Kijana Fred...

Kijana Fred...

mr vata

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2017
Posts
465
Reaction score
617
Jioni moja ya mwaka 2015 nikiwa ofisini kwangu kariakoo nilipokea mteja. Alikua kijana wa kisasa, alivalia pensi (sio kaptula) nzuri tshirt na raba, pia alivaa miwani ya jua. Baadae nikaja kufahamu kuwa kijana anaitwa Fred!

Tukiwa tunaendelea kuongea kama mtoa huduma na mteja wake nikakerwa na tabia ya huyu mteja wangu kuongea nami muda wote pasi na kuvua miwani yake. Nikahisi dharau. Nilipomuuliza akasema kuwa anaumwa macho, nikaridhika tukaendelea.

Shughuli iliyomleta kijana Fred ofisini kwangu haikuisha siku ile, hivyo ikabidi aondoke huku tukibadilishana namba za simu ili tuendelee kuwasiliana kwa ajili ya kazi. Baada ya siku mbili kupita kijana akanipigia simu na kunijulisha kuwa amelazwa hivyo atampa rafiki yake namba zangu ili tuwe tunawasiliana kama kazi itakua tayari aifuate. Ikawa hivyo.
Bahati nzuri ile kazi ikakamilika kabla kijana hajatoka hospital japo alikua ananipigia mara chache chache na nilipokua namuuliza shida nini alikua ananiambia kuwa jicho linamsumbua. Yule rafiki akafanya malipo na kuichukua.

Baada ya kupita wiki kadhaa kijana akaja ofisini, muda kama ule ule wa siku ya kwanza. Alikua smart na mchangamfu kama siku zote ila mara hii kulikua na bandeji kwenye jicho lake moja ambapo kama kawaida yake hakuacha kuvaa ile miwani yake ya jua.

Pamoja na kumpa pole pia tukaongea mambo kadhaa pia akanieleza dhamira ya kilichomleta pale kwangu kwa mara nyingine. Kwa kifupi tulijenga kama urafiki japo ni kwa muda mfupi.

Baada ya siku ile ikapita wiki kijana sikumuona na pia hakunipigia na tulikua na ahadi ya kufanya kazi flani. Moyoni nikahisi labda kijana hajapata pesa na kashindwa kuniambia, nikasema wacha nimchuki whatsapp.

Wakati natafuta jina lake ili nimtumie ujumbe nikaanza kukutana na jina la yule rafiki ake ambae alinipa namba yake, na kilichonivuta ni kuona ameweka picha ya Fred kwenye profile yake. Nilipokua naangalia zaid nikakutana na maneno R.I,P Fred. Nikashtuka!

Ikabidi nimpigia yule kijana na kitu alichoniambia nikahuzunika na kushangaa sana.

Kumbe Fred alikua na kansa ya damu! Kipindi nilichokutana nae alikua kwenye hatua za mwisho na kipindi alicholazwa kumbe alitolewa jicho kabisa.

Nikahuzunika sana kumpoteza rafiki niliejuana nae kwa kipindi kifupi. Pia nilishangaa kwa sbb kijana yule alikua anajua kila kitu. Alijua kuwa anakaribia kufa lakini bado alikua jasiri, mchangamfu na asie na hofu. Leo nimemkumbuka kijana Fred.

R.i.p rafiki.
 
daaaah maisha kama sarakasi tu
 
SAD STORY.
Huwa sipendi kusoma story za kuumiza nafsi yangu yaan kwa hii nimemaliz siku yangu vibaya.
 
Kuna watu mnchekesha sana. Sasa mtu akivaa miwani ni dharau gani?
Anyways sad story.
 
R.I.P
 
Back
Top Bottom