Kikosi Kazi kipo Kisheria

Kikosi Kazi kipo Kisheria

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,393
Reaction score
4,085
Je ni kweli kuwa kile kikosi kazi kilichoundwa na Msajili wa Vyama kujadili Masuala ya Katiba Tume huru na Mikutano ya Vyama vya Siasa HAKIPO KISHERIA kutokana na kutotungiwa Sheria na BUNGE na pia Wajumbe wake Kutokuapishwa kama ilivyokuwa kwa Tume ya Jaji Warioba?

1669367412536.png
Kikosi Kazi ni zao la mapendekezo ya Kikao cha Wadau wa Demokrasia kilichofanyika Disemba 15 - 17, 2021 jijini Dodoma. Kikao hicho kilikutanisha watu wa vyama siasa nchini, hata hivyo Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe, hakuwepo. Kikao kilifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, aliyatangaza majina ya wahusika wa Kikosi Kazi Desemba 23, 2021 na Kikosi Kazi kilianza kazi Januari 10, 2022. Uteuzi huo ulifanywa kutokana na dhamana aliyopewa Msajili wa vyama vya siasa na wajumbe wa kikao cha wadau wa demokrasia.

Kikao cha Wadau wa Demokrasia kilikaliwa baada ya kuwa na sintofahamu ya demokrasia na uhuru wa vyama vya siasa nchini. Na ni moja ya kazi ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa Kuwa kiungo kati ya Serikali na Vyama vya Siasa nchini. Kikosi Kazi kiliundwa ili kupitia hoja za wadau wa demokrasia na kupeleka mapendekezo kwenye Baraza la Vyama vya Siasa ambalo lilikuwa na kazi ya kuwasilisha mapendekezo hayo serikalini.

Baraza la Vyama vya Siasa liko ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ambalo lina jukumu la Kumshauri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya mgogoro inayotokea kwenye vyama vya siasa; Kumsahuri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya masuala yenye maslahi kwa Taifa kuhusiana na vyama vya siasa au kuhusiana na hali ya kisiasa nchini; Kuishauri Serikali kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya kupitishwa kwa marekebisho na utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria zingine zinazohusu masuala ya vyama vya siasa; Kushauri juu ya kanuni zinazosimamia masuala yanayohusu vyama vya siasa; na Kutoa taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya uendeshaji wa chama chochote cha siasa.

Kisheria Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu la kutatua migogoro ya kisiasa, na aliitisha kikao ili kujua tatizo la malalamiko yaliyokuwepo kwenye uwanja wa siasa, ambapo mapendekezo ya kuunda kikosi kazi yalitokea hapo ikiwa ni moja ya namna yake ya kutatua mgogoro wa kisiasa ulikuwa unaendelea hasa kwa wadau wasiasa kulalamikia demokrasia
 
Back
Top Bottom