Kigoma wanapenda upinzani,lakini kwanini wanageukwa?

Kigoma wanapenda upinzani,lakini kwanini wanageukwa?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,941
Reaction score
51,063
Kwa kawaida tangu uchaguzi wa kwanza wa Mwaka 1995 ulioshirikisha vyama vingi, Mkoa wa Kigoma umekuwa ni lazima utoe Kiongozi wa kisiasa toka vyama vingine tofauti na CCM wa kuchaguliwa na wananchi. Lakini kila wakati wanasiasa wa kutoka mkoa huo huachana na upinzani na kujiunga na CCM.

Hii tabia ya wanasiasa wa Kigoma kuwageuka wananchi wa mkoa huo wanaowachagua kila kwenye uchaguzi Mkuu ama uchaguzi mdogo chanzo chake ni nini hasa? Maana inavyoonekana wana kigoma hawaitaki CCM bali wanasiasa wa mkoa huo ndiyo huitaka CCM kwa kupitia upinzani. Ni kama vile wanaomba kuchaguliwa kupitia vyama vingine ili mwisho wa siku wajiunge CCM.

Wanasiasa wa Kigoma wana matatizo gani yanayosababisha kila wakati kuwageuka wana Kigoma kwa kujiunga na CCM inayokataliwa na wananchi hao kwenye kila chaguzi?
 
Kwa kawaida tangu uchaguzi wa kwanza wa Mwaka 1995 ulioshirikisha vyama vingi, Mkoa wa Kigoma umekuwa ni lazima utoe Kiongozi wa kisiasa wa kuchaguliwa na wananchi. Lakini kila wakati wanasiasa wa kutoka mkoa huo huachana na upinzani na kujiunga na CCM.

Hii tabia ya wanasiasa wa Kigoma kuwageuka wananchi wa mkoa huo wanaowachagua kila kwenye uchaguzi Mkuu ama uchaguzi mdogo chanzo chake ni nini hasa? Maana inavyoonekana wana kigoma hawaitaki CCM bali wanasiasa wa mkoa huo ndiyo huitaka CCM kwa kupitia upinzani. Ni kama vile wanaomba kuchaguliwa kupitia vyama vingine ili mwisho wa siku wajiunge CCM.

Wanasiasa wa Kigoma wana matatizo gani yanayosababisha kila wakati kuwageuka wana Kigoma kwa kujiunga na CCM inayokataliwa na wananchi hao kwenye kila chaguzi?
Wanasiasa wa kigoma njaa zimewajaa wengi ni wachumia tumbo...pia wananchi wa kigoma hubadilishwa mawazo kwa siasa nyepesi ni wepesi kubadilishwa msimamo wao ndomana mbunge D alikua chama tawala hakufanya kitu wakampga chini ila yuleyule ambae alifanya madudu karudi wakampa...wakamwamini bwana MCL ila njaa zake zkamfanya ahamie chama tawala...ndomana wanatangatanga wala si kwamba wanapenda upinzani ila wanatapatapa
 
ndomana wanatangatanga wala si kwamba wanapenda upinzani ila wanatapatapa
wanaotanga tanga ni wananchi ama ni wanasiasa wa Kigoma. Maana wananchi wao kila wakati wanachagua wapinzani.
 
wanaotanga tanga ni wananchi ama ni wanasiasa wa Kigoma. Maana wananchi wao kila wakati wanachagua wapinzani.
Wananchi ndio hutangatanga baada ya kukosa viongozi thabiti mf.mbunge wa jimbo fulan la ksl mjin ni wa chama tawala lakn ushindi wake ulikua wa zengwe zilizokua wazi ambazo mpinzani wake ambae alikua former Mp na kwasasa kahamia chama tawala angekua makin kipndi cha uchaguzi angemshinda......angalia hii viongoz wanaaminiwa ila wakikosa uongozi wanawakimbia mnabaki kama firanga mlokosa mama mnabaki kutangatanga ndo issue inayowatafuna wananchi wa kigoma
 
Back
Top Bottom