mbona naona nabii ana koti kama la Chadema?
Hivi vikombe sasa vinaelekea kubaya. Tumekuwa watu wa kuamini vikombe kama watu enzi za kale! Hii ni aibu sana.
Nabii Joshua Mwantyala akiwanyunyuzia maji ya tiba wananchi waliokusanyika katika mkutano wake wa Neno la Mungu la uponyaji na kuwaombea wagonjwa wote wenye magonjwa sugu kama vile Ukimwi, Kansa na mengineyo. Nabii Joshua juzi alianzisha huduma ya tiba yake inayojulikana kama majibu ya tiba ya maajabu ya Loliondo ambapo yeye hutoa matone ya maji ya uponyaji.ambayo huwanyunyuzia wagonjwa vinywani(Picha: Regnald Miruko)
Nadhani tatizo halipo kwa watoa vikombe au matone, tatizo hii nchi ina malimbukeni na majuha wengi ambao hupapatikia mambo bila kutafakari. Mfano mdogo ni pale unapokuta tukio lolote barabarani na mkusanyiko mkubwa wa watu waliokatiza safari zao bila sababu za msingi, leo hii ukisema mavi ya kunguru yanatibu magonjwa sugu hutakosa watu majuha.
Usitumie neno hili "MAJUHA", hayajakukuta na mshukuru Mungu kwa hilo. Kwa kweli kumekuwa na tabia ya kuwabeza watu wanaotafuta suluhu za maradhi waliyonayo. Katika nchi kama yetu ambapo Serikali imeshindwa kuwa na huduma za afya za kueleweka, unategemea nini? Tunaishi kwa kuamini zaidi juu ya uweza wa Mungu, hata serikali inapokumbana na tatizo la umeme huwa wanasubiri uwezo wa Mungu katika kuleta mvua. Takriban watanzania wengi wana matatizo ya afya ambapo wamekosa tumaini, na hii inadhihirika pale ambapo linajitokza tumaini jipya. Wako watu wana uwezo wa fedha lakini wanakosa suluhu ya afya zao kwa magonjwa yanayowasumbua, unategemea watafanya nini?
Jambo la msingi ni kumshukuru Mungu kwa wewe ambaye afya yako inaendelea vyema na bado hujapata maradhi ambayo wanasayansi wameshindwa kutoa suluhu yake. Lakini kumbuka yanaweza kukupata hata wewe, hujatenda mema sana kwa Mungu.
Tutumie kauli njema katika kuwaelimisha wale ambao tunafikiri wanapotea na huku tukiwapatia tiba mbadala.
Charlatans at work..deceiving wadanganyika na serikali ikiwa kama haipo. Biz as usual.
Wanaeza kwenda kwene hiyo tiba na magonjwa kumi wakarudi na magonjwa ishirini..kwanza hizo chupa za maji tu zinaeza kuwa source ya madhara na maambukizi..btw the nadhani ni grade ambayo zinatakiwa zitumike mara moja tu..wajinga ndio waliwao.
Nadhani tatizo halipo kwa watoa vikombe au matone, tatizo hii nchi ina malimbukeni na majuha wengi ambao hupapatikia mambo bila kutafakari. Mfano mdogo ni pale unapokuta tukio lolote barabarani na mkusanyiko mkubwa wa watu waliokatiza safari zao bila sababu za msingi, leo hii ukisema mavi ya kunguru yanatibu magonjwa sugu hutakosa watu majuha.