Kijana tambua nguvu uliyonayo katika maamuzi ya nchi yetu

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Vijana nguvu ya mabadiliko dunuani

Kuna kazi ya kutumia nguvu kubeba viroba vya unga na mahindi vyenye uzito wa 100kg kwa Bakhresa kwa siku wanalipa elfu 10, ila unalipwa kila baada ya wiki. Kula na nauli unajitegemea, ukipiga hesabu hapo kuanzia nauli Tsh. 1, 500/+maji Tsh. 1, 000/+Chai 1, 500/+Chakula Tsh. 2, 000×2+matumizi mengine ya nyumbani labda anapanga chumba cha Tsh. 30, 000/ kwa mwezi÷30=1, 000/, maji na umeme Tsh. 1, 000/.

Hapo hakuna mavazi na matumizi binafsi kama pombe, juice na sigara, kwa watumiaji mpaka hapo matumizi ya kila siku ni Tsh. 9,500, anabaki na akiba ya Tsh. 500/ kila siku. Kwakuwa elimu ya nchi yetu ni tegemezi, haiandai vijana kujitegemea, mtu atajiona analipwa Tsh. 300,000/ kwa mwezi lakini ukweli ni kwamba akiba yake kwa mwezi ni Tsh. 15, 000/.

Akitaka kununua na kiatu na nguo atajikuta anadaiwa, matokeo yake atalazimika kumuibia muajiri ili aweze kukidhi mahitaji yake ya msingi. Kama ni kampuni au shirika litafilisika, serikali itakosa mapato na ajira itakoma hapo ni kwa kijana ambaye hajaoa, sasa mwenye familia sijui nitamchambua mbeleni.

Kwa msingi huo niambie kama kijana anayetegemea kuwa na familia baada ya miaka 20 anaweza kuwa na akili timamu? Hawa ndio kundi kubwa linalobebwa na wanasiasa ili washinde mitandandaoni wanatukana wakosoaji wa watawala, wanaeneza uongo na kupinga ukweli.

Hawa ndio hutumika kuteka na kuua ndugu zao, nasema hawa vijana akili zimevurugwa na wahuni wanaolazimisha kubaki madarakani wakati uwezo wao wa kuongoza umegota, wanatembelea uzoefu hawana tena future, hawaoni mbele macho yao yameishia kwenye mali walizochuma kwa udhalimu.

Siku zote wamejificha kwenye kivuli cha uzalendo huku nafsi zao zikipingana na matendo yao, wako tayari kuhonga pesa ukikataa wataondoa roho yako.

***Turudi kwenye hoja ya kazi za ubebaji.

Kiukweli hizi zilikuwa kazi za Warundi na Wanyarwanda kule kwetu Kagera, hata mashambani walifanya wao, sasa Watanzania wamekuwa makuli katika nchi yao. Nikiwauliza humu ndani nani yuko tayari yeye au mtoto wake kufanya kazi ngumu za ubebaji magunia mazito kuliko uzito wenu au kuendesha bodaboda hakuna ambaye yuko tayari.

Swali dogo tu kama sisi na watoto wetu hatuko tayari kufanya kazi hizi hatari kwa afya zetu tunataka wafanye kina nani? Kama Warundi na Wanarwanda wanaotaka kazi hizi hawawezi kuzipata tena? Kwanini mwanao aliyemaliza chuo asiendeshe bodaboda? Inauma kuona kijana mwenye degree akiendesha bodaboda au kubeba magunia mazito ili apate mlo.

Nchi inaongozwa na watu wasio na maono ndiyo maana rasiliamli za nchi zinanufaisha wezi wanaoishi kwa ukwasi na mapesa yasiyojulikana idadi yake na wageni huku wazawa wakiishi kama mashetani katika nchi yao.

Nitaandika huko mbeleni ila nasikia moyo wangu umefura kwa hasira kuona vijana wachache wanatumiwa kuhujumu kundi la vijana kwa maslahi ya matumbo yao huku wakisahau kuna kesho hawa wanaowatumia wakiona nguvu zimeisha huwasusa na kugeuka ombaomba kushinda vijiweni wakiwapiga wanasiasa mizinga huku wakisubiri kifo.

Vijana zinduka, achana na wahuni ambao wamejificha kwenye vyama kama CCM genge hatari lisilo na uchungu na nchi yetu.

Najua mtatumiwa kuunda Vikosi haramu vya kusaidia wezi kubaki madarakani (asomaye na afahamu) mtalipwa vijisenti uku mkimwaga damu za ndugu zenu na kuwaachia ulemavu wa kudumu na pengine vifo, nawambia hamtapata amani milele, mtahukumiwa na dhamiri zenu mpaka mnaondoka duniani.

Nini kifanyike ili kuwepo na amani sio utulivu
1. Tuungane kupinga wizi kwa wanasiasa wanaotumia siasa kuzika ndoto na mwelekeo wa kizazi hiki na kijacho.

2. Tusimame katika kweli, mkatae kuhongwa kunakowapelekea kuwa watumwa wa wanaowahonga.

3. Tulinde raslimali zetu kwa wivu mkubwa.

4. Acha kutumika kama makarai.

5. Jitambue wewe ninani na kwanini upo, komboa wakati kwa kutengeneza mfumo mzuri wa familia isiyo tegemezi.

6. Kuwa jasiri na kusimamia unalohamini bila kuingiliwa na mtu yeyote kwa maslahi binafsi.

7. Acha uoga ambao uzaa unafiki na mwisho mauti. Tusimame kwa pamoja na kudai Katiba Mpya.

8. Kwa upande wa maendeleo chagua mtu sio chama hii itasababisha mtu afanye kitu kwa kukumbukwa kwa kuwa chama huwa hakina kumbukumbu.

9. Tenga muda wa kutafakari nyakati zilizopita umefanya nini na kwa faida ya nani!
(B) Wakati uliopo unafanya nini na kwanini?
(C) Wakati ujao kwa kumbukumbu ipi?

10. Mwisho, tumia akili zako vizuri kwa kukomboa wakati Huku ukijua kuwa kila muda unaopita ama umeutumia vizuri ama vibaya, utautolea hesabu baada ya ujana wako, utatamani kurudi nyuma lakini utakuwa umechelewa, utahuzunika lakini haitasaidia, utakutana na majina mengi usiyoyapenda lakini utalazimika kuyakubali kwakuwa ulitumia muda vibaya kwa faida ya wengine.

Wwisho utakuwa unaamka asubuhi unaenda kijiweni kusubiri kusimulia yaliyopita huku wenzako wakisimulia yaliyopo na yanayokuja watakuona hauna maana, hata kukusikiliza wataacha, aliyekuwa anakupa 10,000/- hautamuona kijiweni, badala yake mtoto wake ndiye atakuwa mtawala. Atapitia kijiweni mala moja kwa mwaka na kuwaachia ele ya kahawa na gongo ili mlewe msahau shida zenu kwa muda.

Katikabakama naishia apo mwenye masikio asikie.

IMG-20230901-WA0107.jpg
 
Awa ni vijana waliotumiwa vibaya na wanasiasa lakini leo future yao imeishia apo. Lakini wanasiasa wapo wanapeta wao na familia zao wanalia na kuomboleza. Kijana jitambue acha kutumika kama dodoki na karai.
 
Back
Top Bottom