Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi, Kenani Kihongosi, amewaonya vijana kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kushangilia vifo, na amesisitiza umuhimu wa kulinda amani na mshikamano wa taifa.
Akizungumza katika ziara yake, Kihongosi alisema vijana ni nguvu ya taifa na wanapaswa kutambua na kulinda urithi wa nchi uliopatikana kupitia juhudi za wazee waliopigania uhuru na utulivu.
Aliwataka vijana kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha mshikamano wa jamii, akisisitiza kuwa kifo ni sehemu ya maisha na hakipaswi kufanywa kuwa jambo la kushangiliwa.
Aidha, alihimiza kulinda mafanikio ya serikali na kuchangia maendeleo ya nchi, huku akieleza kuwa chama kitaendelea…