Kijana kushindwa sio kosa, bali ni nafasi nyingine ya kukufanya usikate tamaa

Bonge La Afya

Member
Dec 19, 2016
35
83
Mafanikio ni kuchagua, ni kweli unaweza kuwa una hali ngumu ya maisha kiasi cha kuona wewe si kitu tena, ila jiulize ?, ni wangapi wamepitia shida nyingi kama wewe tena walizaliwa
familia masikini haswaa lakini hawakuchoka kujaribu na leo hii tunawaita matajiri na watu wenye mafanikio zaidi duniani.

Ebu sikiliza sentensi hizi kutoka kwa watu hawa mashuhuri zitakazo kuaminisha kuwa kumbe hata wewe unaweza kuishi ndoto yako.

"Nilibakwa nikiwa na miaka 9 lakini leo mimi ni mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani"- OPRAH WINFREY!

"Sikumaliza elimu yangu ya Chuo Kikuu lakini mimi ndiye binadamu tajiri kuliko wote duniani" - BILL GATES!

"Nilikuwa napata matokeo mabaya sana darasani wakati nilipokuwa shule ya msingi lakini bado mimi ni Daktari Bingwa wa Upasuaji duniani" - DR. BEN CARSON

"Nilimwambia baba yangu tutakuwa na mali na utajiri mkubwa lakini hakuamini, leo hiyo ndiyo hali halisi"
- CHRISTIANO RONALDO

"Nilikuwa mhudumu kwenye mgawahawa wa chai ili kulipia ada za mafunzo yangu ya mpira lakini leo mimi ni mchezaji bora wa dunia" - LIONEL MESSI

"Nilikuwa nalala chini kwenye vyumba vya marafiki zangu, natafuta chupa tupu za soda nipate chakula, pesa na mlo wa bure wa kila wiki lakini bado mimi ndiye mwanzilishi wa APPLE" - STEVE JOBS

"Walimu wangu waliniita mwanafunzi mjinga na asiyejiweza lakini bado nimekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza" - TONY BLAIR

"Niliendesha TAKSI ili kulipia ada yangu Chuo Kikuu lakini leo mimi ni Bilionea" - MIKE ADENUGA.

Kushindwa au Vikwazo vya nyuma ni mambo yasiyo na nafasi kwa UWEZO mkubwa uliomo ndani yako. Kwa mtu anayeamini, kila kitu kinawezekana. Ni tunu ulizonazo na talanta ulizopewa ndizo ufunguo wa maisha yako. Usiende kukopa shaba kwa jirani wakati umeacha dhahabu nyumbani kwako, tumia dhahabu
 
Mi demu amenikimbia na kunidharau kisa ramani zangu hazisomeki kwa sasa.. Nilijisikia vibaya kwa muda mrefu pia na moyo wangu kufadhaika na kujiona mnyonge sana.. Nilipo jaribu kumpigia simu angalau ni m'promise good things alikata na wakati mwingine hakupokea kabisa.. Kuna kipindi alinitumia text kuwa hawezi kuwa na mimi tena kwa sababu sina good future... Sasa Jennifer popote ulipo kaa ukijua mungu hana ubaguzi hata mimi mungu ananipenda pia na ninakuomba uishi miaka mingi ili uone utukufu wa mungu live tena bila chenga.. Sitasahau kauli yako uliniita mchunga mbuzi..(Bwana ndie mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu... Zaburi 23:1...
 
Kweli kabisa mkuu hakuna kinachoshindikana chini ya jua cha muhimu ni kuwa na malengo na kutokukata tamaa.
 
Mi demu amenikimbia na kunidharau kisa ramani zangu hazisomeki kwa sasa.. Nilijisikia vibaya kwa muda mrefu pia na moyo wangu kufadhaika na kujiona mnyonge sana.. Nilipo jaribu kumpigia simu angalau ni m'promise good things alikata na wakati mwingine hakupokea kabisa.. Kuna kipindi alinitumia text kuwa hawezi kuwa na mimi tena kwa sababu sina good future... Sasa Jennifer popote ulipo kaa ukijua mungu hana ubaguzi hata mimi mungu ananipenda pia na ninakuomba uishi miaka mingi ili uone utukufu wa mungu live tena bila chenga.. Sitasahau kauli yako uliniita mchunga mbuzi..(Bwana ndie mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu... Zaburi 23:1...
Usikate tamaa bro iko siku nawe utafanikiwa na katika maisha changamoto hazikosekani cha muhimu ni kuganga yajayo.
 
Mi demu amenikimbia na kunidharau kisa ramani zangu hazisomeki kwa sasa.. Nilijisikia vibaya kwa muda mrefu pia na moyo wangu kufadhaika na kujiona mnyonge sana.. Nilipo jaribu kumpigia simu angalau ni m'promise good things alikata na wakati mwingine hakupokea kabisa.. Kuna kipindi alinitumia text kuwa hawezi kuwa na mimi tena kwa sababu sina good future... Sasa Jennifer popote ulipo kaa ukijua mungu hana ubaguzi hata mimi mungu ananipenda pia na ninakuomba uishi miaka mingi ili uone utukufu wa mungu live tena bila chenga.. Sitasahau kauli yako uliniita mchunga mbuzi..(Bwana ndie mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu... Zaburi 23:1...
Sorry bro, japo hata mimi demu nilie nae nimemnyang'anya mtu. Dunia ni kama uwanja wa vita, wakati mwingine ukiwa mr. Nice guy utakufa peke yako.
 
We una fikiri ningefanya nini? Na mtu mwenyewe kaamua kuondoka?? Ninge mlazimisha vip abaki na mimi..??
 
Back
Top Bottom