Kihiyo wa CCM na plan B(UTAPELI) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kihiyo wa CCM na plan B(UTAPELI)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PrN-kazi, Jul 20, 2012.

 1. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Aliye wahi kuwa mbunge wa Temeke kupitia tiketi ya CCM Mh. Ramadhan Ally Kihiyo na baadaye kuenguliwa katika nafasi kwa tuhuma za kuwa na vyeti feki; anatuhumiwa kwa kesi ya utapeli(wizi)

  Kihiyo alifikishwa polisi(kituo cha polisi Usalama-Changombe) ijumaa ya tarehe 14 Julai akidaiwa kutapeli gari dogo(toyota-sprinter), iliyosemekana awali aliikodi kutoka kwa kijana mmoja jina linaifadhiwa kwa nia ya kulitumia kwa muda wa siku 5 kwa makubaliano ya kumlipa sh.elfu 70 kwa siku, kabla ya hizo siku 5 Kihiyo alikuwa akimkodi kijana huyo na kumzungusha mjini akimwambia ana majukumu mazito ya chama na ukizingatia kuwa ni Mbunge mstaafu basi huyo kijana alimwamini sana na ndo maana ilifika atua akamwachia gari kwa makubaliano ya kuja kumlipa sh. 350,000: cha kushangaza muda wa makubaliano ulipofika Kihiyo alianza kupiga chenga mara akipigiwa simu hapokei na hata akipokea anatoa majibu mafupi na kwa ukali, kitendo kilichomwongezea kijana huyo wasiwasi na kulazimika kwenda polisi.

  Kihiyo alipofikishwa polisi, alitoa maelezo na kutakiwa kuingia mahabusu huku akiambiwa aonyeshe gari ilipo; lakini cha kushangaza mapolisi haohao walijitolea kumdhamini na mpaka sasa hivi yuko nje kwa dhamana ya mapolisi lakini gari halijulikani liliko na Kihiyo ametoa taarifa kuwa amepata msiba hivyo yuko safarini.

  My take: iweje Polisi wakubali kumdhamini mtu mwenye dalili zote zinazoashilia kuwa kuna wizi umetendeka?
  Na kwanini hakuamurrishwa aseme wapi alipeleka hilo gari?.
   
Loading...