanyaji maoni unaofanywa na Tume ya Warioba na ukamilishaji wa uchambuzi wa maoni hayo hadi kufikia kuandika katiba mpya ya Muungano imesemwa itafika 2014.

Kama Rasimu hiyo ya Katiba Mpya ya Muungano itapelekwa kupigiwa kura na pande mbili za muungano. Ni wazi matakwa ya UAMSHO kama hayakutimizwa katiba hiyo haitakubaliwa/ haitapitishwa na wananchi wa huko na hivyo kupelekea 2015 inaingia na uchaguzi mkuu ukiitishwa chini ya katiba ya zamani/hii iliyopo. Likitokea hilo sote tunajua nini yatakuwa matokeo ya Uchaguzi huo.

Je Rasimu ya Katiba mpya itakapokataliwa nini kitafanyika kuhusu uchaguzi mkuu? Na kama upande mmoja utakuwa haukupitisha katiba hiyo je Tanzania bara(Tanganyika) itapasa kuandika Katiba yake? (na kinyume chake,ingawaje Zanzibar wanayo katiba yao tayari)

Mada ya Mwiba inaudhi/ inachekesha lakini pia inaibua fikra ambazo wengine hatujazifikiria.

Tujaribu kuzitizama hizo chachu/ Changamoto alizoibua mwisho wa makala yake fupi. Yakitokea hayo, tutafanya nini?
Tutacheka sanaaa? Tutapigana na kuuana? Au tutakuwa wavumilivu na kukamilisha taratibu za kupata Katiba ya Muungano? Kwa kawaida kupata Katiba ya muungano huwa si rahisi (tunaweza kuchukua uzoefu wa kura za kupitisha Katiba ya EU) ...pengine ni wakati sasa kufikiria kuandika sambamba na Katiba ya muungano, Katiba ya Tanganyika..just in case.
Au?
..WaTanzania hawana budi kumpa tena muhula wa uongozi kwa miaka kumi mingine.Huku tukisubiri Katiba mpya au Tanganyika mpya.
 

Are u mad?
 
Mpe nafasi aiongoze familia yenu,atawaletea maendeleo sana,especialy kama kwenu kuna warembo itakua mpango mzima....
 
Rais KIkwete anastahili pongezi sana especially kwa kutuletea hawa mawaziri wawili ambao ni watendaji sio wanasiasa. Hawa si wengine bali waziri wa Fedha Mgimwa na waziri wa Nishati. Naomba aendelee kuwapunguza wanasiasa na kutuletea watendani ili tuone kasi hii ikiendelea.
 

Kwani lazima aendelee kutuongoza? katiba inasemaje na kwanini tuipindue katiba sababu ya JK tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…