PreGE2025 Kihenzile: Serikali yaanza Ujenzi wa Meli kubwa ya Mizigo Tani 3,500, Urefu zaidi ya Uwanja wa Mpira Ziwa Tanganyika

PreGE2025 Kihenzile: Serikali yaanza Ujenzi wa Meli kubwa ya Mizigo Tani 3,500, Urefu zaidi ya Uwanja wa Mpira Ziwa Tanganyika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema Serikali imeanza ujenzi wa meli kubwa ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,500 katika Ziwa Tanganyika, ikiwa ni hatua kubwa ya kuimarisha usafiri wa majini na biashara katika eneo la Maziwa Makuu.

Kihenzile amesema:
"Meli hii itakuwa kubwa zaidi ya uwanja wa mpira, yenye urefu wa mita 124 na uwezo mkubwa ambao haujawahi kushuhudiwa katika mwambao wetu wa Maziwa Makuu."

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesisitiza kuwa mradi huo ni sehemu ya mpango mpana wa Serikali wa kuboresha miundombinu ya usafiri majini ili kuchochea uchumi wa mikoa inayozunguka ziwa hilo na nchi jirani.

 
Bonge la meli.watu mnakunywa,mnacheza tennis ma helicopter humohumo
 
Back
Top Bottom