Kigoma: Mkuu wa Wilaya ya Kasulu avuliwa ukuu wa wilaya na kurudishwa kazi ya awali jeshini

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
IMG_20160902_070425-750x375.jpg

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi, ameondolewa katika wadhifa huo na kurejeshwa katika Makao Makuu ya Jeshi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu (DAS), Titus Mughuha amethibitisha kutokea kwa hatua hiyo ambapo amesema, Kanali Mkisi alitoa taarifa za uhamisho huo katika Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na kusema kuwa, anarejea makao makuu ya jeshi alikokuwa awali kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

‘Ni kweli Kanali Martin Mkisi amepata barua ya kurudi makao makuu ya jeshi, uhamisho huo ni wa kawaida na haupaswi kuhusishwa na uzushi ama sababu zozote,” alisema Mughuha.

Kutokana na mabadiliko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani humo, Kanali Marko Gaguti, atakaimu nafasi hiyo hadi uteuzi mwingine utakapofanyika kujaza nafasi hiyo.

Kanali Martin Mkisi amedumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi tisa, akitokea Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), kutokana na uteuzi wa Rais, Dk. John Magufuli kwa wakuu wa wilaya 139 alioufanya Juni, mwaka jana.

Maoni yangu;
Hivi majeshi hizo kadi za chama wanazimiliki kwa chama tawala tu ukiwa mpinzani utaachwa jeshini?
 
Ndio Huyo mpiganaji hatari alipigana vita Uganda huyo na Akabaki kule muda mrefu tu akifunza upambanaji. Kifaa kikali cha jeshi hicho anapenda jeshi huyo acha tu.Ukimtizama usoni Kama mwamunyange haonyeshi Kama mpambanaji akiingia vitani ndipo utamjua yeye nani
Mkisi ajapigana vita vya Uganda bana Ata kama hatupo Bongo siyo lazima tusijue yanayoendelea na yaliotokea labda baba ake yule alikua mkuu wa Jkt by then, mkisi jr ni kabaisaa kama mr blue anatembelea nyota ya baba. Am standing for correction.
 
Martin hawajamloga huko na kumlaza nje? Nilisikia kuna mkuu mmoja wa wilaya wamemfanya mbaya sana yeye pamoja na dereva wake.
Aliwazalo mjinga ndilo linalomtokea.
Mwenzio hana mawazo ya kulazwa nje na kazi alikuwa anapiga kama kawa
 
Ndio Huyo mpiganaji hatari alipigana vita Uganda huyo na Akabaki kule muda mrefu tu akifunza upambanaji. Kifaa kikali cha jeshi hicho anapenda jeshi huyo acha tu.Ukimtizama usoni Kama mwamunyange haonyeshi Kama mpambanaji akiingia vitani ndipo utamjua yeye nani
Aliyepigana vita ni baba yake huyu mkuu wa
wa wilaya sio km yeye ndio aliyepigana wewe kama huamini piga hesabu kuanzia 1978 vita ilipoanza mpaka leo ni miaka mingapi?ni miaka 39 tangu vita itokee sasa tufanye ndio huyu kapigana hyo vita na alikuwa na miaka 20 kipindi hicho kwahyo sasa hv huyo kamanda ana miaka 59 kwa unavyomuona ashafika hyo miaka?
 
Ndio Huyo mpiganaji hatari alipigana vita Uganda huyo na Akabaki kule muda mrefu tu akifunza upambanaji. Kifaa kikali cha jeshi hicho anapenda jeshi huyo acha tu.Ukimtizama usoni Kama mwamunyange haonyeshi Kama mpambanaji akiingia vitani ndipo utamjua yeye nani
Naambiwa hata akipigwa risasi inadunda!!!
Daah!!!
Uthibitisho tafadhali
 
Back
Top Bottom