Kijana haikikisha ndoto zako zinatimia

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
6,725
2,000
najua kila mtu kuna ndoto zinazoisumbua akili yake. simaanishi zile picha zinazokuja usingizini bali ndoto ninazojaribu kuzielezea hapa ni yale mawazo makubwa ya mafanikio ambayo yanatawala akili za watafutaji wa maisha. watu wengi tunashindwa kuzifanya ndoto zetu zitimie kwa kupuuza baadhi ya mambo yanayotutokea katika maisha yetu.

Utakuta labda umefeli mitihani ya mwisho ya chuo kikuu wengi huzani kufeli mtihani ndio mwisho wa mafanikio yao. lakini ipo tofauti kwani "KUSHINDWA NDIO NJIA KUBWA YA MAFANIKIO" maana ya kushindwa si kukata tamaa ila kushindwa ni ujumbe unaopewa wa kuwa hicho ulichokuwa unakifanya hakitakusaidia fanya jambo jingine. kila aliefanikiwa kwenye jambo lolote alishindwa mara nyingi lakini mwisho wa safari yake kwa kuwa hakukata tamaa anaenda kufanikiwa.

Mfano MH.JAKAYA MRISHO KIKWETE mwaka 1995 aliingia katika kinyang'anyilo cha kuwania urais lakini alijikuta anaanguka vibaya, KIKWETE angeamua kukata tamaa sizani kama leo angetufikisha hapa tulipofika na sizani kama leo hii KIKWETE angekuwa na heshima aliyonayo kwenye taifa hili kumbe kikubwa ni kutokukata tamaa kujaribu na kujaribu. maana KIKWETE aliposhindwa alikaa akafikili kwanini ameshindwa mwisho alirekebisha alipokosea akasimama, akagombea tena kwa KASI, HALI na NGUVU MPYA
nyerere%252Bpic.jpg

ndoto zetu mara nyingi hushindwa kutimia kwa sisi wenyewe kukata tamaa mwanzo tu wa safari, ukiamua kuanzisha safari hakikisha unaandaa mpango utakao kufikisha salama katika hiyo safari, ndio maana waliotengeneza magari kwa kutambua kuwa kutakuwa na ajali waliweka vipunguza mwendo {breack} yote ni kuhakikisha wanadhibiti mwendo pindi uwapo mkubwa ili kuzuia ajali. vivyo hivyo kwenye safari ya kutimiza ndoto zako hakikisha unabuni mbinu zitakazo kuinua pindi utakapo anguka. maana ata mtoto mdogo mara nyingi huanguka pindi ajifunzapo kusimama ila mwisho wa yote mtoto hujikuta anatembea.
baby_milestone_learning_to_walk.jpg

wengi tunashindwa kutambua kuwa ili tufanikiwe tunaitaji watu wa kutushika mkono na kutuongoza kule tunapo pahitaji. kamwe huwezi kufanikiwa kwa kuwazarau wengine. kumbuka huyo unae mzarau pengine ndie aliyekuwa daraja la kukuvusha kule ulikokuwa unapahitaji. ndio maana MUNGU hakumuumba mtoto peke yake bali aliwaumba wazazi kisha akawafundisha kugusanisha viungo vya uzazi baadae mtoto akatokea wakamlea kwa uangalizi mkubwa hadi mtoto anakuwa mtu mzima kama tokea upo mdogo ulikuwa chini ya uangalizi maalum ata kwenye mafanikio yako pia unatakiwa uwe chini ya uangalizi maalum.
first_steps03.jpg

hakikisha unaandika ndoto ziorodheshe ata kama una ndoto zaidi ya tano {5} hakikisha unaziorodhesha sehemu, ukisha ziorodhesha zihifadhi ndani kabisa uvunguni mwa moyo wako. unajua vitu vingi vinavyotuumiza ni vile tulivyovihifadhi ndani mwa mioyo yetu. hivyo ndoto zako zote hakikisha unazihifadhi ndani ya moyo wako. kitu chochote kilichohifadhia moyoni huwa hakifutiki, lengo hasa la kuhifadhi ndoto za mafanikio yako moyoni ni ili kuhakikisha kila siku unakukumbuka.
10194277-Businessman-deep-in-thought--Stock-Vector-thinking-man-cartoon.jpg

hakikisha unakuwa karibu sana na watu wenye muonekano wa jinsi unavyohisi na wewe utakuja kuwa baada ya ndoto zako kutimia, kama una ndoto za kuwa mwanasheria mkubwa hakikisha unakuwa karibu na wanasheria, kama ndoto zako ni kuwa mfanyabiashara mkubwa hakikisha unatafuta urafiki na wafanyabiashara wakubwa. kwa kufanya hivyo itakusaidia kujua mbinu walizotumia kufikia pale walipofika. hakikisha unahifadhi mambo yao mema yote waliyoyafanya kufika pale walipofika, epuka sana kuzungumza mafanikio ya yeyote kwa ubaya ata kama unajua kuwa eddy_mhando ni mfanyabiashara lakini ni jambazi usimseme kwa ujambazi wake ila fuata vile anafanya biashara zake na akafanikiwa kwa kumsema kwa ujambazi utakuwa unajijengea uoga ambao utakuja kuzuia ndoto zako kutimia.

Najua pengine unapenda kuwa mwanasiasa mkubwa lakini wanasiasa hao hao miongoni mwa unaowapenda wanahusishwa na vitendo vya ufisadi sasa usiangaike kujua kwanini ni mwanasiasa mzuri lakini anajihusisha na ufisadi unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unafuata zile atua zake nzuri zilizomfikisha pale huyo mwanasiasa {usiangalie ufisadi wake} pengine kuna wanaomshutumu ili wamchafue.
DeepThoughts.jpg

jikubari na jenga imani kuwa vyovyote iwavyo unaweza kufikia pale moyo wako unapotaka. kikubwa hakikisha umwabii mtu kile unachowaza. maana siri ina nguvu kubwa ya kukufikisha pale unapopataka na kutoa siri kuna nguvu kubwa sana ya kuzuia kufika pale unapo pataka, hivyo ili ufike unapotaka hakikisha ndoto zinakuwa siri yako usimwambie mtu yeyote yule.

ITAENDELEA. hayo ni maneno ya eddy_mhando
 

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
6,725
2,000
ASANTE KWA USHAURI WAKO KUNA KITU NIMEKIGUNDUA BAADA YA KUSOMA HII POST...UBARIKIWE SANA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom