Kijana(wa kiume) kuwa makini sana ufikapo kipindi cha miaka 24 hadi 29

DiasporaUSA

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
23,381
29,627
SINTOFAHAMU MAISHANI KATI YA MIAKA 24 HADI 29

1. Umri mgumu zaidi katika maisha yako ni kati ya miaka 24 hadi 29 hivi. Presha ya kuwa mtu wa aina fulani au levo fulani ya maisha katika umri huo ni kubwa sana.

2. Kila ukitazama unaona watu wengine wanaishi vizuri sana, tena maisha unayoyatamani na wanayafurahia. Wewe unahisi kama unasukuma siku tu.

3. Umeomba kazi sehemu kibao lakini kila ukijibiwa ni jibu la kwamba umekosa na tena sehemu nyingine hata jibu hupati.

4. Bahati mbaya sana huu ndio muda au umri ambao wengi wanachanganyikiwa kabisa. Muda ambao kama mtu hana subira au umakini wa kutosha anajikuta katika ulevi wa kupindukia au madawa ya kulevya au kilevi chochote.

5. Kwa sababu kukata tamaa kunakuwa kwingi unajikuta unatafuta njia mbadala za kukimbia uhalisia. Unatafuta ulevi wako. Pombe! Madawa! Bangi! Kamari! Mwanamke!

6. Mbaya zaidi unakuta baadhi ya watu uliosoma nao wamepata bahati ya kupata kazi nzuri. Jinsi muda unavyoenda unahisi idadi ya marafiki zako inapungua –

7. Sio kwamba marafiki wanakutenga lakini wewe mwenyewe tu unaona bora ujitenge kwa namna hali ilivyo.

8. Hebu fikiria utafanya nini ukiwa katika WhatsApp group na marafiki zako wanajadili kuhusu safari ya kula starehe Zanzibar wiki ya wiki iliyopita

9. na hapo wanaendelea kujadili mipango ya kuchagua wikiendi fulani wakavinjari Ngorongoro au Serengeti na wake au wapenzi wao. Wewe utachangia nini wakati hata hujui mlo wako kesho utatoka wapi?

10. Mara nyingi unajikuta chat za kwenye group WhatsApp kama hizo unazisoma kimyakimya mwenyewe kama msalaba kwenye kaburi.

11. Kidogo kidogo unagundua hao watu na hili group la WhatsApp sio saizi yangu

12. kwa sababu kadiri unavyokaa karibu na group kama hilo au watu wa aina hiyo ndivyo jinsi ambavyo unazidi kupata au kujipa presha.

13. Si unajua zile stori za kwenye magroup ya WhatsApp za house party zikianza inabidi ujifanye bubu maana unawaza ikifika zamu yako hili kundi la watu 15 litaenea wapi katika chumba chako kimoja ulichopanga Sinza kwa Remi.

14. Ushawahi kukaa kwenye kundi la watu wanajadili iPhone mpya au jinsi ambavyo Fastjet wanatoa huduma mbovu?

15. hapo unasikia moyo wako unakwambia “kijana, huu ni ule muda wa maumivu ya moyo, huwezi kutafuta group ambalo wanajadili bodaboda?

16. Ila unabaki tu katika hilo group, unatulia kimya unatazama raia wanavyojadili maisha yao bora na wewe unakuwa kama secretary anavyoandika summary za vikao.

17. Unasahaulika kabisa kama kilema aliyesinzia kwenye daladala (huwa hadi wanapitishwa vituo)

18. Mara moja moja unakuta mmoja ya marafiki zako anakuuliza kama unahitaji bia nyingine

19. unawaza sijui niseme hapana niondoke zangu niende home? Ila unawaza tena home nikafanye ishu gani mida hii?

20. Unajikuta unajibu: “Yes kaka, ngoja ninywe moja ya mwisho”. Mwongo!

21. Kosa kubwa unaloweza kufanya kipindi kama hiki bro ni kujaribu kuwa na mpenzi.

22. ukweli ni kwamba mtu ambaye anapitia nyakati kama hizi kwenye mapenzi ataleta tafrani tu. Mapenzi ni furaha na ili umpe mtu furaha lazima kwanza wewe mwenyewe uwe na furaha. Huwezi kumpa mtu kitu ambacho huna.

23. Huu ndo ule wakati ambao utaona wasichana ambao ungetamani kuwa nao wanatoka au wanaolewa na wanaume waliokuzidi umri zaidi ya miaka 10.

24. Halafu ndugu yangu huwezi hata kuwalaumu. Ni kwamba tu spidi ya maisha yako haiendani na malengo yao. So inabidi tu uelewe.

25. Wasichana wengi ambao utakuta nao muda kama huu tena kama una bahati sana wanaweza kukuvumilia mpaka utimize miaka 28 au 29,

26. na ukitimiza 29 maisha yako bado hayasomeki jiandae kuachwa.

27. Lakini katika umri huu unajifunza mengi sana kuhusu maisha.

28. Maisha yanakufunza mengi kuhusu uvumilivu, na kushukuru Mungu wako kwa kile unachopata kila siku,

29. yanakufundisha kitu kuhusu urafiki, mapenzi, kazi na kujitambua mwenyewe.

30. Huu daima ndio wakati wako wa kuamka au kuanguka moja kwa moja kwenye maisha kutegemea nini utaamua kufanya.

31. Namna utakavyoishi maisha yako kati ya miaka 30 hadi 39 na kuendelea itategemea sana namna ambavyo utayashinda maisha haya ya majaribu mengi kati ya miaka 24 hadi 29.

Never giv up....

 
Ulichoongea ni ukweli mtupu mkuu ila mwisho hujatoa mawazo yako sas wafanye nn kukabiliana na hali hyoo katika huoo umri..umri wa kijinga saana huoo,kuna cku nlitaman ninunue lamborghin wakat cjapat ata kazi nakula kwa baba wala cna source yoyte ya income..nkatafakali nkajiona mjinga saana
 
Back
Top Bottom