Kikao cha bunge kinakaribia

cencer09

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
3,622
1,751
tutegemee nini watanzania safari hii?kwanza tayari waziri wa nishati na madini kaishaanza kutoa msimamo kuwa hataomba radhi kwa bunge wakati kikao kikianza baada ya tetesi kuvuja kuwa kamati au tume ya bunge iliyokuwa inaoongozwa na mheshimiwa Brigadia Ngwilizi mojawapo ya mapendekezo yake ni kumtaka profesa aliombe radhi kwa kwa tuhuma kuwa amewadhalilisha wabunge kiwa kuwaita wezi.
Hili naona kama linataka kumalizwa mapema kwa sababu linahisi maslahi ya waheshimiwa wabunge hasa wakiwemo wa chama tawala ambao kwa siku za karibuni shutuma za ufisadi na wizi kwenye chama hicho ni wimbo.
Hebu fikiria wakati wa uhai wa uongozi wa Mwalimu Nyerere alivyokuwa anaipiga vita rushwa tena kwa vitendo lakini leo hii mwenyekiti wa ccm akiwa kwenye mkutano wa uchaguzi analalamikia kuwa hata wanawake nao wnachaguliwa kwa rushwa,mind you ANALALAMIKA SI KUCHUKUA HATUA,ANA JESHI,ANA POLISI,ANA TAKUKURU,lakini anabaki na yeye kulalamika kama mimi na wewe.
ni amiri jeshi ambaye anatakiwa aonyeshe njia katika katika kupiga vita rushwa.
tutoke huko turudi kwenye bunge,aliyekuwa mbunge wa arusha mheshimiwaLema aliwahi kumuuliza swali waziri mkuuPinda kwa nini serikali inaua wananchi wake.
Spika akahemka na kumpamuda haraka wa kuwasilisha ushahidi la sivyo atachukuliwa hatua,mpaka mahakama ilipotengua matokeo spika hakutaka tena kuweka wazi tujue ushahidi huu.
halikadhalika mhTundu lissu kama waziri kivuli wa sheria na katiba alitoa msimamo wa kambirasmi ya upinzani kuwa baadhi ya majai wanateuliwa bila kufuata vigezo,bunge zima upande wa magamba ukaja juu na akapelekwa kwenye kamati ya haki na kinga ya bunge kushtakiwa,hadi mwenyewe akadai anataka kesiyake isikilizwa ili apate kuwaelezea watz ukweli wa kauli zake.sijui itatokealini.
Ona uharaka wa mwenyekiti mh Mhagama wakati mnyika alipomtuhumu Mh Mchemba wakuleta ushahidi kwenye kiti cha spika,hakupewa nafasi kudhibitisha na kama akishindwa kutokana na kanuni za bunge zfute,wapi kaingia huyo hapo hapo kamatia.
kuhusu kauli zakuudhi na kudhalilisha nadhani kwa mtazamo wangu mimi kiti cha spika hasa naibu wa spika anaongoza kumbuka incidence hizi mbili.kama kiongozi kudiriki kumuita mbunge wa kuchaguliwa na wananchi tena wa mjiniwalikosoma na maendeleo zaidi si Kongwa vijijini,mbunge wa Kawe halima Mdee Eti ona wananchi mmechagua kituko.je ni njia sahihi ya kumuelekeza mheshimiwa aliyekosea?hapana katika kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani.
pili kunambungemmoja wa ccm ambaye alitamka Bungeni kwenye Mchango wake kuwa mwenye uchungu akazae.hata alipokumbushwa kuifuta kauli ya kudhalilisha naibu spika aliitetea na kusisitiza kuwa kweli mwenye uchungu akazae.
Hapa amewadhalilisha akina mama,wabunge na watanzania tuliokuwa tunasikiliza lakini ile kiu ya kutaka kuwashalilisha wapinzani yaani ukada umemjaa kiasi kwamba anatetea.
angalia mahakama ilivyotumiwa na serikali pamoja na spika wao ili kutunyima haki watanzania,gazeti la mwanahalisi limefungiwa kwa kufanya kazi ya polisi ambayo polisi aidha wameshindwa au wanaogopa kufanyakazi ya kuwakamata waliojaribu kumuua dk stephen Ulimboka.
Spika kwakisingizio cha mahakama ambako kapelekwa chizi walizuia wawakilishi wa wananchi wasilizungumzie.
Mwisho wa mwezi huu wanakutana tutegemee jipya la maana wanatz au yale yale tusipoteze mudawetu?
 
Back
Top Bottom