Kikombe cha babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikombe cha babu

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by AmaniGK, Mar 23, 2011.

 1. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Malenga nawasalimu, Kwa jina lake Rabuka
  Nimeona nijihimu, japokua kushakucha
  Kwa hili jambo adimu,linalotusuka suka
  Kikombe, kikombe gani, Malenga nielezeni

  Kikombe, kikombe gani, atoacho Mwasapile
  Ni nini kilicho ndani, naombeni nifunzile
  Nambieni kwa undani,nende zangu na dumule
  Kikombe kikombe gani,Malenga nielezeni

  Mugariga mesikia,ni sumu ya kuwindia
  Wasonjo wanatumia, nyama pori tafutia
  Mishale waipakia , nyama pori tafutia
  Kikombe kikombe gani,Malenga nielezeni

  Mamia na kwa malaki, Semunge wameshafika
  Kwa sasa kilichobaki, Ushuhuda kutufika
  Au paka ende Kibaki,Ndio labda tasituka
  Kikombe kikombe gani, Malenga nielezeni

  Sio kwamba sina jero, ya kulipia kikombe
  Naweza kopa kwa Yero,Au Mudy shombeshombe
  Sitaki kuwapa kero,Kuelewa niwaombe
  Kikombe kikombe gani, Malenga nielezeni

  Kadi tamati wa tama, Mwisho mimi nimefika
  Mebaki nashika tama, Moyo warukaruka
  Naomba zenu hekima, Nipate kushawishika
  Kikombe kikombe gani, Malenga nielezeni   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda kaka, kwa kuwa inasadifu ya sasa... Kip it up malenga!
   
Loading...