Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 726
- 953
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) leo Machi 18, 2025, imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara ya Kasulu - Kabingo yenye urefu wa Kilometa 260, inayotekelezwa kwa awamu nne (Lot 1 - Lot 4) kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 400.
Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Augustine Vuma, amesema kamati imejiridhisha na maendeleo ya ujenzi huo, ambao umefikia asilimia 83.
Ameeleza kuwa ujenzi wa loti zote nne kwa wakati mmoja katika mkoa mmoja ni jambo la kipekee, na ameitaka Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, ameeleza kuwa, miradi hiyo inagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambapo mikataba ilisainiwa kati ya mwaka 2020 na 2022, na muda wa utekelezaji umepangwa kuwa miezi 36 kwa kila loti.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), utekelezaji wa ujenzi wa barabara hizo umeendelea kwa viwango tofauti. Barabara ya Kasulu - Manyovu yenye urefu wa kilomita 68.25 imefikia asilimia 84.63 na inatarajiwa kukamilika Mei 30, 2025. Ujenzi wa barabara ya Kanyani Junction - Mvugwe yenye urefu wa kilomita 70.5 umefikia asilimia 75.38 na unatarajiwa kukamilika Oktoba 30, 2025.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha, ujenzi wa barabara ya Mvugwe - Nduta Junction yenye urefu wa kilomita 59.35 umefikia asilimia 90.75 na utakamilika Mei 7, 2025. Kwa upande wa barabara ya Nduta Junction - Kabingo yenye urefu wa kilomita 62.50, ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100.
Miradi hii ya barabara inatarajiwa kuimarisha uchumi wa mkoa wa Kigoma kwa kuboresha usafiri wa ndani na wa kimataifa, kwani barabara hizo ni sehemu ya mtandao wa ushoroba wa Magharibi unaounganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kamati ya PIC imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi hii muhimu, ambayo imesaidia kuondoa vumbi katika barabara za Kigoma na kurahisisha usafiri wa wananchi