Ulipokuwa mtoto ulitamani ukiwa Mkubwa uwe nani?

Dadavua mkuu. Bwana yaani?
... huyo bibi, enzi zile, alikuwa tishio mtaani kwetu! .... kiasi 'fantasies' zangu zote zilikuwa ni mapenzi mazito baina yetu!

Mbaya zaidi na yeye akajua, kiasi kila tukikutana naye hadi leo huwa anacheka sana!

UKWELI NI KUWA MZURI NI MZURI TU!

YAANI MPAKA SASA BADO NAHISI BIBI YULE ANA KITU NINAKIMISS!
😅

ACHA MAPENZI YAITWE MAPENZI!
 
Wakuu,

Leo ni Siku ya Watoto Duniani! Ulipokuwa mtoto, ulitamani kuwa nani?

Je, umefikia ndoto zako, au bado unazifanyia kazi?

Kumbuka, ndoto za watoto ni halali na zinaweza kutimia! Tuendelee kujenga mazingira yanayowawezesha watoto wetu kufanikisha ndoto zao
Niwe sheikh, ulamaa mkubwa na pia niwe msomi . Kwa bahati Ulamaa na usheikh sijaupata
 
Wazazi wengi zamani walikua hawana upeo na elimu kama sasa.
Hivyo vijana wengi wa 1995 kurudi nyuma hawaku pata bahati za kuandaliwa na wazazi wao kua nani/flani.
Miaka ile ilikua ni ukiwa nje ya 10 bora ni kipigo nyumbani, na usipo enda shuleni na kifagio na kidumu ni kipigo shuleni.
Yaani miaka ile watoto walijengewa hofu kuliko kujitambua na kuandaliwa kuwa somebody.
Ile miaka haya ushauri vijana hawakupata kutokana na mpenzi yao ama kuchagua course zipi wakasomee ama waombe ili wawe nani/flani.
Watoto wa Gen Z wanaraha sana.
 
Wakuu,

Leo ni Siku ya Watoto Duniani! Ulipokuwa mtoto, ulitamani kuwa nani?

Je, umefikia ndoto zako, au bado unazifanyia kazi?

Kumbuka, ndoto za watoto ni halali na zinaweza kutimia! Tuendelee kujenga mazingira yanayowawezesha watoto wetu kufanikisha ndoto zao
Nilikuwa nawazaga kuwa daktari siku mzee mmoja akanipeleka kule wanakojifunzia madaktari kwa ile miili ambayo imekoswa ndugu toka Ile siku sitaki tena kusikia hzo habari
 
Nilitamani kuwa Afisa mtendaji wa kijiji,kipindi hicho wanaitwa makatibu wa vijiji.

Kilichofanya nimpende ni kwamba yeye ndiye aliyekuwa na baiskeli kijiji kizima inayoitwa Hamilton.

Huku akimiliki redio ya Santuri akiwa ndiye mwenye maisha mazuri kijiji kizima.

Hakika alikiwa Role model wangu eti😂😂
 
Back
Top Bottom