Kikulacho ki nguoni mwako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikulacho ki nguoni mwako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lekanjobe Kubinika, Jul 5, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  TRUE STORY in the late eighties, DSM:
  Kuna huyu bwana mwingine daktari ambaye alikwenda kusoma Urusi digree ya pili. Alikuwa anakaa Flat moja na daktari mwingine milango ikitizamana. Wake zao wote walikuwa wauguzi hospitali moja lakini vitengo tofauti. Hawa mabwana walikuwa ni marafiki wakubwa sana.

  Wa kusoma alimwomba mwenzake kwamba kwa kuwa mkewe hajui kuendesha gari, anamwomba awe anamsaidia pale uhitaji ukijitokeza. Akaitikiwa vizuri sana. Safari ilipotimia, huku nyuma jirani alijituma sana kumsaidia shemeji yake kwa kumpeleka Karakoo na sehemu nyingine kila ilipohitajika. Pia alilazimika kutembelea ndani ya jirani yake ili kujua usalama na kujionea kama kuna mambo mengine shemejiye angeogopa kuyasema ili ajionee mwenyewe na atafute namna ya kusaidia.

  Safari na gari zikaongezeka sana na wakajikuta wako karibu zaidi. Haikuchukuwa muda mrefu wakajikuta wanaanza kutengeneza mikasi. Kwa kuwa wote ni watu wazima walijitahidi kuyafanya in low profile in public. Lakini si unajua kikohozi kinavyosumbua mapaka ukohoe? Bila kutegemea wakanogewa na ikawa mara mbili, mara tatu , mara nne kila siku. Mama mwenye hati miliki ya bwana yule alilazimika kukaa na njaa mfululizo kama vile mwenza kasafiri, wakati mwenye mume aliyesafiri ndio aliona bukheri wa afya kuliko mume akiwapo.

  Mke wa huyu daktari mtoa msaada alisikia pia kwamba fimbo yake inatumiwa na jirani yake, tena basi wamama hawa walisoma pamoja chuoni na wakajikuta wanafahamiana vizuri. Ujirani wa makazi yao ukawafanya wawe marafiki zaidi. mama akamuuliza mumewe kama kweli anayoyasikia mitaani ni kweli. Mumewe alipobanwa alilazimika kukubali. Mkewe akamwambia aachane na mambo hayo haraka sana japo amemsamehe. Yule bwana akasema akijitetea, kwamba ataacha lakini asingeweza kuacha mara moja kwa sababu kufanya hivyo kungemuumiza sana mwanamke jirani, Akaahidi kuachia polepole mpaka jamaa akirudi ndipo asitishe kabisa. Ilikuwa pata shika usemi huo kukubalika.

  Wapambe walianza kumtonya jamaa akiwa bado masomoni, hasa Matron wao wa harusi. Aliporudi jamaa kutoka Urusi, aliwajia juu wapambe akiwasakama kwamba hawaamini maneno yao na wanaihatarisha ndoa yake. Akafanya mpango kumbamisha kituo cha kazi mkewe akafanye kazi mbali na wabaya wake.

  Je, kama ingekufika wewe ungefanyaje? Nimeepusha undani watu waliopita maeneo yale lazima watakumbuka songombingo hilo, ni pamoja na kutunza heshima ya JF lakini kutumia matukio hayo kujifunza kitu katika maisha.

  USIMWAMINI MTU!!!!!
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Duh hii hatari sana ...kwa hiyo jamaa hakuamini kama wife wake alikuwa anamegwa ?
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,789
  Trophy Points: 280
  Kwenye bold: Huyu daktari aliyeenda masomoni atakuwa ana upungufu wa akili. Mbuzi umuachie fisi mwenye njaa kali?
  Kwenye red: Daktari aliyechiwa mke naye taahira: Unawezaje kumuambia mkeo eti utaacha taratibu kumega mke wa mtu, tena mke wa rafiki yako?

  Nashindwa kujibu swali lako kuwa kama ingekuwa mimi ningefanyaje kwakuwa hujawa specific kuwa kama ningekuwa nani kati ya hao wanne.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hehhehhe umeniachia kali na 'mama mwenye hati miliki' lol

  anyway mimi kwa upande wangu nakubaliana na wewe............usimuamini mtu. kaka yako mzazi usimuamini na mkeo kiasi hicho achilia jirani!

  akiwemo mwanamme na mwanamke kwa ukaribu lazima shetani atapita tu
   
 5. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hawa madoctor wote na wake zao naona wana akili za kiaina hivi maana mi si imagn itakuwaje mr anaamua kukiri anatoka nje na ataacha taratibu? how come?
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,789
  Trophy Points: 280
  Samahani naomba kufahamishwa, kaka mzazi ndio nani?
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Si unajua kipenda roho hula nyama mbichi, na mapenzi hupofusha macho. Mapenzi ni dumuzi wa akili. Kuna kumuamini mwenzio kupita kiasi hata usisikie unachoambiwa tofauti. Huyu daktari alikuwa mbogo kwa mtu yeyote anayeonekana kutaka kuongelea hayo, watu wakaamua kunyamaza tu. Namuona mama huyo hata leo hajastaafu bado, tena sasa ana cheo kikubwa sana kwenye system za uuguzi hospitalini hapo. Alirudishwa baadaye kutoka alikohamishiwa. Yote ni maisha. Tatizo ni je, wameacha kamchezo kale?
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu... dakitari aliyekua urusi alichagua lililo bora sana!!! hakutaka mtu kuingilia ndoa yao, na ameonyesha imani kwa mkewe, time will tell kama alikua right or wrong

  Ila naskia kusisimka maana siamini kwa namna yoyote ile [no disrespect to any woman in this world] mtu kukabidhi familia yake kwa mwanaume mwingine, its like you are hadning over your responsibilities to your deputy. before leaving a family kwa long term lazima mama awezeshwe kuishi mwenyewe with minimum dependency kwa wengine hata kama ni ndugu
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ni kweli De Novo; vinginevyo utawataka ubaya watu bure ni heri ukamwacha yeyey mwenyewe ili kama kuanzisha aanzishe kwa matakwa yake moja kwa moja lakini ukishawaweka akribu yakitokea haya utajilaumu kwa kuweka misingi ya hilo kutokea!
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kamanda tuko pamoja.. we hebu fikiria unakabidhi kabisa maa kwa mshkaji wakati unajua physiology ya binadamu na mahitaji mengine ya jamii. bora ungeacha tu
   
 11. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  :closed_2:
  Hayo yanatokea sana kwenye jamii yetu, mke wa mtu sumu sana, ningekuwa mimi ningemkojolesha dagaa jamaa au ningemchukulia ile dawa ya kunatana ya mbeya waadhilike. Toooo bad.
   
 12. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Wewe unajiweka wapi kwenye hili anguko?
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,789
  Trophy Points: 280
  Hivi wakinatana si ndio wanazidi kufaidiana?
   
Loading...